Barua ya wazi kwa marais wa EAC na Issa Shivji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa marais wa EAC na Issa Shivji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Binti Maria, Jan 4, 2008.

  1. B

    Binti Maria Senior Member

    #1
    Jan 4, 2008
    Joined: Jun 26, 2007
    Messages: 159
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Sijui kama mmeshaiona hii barua ya Issa Shivji kuhusu yaliyotokea na yanayoendelea kutokea Kenya. Soma jinsi huyu Profesa mahiri na mzalendo alivyomkoma nyani gladi. Hamumunyi maneno, anaweka vitu hadharani. Haya jisomee sasa mwenyewe.
    _______________________________________________________________

    2-01-2008

    Barua ya wazi kwa Marais Kikwete, Kagame na Kiguta juu ya hali ya Wakenya

    Waheshemiwa Marais:

    Ninashindwa kuwasalimia kwa kheri za mwaka mpya. Katika eneo letu hili la Afrika, hakuna heri, kuna shari tu. Waafrika wenzetu huko Kenya wanakufa bila sababu. Sababu ni moja tu – uchu wa madaraka. Inanishangaza sana kwamba nyie kama viongozi wa nchi za Afrika zinazoshirikiana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye lengo la kujenga msingi wa Shirikisho la Afrika, mko kimya. Hi sio wakati wa kucheza mchezo wa kidiplomasia. Hatutaki, hatutaki kabisa kuona tena jangwa la mauaji ya halaiki yatokee barani Afrika. Tumechoka kuona wanaadamu, Waafrika wenzetu, wakiuawa kama wanyama mitaani na hao wanaojiita eti vyombo vya usalama. Usalama wa nani kama sio wa wananchi?

    Jukumu la awali kabisa la vyombo hivyo ni kulinda usalama wa raia; kutuliza ghasia sio kuchochea ghasia au chuki. Wakiwakuta waandamaji bila silaha wawalinde, wawashauri kufanya maandamano yao kwa amani, wawapatie nafasi ya kuonyesha madukuduku yao kuhusu uchaguzi. Uchaguzi wa rais na wananchi kutokuridhika na jinsi ulivyoendeshwa ni suala la kisiasa, sio la kivita. Kama wananchi wana hisia za dhati kabisa kwamba watawala wameiba kura, wamepokonya haki yao ya kuchagua viongozi wao, wanahaki kabisa kuonyesha hisia zao. Kuwazuia wahalifu ni sawa; kuwazuia wezi ni sawa, lakini kuwaua wananchi wa kawaida kabisa kwa sababu wameandamana au wanaelekea kwenye mikutano ya kisiasa ni dhuluma. Haikubaliki na tusikubali kamwe. Kutawala sio haki ya kuzaliwa ya mtu fulani, au rika fulani, au ukoo fulani, au kabila fulani. Ni chaguo la wananchi.

    Sasa nyie viongozi wetu mmesema nini kuhusu hali hio? Kwanza, kuhusu uwizi wa kura wa waziwazi kabisa. Mkikaa kimya maana yake mnamuoneya haya mwenzenu mtawala hata kama anatawala kwa mabavu bila ya ridhaa ya wananchi. Pili, mkikaa kimya juu ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya usalama kwa niaba ya mtawala haramu, mnaweka mfano mbaya mno na mfano huo unaweza ukaugeukia kwenu, na kwetu pia. Tatu, mkifikiri kwamba jambo hili ni jambo la kidiplomasia, jambo la kusuluhisha chinichini au katika faragha ya Ikulu, mnachanganya jambo la msingi la haki ya wananchi kuishi na kujitawala, na mambo ya kiitifaki. Tumieni, mkitaka, lugha zenu za kidiplomasia. Tumieni njia zozote zinazowezekana kutuliza hali ya nchi hiyo ili wananchi wasiona hatia wasiendelee kupoteza maisha yao. Lakini kamwe msikubali utawala wa mabavu bila ya ridhaa ya wananchi.

    Juu ya jambo hili la utawala wa mabavu, ukiwa wa kijeshi au wa kiraia wa uwizi bila ya ridhaa ya wananchi, semeni kwa sauti kubwa bila kutafuna maneno. Mkishindwa kufanya hivyo, sisi raia hatutawaelewa.

    Wananchi wanataka amani; wao ni wa kwanza kutaka na kulinda amani. Lakini amani halisi hujengwa katika msingi wa haki, haki ya kisiasa na haki ya kijamii. Suala sasa ni nini la kufanya? Kwa maoni yangu, kama raia wa kawaida, naona hatua zifuatazo (katika lugha na njia mtakayaona inafaa kidiplomasia) zinaweza kuchukuliwa mara moja:

    Mosi, iwekwe wazi kabisa kwamba nchi zetu hazikotayari kutambua utawala wowote ule ambao uhalali wake unatiliwa shaka na wananchi na watazamaji na watu wa kawaida ambao walikuwa wanafuatilia uchaguzi huu wa Kenya.

    Pili, Mwai Kibaki awaamrishe mara moja jeshi na polisi wake kutokutumia silaha zozote za moto kuwatuliza wananchi isipokuwa pale to ambapo hakuna njia nyingine yoyote ya kutuliza machafuko.

    Tatu, Kibaki akubali moja kwa moja bila masharti, kamati ya uchunguzi ulioteuliwa na Marais wa Afrika Mashariki wakishirikiana na Umoja wa Afrika, kuchunguza uchaguzi wa rais na kusimamia kuhesabiwa kura tena (recount) na kutangazwa hadharani.

    Nne, wagombea urais wote kwa pamoja na mbele yenu wakubali kwa maandishi kwamba yeyote atakayeonekana ameshinda urais baada ya kura kuhesabiwa:

    a) Maramoja ataunda serikali ya umoja wa kitaifa na rais na mawaziri waapishwe kwa wakati moja;

    b) Ataliitisha Bunge na kupendekeza Azimio itakayoweka taratibu za Rais na Baraza la Mawaziri kuapa kwamba watailinda, kuikuuza na kuiendesha serikali ya umoja wa kitaifa kwa maslahi ya taifa bila kujali itikadi za chama, na kwamba kamwe hawatatumia ukabila, kwa vitendo au maneno, kama njia, chombo au jinsi ya kubaki katika au kugombea vyeo vya kisiasa. Serikali ya umoja wa kitaifa iendelee mpaka uchaguzi mkuu ujao.

    Haya ni hatua za kisiasa; sio za kisheria. Zikikubalika kisiasa, njia za kitaalamu za kisheria zinaweza kubuniwa. Msikubali visingizio vya kisheria. Makubaliano ya awali, na yaliyo magumu, ni ya kisiasa. Sheria inafuata siasa, sio kuitangulia.


    Wenu,

    Raia Issa Shivji

    Mwananchi 03-01-2008
     
  2. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #2
    Jan 4, 2008
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 31,362
    Likes Received: 6,393
    Trophy Points: 280
    Ni utawala gani wa mabavu wenye ridhaa ya raia?
     
  3. BAK

    BAK JF-Expert Member

    #3
    Jan 4, 2008
    Joined: Feb 11, 2007
    Messages: 70,687
    Likes Received: 82,538
    Trophy Points: 280
    M7 ni dikteta ambaye alibadilisha katiba ili kukidhi matakwa yake ya kuendelea kuwa madarakani. Huyu wa kwetu naye tunajua historia ya chama chake kuhusiana na wizi wa chaguzi. Sidhani kama wataweza kusema lolote la maana katika hali hii, na kama wakisema basi watakuwa upande wa fisadi Kibaki.
     
  4. D

    DAR si LAMU JF-Expert Member

    #4
    Jan 4, 2008
    Joined: Mar 31, 2007
    Messages: 2,942
    Likes Received: 286
    Trophy Points: 180
    ..aliyoyasema shivji yamesemwa na wengi,na bado hayajaoneka ya maana au yameingia hapa yametokea kulee!

    ..tuendelee kushuhudia genocide nyingine east africa,mpaka pale mito itakapo tiririka damu na maziwa kujaa miili ya binadamu ndipo tutang'amua nini kimetokea!

    ..kwasasa usingizi ni mtamu bado!
     
  5. BAK

    BAK JF-Expert Member

    #5
    Jan 4, 2008
    Joined: Feb 11, 2007
    Messages: 70,687
    Likes Received: 82,538
    Trophy Points: 280
    Posted Date:: 04.01.2008 @01:29 EAT

    Museveni congratulates Kibaki on election 'win'
    KAMPALA
    THE CITIZEN

    Ugandan President Yoweri Museveni has congratulated Kenyan President Mwai Kibaki on his disputed re-election, in the first endorsement by a fellow African leader.

    The silence by most African leaders after Kibaki was declared the election winner has underlined concerns over alleged rigging of the vote, which has been followed by a week of violence.

    "President Museveni telephoned President Kibaki to congratulate him on his re-election," said a statement by a spokesman for Museveni, in power since 1986 and himself accused of fraud by the opposition at his 2006 re-election.

    The only other nation to congratulate Kibaki has been the United States -- within hours of his swearing-in on Sunday.

    But U.S. officials have since expressed concerns at election violence and irregularities in the Kenyan vote count.

    A statement from Museveni said that in his capacity as chairman of the five-member East African Community (EAC), he and Tanzanian President Jakaya Kikwete had been in touch with Kibaki and opposition leader Raila Odinga.

    It was not clear if Kikwete, or any other EAC presidents, had formally congratulated Kibaki too.

    They were looking at "the possibility of the community finding an amicable and immediate solution to the problem," the statement said. "The efforts have not yet borne fruit but they are continuing."
    Uganda has closed its border with Kenya for business, but is allowing refugees to cross.

    Uganda's military spokesman, Major Felix Kulayigye, said soldiers had been deployed heavily on the border "to avoid violence spilling over".
    About 1,000 Kenyan refugees have already crossed as the death toll from post-election violence passes 300, according to human rights groups.

    "The government and the International Red Cross have moved in to make sure these people are sheltered well, but for now they are in schools and churches," said Disaster Preparedness Minister Musa Ecweru.

    At the border, no trucks were allowed to cross from either side, on what is usually a bustling trade route. Rotting fish was dumped on the roadside from some vehicles.
     
  6. Pundit

    Pundit JF-Expert Member

    #6
    Jan 4, 2008
    Joined: Feb 4, 2007
    Messages: 3,741
    Likes Received: 25
    Trophy Points: 135
    Shivji ameongea vizuri.

    Lakini pia kama mtu mwenye mizani yenye tarafu napenda kusema kuwa mauaji yanayofanywa na watu wanaosemwa kuwa ni wafuasi wa Raila, ambao inawezekana kabisa ni machakaramu wasio na itikadi zaidi ya ukabila na kufedheheshwa na umasikini hayakemewi kwa kutosha.

    Ingekuwa vizuri kama kungekuwa na usawa katika kukemea maovu na hili swala lisipewe uzito wa kisiasa tu wa kuwasema madikteta na mbwa zao (polisi na washabiki wao) bila kuwasema Wakenya wasio responsible katika upinzani na machokoraa waliojichokea.

    Hata kama umekuwa oppressed, violence is despicable.
     
  7. Azimio Jipya

    Azimio Jipya JF-Expert Member

    #7
    Jan 4, 2008
    Joined: Nov 27, 2007
    Messages: 3,370
    Likes Received: 14
    Trophy Points: 135
    Babu iko na wewe.. Niongezee kidogo tu hapa ...Huyu wa kwetu naye tunajua historia ya chama chake kuhusiana na wizi wa chaguzi.. Huyu wa kwetu ana Ugonjwa wa kutaka kupendwa Kirahisi rahisi na kila mtu. Hana ujasiri wa Kutetea kwa ujasiri chochote ambacho Kinatofautiana na watu wengi. Anaumwa na ugonjwa wa kuhitaji watu wamuenzi..Hawezi kukaa bila Kuhitajiwa na watu..Atakubaliana na chochote hatu Upuzi ilimradi kapigiwa makofi na Kuendeleza mzaha mzaha. He is "a people pleser". Ogopa viogozi wa aina hii! Kamwe hawezi kutofautina kimsingi na upande wenye wafuasi wengi..Atakufa hapo hapo! Hamuwezi M7 hawezi kumpinga kinaganaga..wala usitegemee..M7 ameshaunga mkona matokeo..haoni tatizo lolote!
     
  8. Bin Maryam

    Bin Maryam JF-Expert Member

    #8
    Jan 4, 2008
    Joined: Oct 22, 2007
    Messages: 685
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 0

    BM:

    Shivji amesema kweli kabisa. Cha kukumbuka pia ni kuwa yeye ni raia wa kawaida na hana-responsibility na kila anachosema. Shivji anaweza kumwita Museveni Mbwa Koko au Mchawi na kitu chochote kisitokee.

    Ingawa viongozi wa juu wa Tanzania ni raia wa kawaida, wanayo-responsibility ya kile wanachokisema. JK atakachosema sio chake pekee bali cha nchi anayowakilisha.

    Wako katika kusukuma gurudumu la maisha.

    BM
     
  9. Gamba la Nyoka

    Gamba la Nyoka JF-Expert Member

    #9
    Jan 4, 2008
    Joined: May 1, 2007
    Messages: 6,596
    Likes Received: 6,757
    Trophy Points: 280
    mimi nafikiri wanaweza kufanya yote hayo aliyoyapendekeza Shivji bila kutoa kauli za makemeo kwa kibaki.lengo liwe kumfanya mzee mzima kibaki aone "reason",maana amepotoka, wakimpa mapressure makali na kumbana katika kona mbaya anaweza akageuka dikteta mbaya sana na matokeo yake hali ndo ikawa mbaya zaidi.

    hili la Makemeo na kauli za kutoridhishwa na uchaguzi Kenya linaweza kufanywa vizuri sana "at a ministrial level",na wanadiplomasia wa nchi hizi za maziwa makuu, lakini "at a presidential level" mimi ninaona ni bora zaidi kuhangaikia solution hatua kwa hatua.makaripio na kuzomea sidhani kama ni busara kwa Maraisi wetu kufanya hivyo.
     
  10. M

    Mtanzania JF-Expert Member

    #10
    Jan 5, 2008
    Joined: May 4, 2006
    Messages: 4,818
    Likes Received: 49
    Trophy Points: 145
    Kwanini tume ya uchaguzi hawapewi watu ka Shivji au jaji Kisanga? Hawa hawaogopi mtu na wangefaa kuwa waamuzi.
     
  11. J

    Jasusi JF-Expert Member

    #11
    Jan 5, 2008
    Joined: May 5, 2006
    Messages: 11,484
    Likes Received: 165
    Trophy Points: 160
    Pundit,
    Yale mauaji yaliyofanyika Kisumu yalifanywa nani?
     
  12. K

    Kwaminchi Senior Member

    #12
    Jan 5, 2008
    Joined: Dec 30, 2007
    Messages: 154
    Likes Received: 2
    Trophy Points: 0
    Bwana Issa Shivji ameandika kwa niaba yetu wengi tu. Lakini, si inasemwa kuwa, "ndege wenye manyoya sare, huruka pamoja?" Marais waseme kwa niaba ya nani? Kibaki au wananchi?
     
  13. Kibunango

    Kibunango JF-Expert Member

    #13
    Jan 5, 2008
    Joined: Aug 29, 2006
    Messages: 7,639
    Likes Received: 184
    Trophy Points: 160
    Kwani Tume ya Tz Bara ina matatizo? Au sio huru ka ya Zenj? hivi TZ Bara nako kuna wizi wa kura?
     
  14. A

    Atanaye Senior Member

    #14
    Jan 5, 2008
    Joined: Oct 31, 2007
    Messages: 153
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 35
    Hisia za Kidemokrasia. Aliyoyasema nilishanena, naafikiana na yeye."Ni chaguo la wananchi" hakuna siasa hapo.

    Atanaye Kijiko
     
  15. F

    Fundi Mchundo JF-Expert Member

    #15
    Jan 5, 2008
    Joined: Nov 9, 2007
    Messages: 4,706
    Likes Received: 61
    Trophy Points: 145
    Hivi huyu bwana anaweza kugombea uraisi? Kama Obama anaweza, sisi je?
     
  16. Pundit

    Pundit JF-Expert Member

    #16
    Jan 5, 2008
    Joined: Feb 4, 2007
    Messages: 3,741
    Likes Received: 25
    Trophy Points: 135
    Jasusi, it is reported that police opened fire.I condemn that.The first thing I commented on is my support for Shivji's critical condemnation of the administrations.

    What I did not hear from Shivji and many contributors in this forum is an equally critical condemnation of killings of Kikuyus and government supporters.

    The political dimensions of this hullabaloo should not blunt our sense of justice and adherence to basic decency.Violence is despicable under any clothing.
     
  17. Mnhenwa Ndege

    Mnhenwa Ndege JF-Expert Member

    #17
    Jan 5, 2008
    Joined: Dec 5, 2007
    Messages: 243
    Likes Received: 12
    Trophy Points: 0
    HILI NI SWALI AU UNATUCHOKOZA TUSEME MENGI, AMA TUMUULIZE SWALI HILI MNYIKA WA CHADEMA KATIKA JIMBO YAKE LA UBUNGO
     
  18. Kibunango

    Kibunango JF-Expert Member

    #18
    Jan 5, 2008
    Joined: Aug 29, 2006
    Messages: 7,639
    Likes Received: 184
    Trophy Points: 160
    Hilo ni swali ambalo linahitaji jibu, Iwapo Mnyika au mtu yeyote atakaye weza kunifahamisha itakuwa ni jambo la mbolea zaidi...
     
  19. M

    Masatu JF-Expert Member

    #19
    Jan 5, 2008
    Joined: Jan 29, 2007
    Messages: 3,285
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 135
    Tusianze ku spin hapa hakuna alimuibia kura Mnyika wala nini kashindwa tu and he is a looser big time...
     
Loading...