Kinana alihusika saana kung'oa makucha viongozi waastafu...Wakati hili baraza linaundwa awamu ya jana kama sikosei kulikuwa na minong'ono ya ni kama mbinu za kuwaweka Wastaafu wa ngazi za juu pembeni ili wasitie kauzibe katika vikao rasmi vya chama. Ndio utaona huto tuvifungu twa ajabu twa ushauri unaombwa, unaweza uzingatiwe au upuuzwe na mambo mengine ya juujuuu tu hivi na yasiyo ya msingi. Na fikiri clip itawakumbusha nani ni muumini wa sera za juu juu.
Lakini hujafa hujaumbika Msekwa naye kawajibu kijuu juu kama msingi wa kuanzishwa baraza leyewe ulivyo kusudia. Na msingi utaona ni Wazee Wastaafu washirikishwe kijuu juu tu.
Sasa anahitaji makucha yao yamuokoe hayapo.
Kasahau aliyang'oa yeye