Alimuandikia rafiki yake Horace Waller akisema ."I am terribly knocked up but this is for your own eye only," "Doubtful if I live to see you again." .Alisoma biblia na kusoma mpaka akaanza kuchanganyikiwa bila dalili yoyote ya kuondokana na kukata kwake tamaa.[/url]
Hatimaye barua halisi ya mmishionari David Livingstone imepatikana tena huku London kwenye mnada mmoja miaka 140 tangu aiandike barua hiyo katika hali ya kukata tamaa.
Alimuandikia rafiki yake Horace Waller akisema ."I am terribly knocked up but this is for your own eye only," "Doubtful if I live to see you again." .Alisoma biblia na kusoma mpaka akaanza kuchanganyikiwa bila dalili yoyote ya kuondokana na kukata kwake tamaa.`Katika hali hiyo aliyokuwa nayo ilibidi aombe msaada kutoka kwa waislamu wanaoitwa wafanyabiashara ya utumwa.Alisaidiwa sana na Tippu Tipu kwa kila hali.
Maandishi yake hayo, kulingana na bibi Debbie Harrison, mtafiti katika chuo kikuu cha Birkbeck University cha London yanamfanya atiliwe shaka katika ushujaa aliotajwa nao.Mwaka 1871 mmishionari huyu alikwama kwenye kijiji cha Bambarre huko Kongo na hatimaye kufariki huko Chitambo katika Zambia ya leo mwaka 1873.
David Livingstone letter deciphered at last - Yahoo! News
Adding insult to injury, Livingstone, a crusading abolitionist, had been forced to seek help from Arab slave traders while he waited for outside support
Sijaona bado unataka kusema nini unamuonea huruma au?????????? Nenda muesum za Bagamoyo na Ujiji. Kilichofuata baada ya biashara ya utumwa ni kama biashara hiyo hiyo hiyo lakini kwa utaratibu mwingine.
Hapa ninachotaka uelewe kwanza ni kuwa uislamu ulitangulia kwa mbali kufika Afrika mpaka ndani Kongo.Wakati mara nyingi kuna dharau kwa waislamu na hujuma za kila aina kumbe wakristo wa mwanzo Afrika walifikia mikononi mwa waislamu.Nyinyi hamna shukrani kabisa!.
Kuhusu mada ya biashara ya utumwa humu imejadiliwa mara nyingi lakini nakuhakikishia walion'gang'ania uzushi unaouamini wewe walishindwa na kukimbia.Zamani mwaka 2008 na karibuni kabisa.Kabla hujaamua kuendeleza ubishi wako angalia kule https://www.jamiiforums.com/habari-...abu-wenye-asili-ya-kiafrika-6.html#post934898
usiwe mwepesi wa kuhamaki, harafu mgumua kufikiri, kama usingelikuwa na pupa ungelijua kwanini nimesema tatizo la ilimu madrassa, usikurupuke tu kupost ishu juu ya ulikisoma hata kama hujakielewa. pole lakini kama umekwazwa na hiyo, tafuta elimu na ilimuWewe Anyisile hizo chuki zako zitakupa pressure. Sasa hiyo elimu ya madrassa vina uhusiano gani na kumsaidia Livingstone au hiyo barua yake aliyoandika?
uko sahihi mkuu kuna eneo moja pale Oman linaitwa Zanzibar, na warabu wa pale ni warabu weusi kama waha kabisa, na uarabu wao ni kwa ajili wamezaliwa pale tangu zama, kwa hiyo ni kweli kabisa kuwa hawa ni masalia ya wale waafrika wa kipindi hicho cha utumwa wakajikuta wako settled maeneo yale na kupaita ZanzibarBimkongwe, heshima yako ndugu yangu. Japo kuwa Tipp Tipu hakuuza watumwa ( Labda; sina uhakika kuhusu hili) Wachukuzi wa mizigo yake walikuwa kaka zetu weusi, sasa sijui kama waliajiriwa na Tipp Tipu au walikuwa watumwa au manamba au vip[i. Kwa hali yoyote ile wale wachukuzi walinyanyasika na kuumia vibaya sana hebu fikiria kubeba pembe ya ndovu toka kigoma kwenda pwani ya Tanzania, na hatimaye kwenda kuyapakua unguja au uarabuni. Sijafika uarabuni, bali naambiwa kuwa kuna watu wengi tu weusi kama sisi na nywele zao kipilipili, nadhani hawa ni masalia ya wapagazi hao masikini.
Nakubaliana na wewe kuwa sio kila kitu kichambuliwe kwa mtazamo wa kidini, na kwa kweli sikuona sababu ya mwanzisha mada kuandika kuwa alisaidiwa na waisilamu
Soma kipande kimoja cha maelezo ya Tippu Tip.Ikiwa kuna sehemu hujaelewa nitakusaidia.Ukipenda nitakuletea vipande zaidi.Bitimkongwe,
Hicho kitabu cha Tip tip kiliandikwa na nani mpaka huyu mzungu (I presume) kuja kukitafsiri?
Soma kipande kimoja cha maelezo ya Tippu Tip.Ikiwa kuna sehemu hujaelewa nitakusaidia.Ukipenda nitakuletea vipande zaidi.
hiki nini sasa?
╞ Nalipopata miaka thenashara ,nalishika safari za karibu.Hafanya biashara ya sandarusi pamoja na ndugu yangu Muhammed bin Masud el Wardi na mjomba wangu Bushiri bin Habib wa Abdallah bin Habib el Wardijan.Nachukua bidhaa kidogo,maana kijana.Nao wao ndugu yangu na wajomba wangu wakichukuwa bidhaa nyingi kidogo.Hafanza biashara ya sandarusi mwaka mmoja╡ (12)
Soma kipande kimoja cha maelezo ya Tippu Tip.Ikiwa kuna sehemu hujaelewa nitakusaidia.Ukipenda nitakuletea vipande zaidi.
╞ Nalipopata miaka thenashara ,nalishika safari za karibu.Hafanya biashara ya sandarusi pamoja na ndugu yangu Muhammed bin Masud el Wardi na mjomba wangu Bushiri bin Habib wa Abdallah bin Habib el Wardijan.Nachukua bidhaa kidogo,maana kijana.Nao wao ndugu yangu na wajomba wangu wakichukuwa bidhaa nyingi kidogo.Hafanza biashara ya sandarusi mwaka mmoja╡ (12)
Hili jibu la nani aliandika autobiography ya Tippu Tip lilikwishajibiwa na BintMkongwe hapo juu.Baina ya post yake na yako ni 4posts.Kama wewe ni mtu madhubuti usingepaswa kunijibu mimi tena wala kuniuliza wala kushangaa kwamba hujajibiwa.....and HOW ON EARTH hii inajibu swali langu???
Kama huelewi posts zangu tafwadhaal zione kama kituo cha polisi.
Ni rahisi. Nadhani mleta hoja alikusudiwa kwamba ingawa Livingstone ambaye alikuwa mkristo alitegemewa kusaidiwa na waumini wenzake, alijikuta msaada wa maana anaupata kutoka kwa wenye imani tofauti na yake. Labda hilo linatufundisha kwamba tangu kale haukuwapo ubaguzi kama huu tunaoujenga kwa bidii zama hizi kidini. Mwenye akili na alielewe jambo hili kwa kina na kumsaidia. Kwa misingi hiyo ndio maana waisla na wakristo wanakaa mtaa mmoja majirani na hata kupanga nyumba moja wakisaidianaa kwa kila hali. Sasa wanaoshabikia udini wa kutugawanya wasitupotoshe kumbe hata mamisionari hawakulenga kutugawanya. Tippu Tip aliliona hilo, naye aliangalia maslahi na sio imani zisizo na tija. Ama sivyo angemfanya Livingston adui nambari moja kwa kukataza utumwa. Japo unanifumbua macho leo kwamba Tippu Tip hakuuza watumwa, that is likely kwa sababu aliwatumia watumwa kama malori ya kusomba mizigo yake na sio kama bidhaa.Nakubaliana na wewe kuwa sio kila kitu kichambuliwe kwa mtazamo wa kidini, na kwa kweli sikuona sababu ya mwanzisha mada kuandika kuwa alisaidiwa na waisilamu
Kwa kweli hakuwatumia kama malori ya kusomba mizigo,bali aliwalipa kwa kupatana nao.Na wengi walikuwa wakibeba masafa maalum na kurudi makwao kutumia pesa zao.Ni rahisi. Nadhani mleta hoja alikusudiwa kwamba ingawa Livingstone ambaye alikuwa mkristo alitegemewa kusaidiwa na waumini wenzake, alijikuta msaada wa maana anaupata kutoka kwa wenye imani tofauti na yake. Labda hilo linatufundisha kwamba tangu kale haukuwapo ubaguzi kama huu tunaoujenga kwa bidii zama hizi kidini. Mwenye akili na alielewe jambo hili kwa kina na kumsaidia. Kwa misingi hiyo ndio maana waisla na wakristo wanakaa mtaa mmoja majirani na hata kupanga nyumba moja wakisaidianaa kwa kila hali. Sasa wanaoshabikia udini wa kutugawanya wasitupotoshe kumbe hata mamisionari hawakulenga kutugawanya. Tippu Tip aliliona hilo, naye aliangalia maslahi na sio imani zisizo na tija. Ama sivyo angemfanya Livingston adui nambari moja kwa kukataza utumwa. Japo unanifumbua macho leo kwamba Tippu Tip hakuuza watumwa, that is likely kwa sababu aliwatumia watumwa kama malori ya kusomba mizigo yake na sio kama bidhaa.