Barua ya livingstone yapatikana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya livingstone yapatikana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ami, Jul 3, 2010.

 1. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hatimaye barua halisi ya mmishionari David Livingstone imepatikana tena huku London kwenye mnada mmoja miaka 140 tangu aiandike barua hiyo katika hali ya kukata tamaa.
  Alimuandikia rafiki yake Horace Waller akisema ."I am terribly knocked up but this is for your own eye only," "Doubtful if I live to see you again." .Alisoma biblia na kusoma mpaka akaanza kuchanganyikiwa bila dalili yoyote ya kuondokana na kukata kwake tamaa.`Katika hali hiyo aliyokuwa nayo ilibidi aombe msaada kutoka kwa waislamu wanaoitwa wafanyabiashara ya utumwa.Alisaidiwa sana na Tippu Tipu kwa kila hali.
  Maandishi yake hayo, kulingana na bibi Debbie Harrison, mtafiti katika chuo kikuu cha Birkbeck University cha London yanamfanya atiliwe shaka katika ushujaa aliotajwa nao.Mwaka 1871 mmishionari huyu alikwama kwenye kijiji cha Bambarre huko Kongo na hatimaye kufariki huko Chitambo katika Zambia ya leo mwaka 1873.
  David Livingstone letter deciphered at last - Yahoo! News
   
 2. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hili ndiyo tatizo kubwa la ilimu ya madrassa
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Wewe Anyisile hizo chuki zako zitakupa pressure. Sasa hiyo elimu ya madrassa vina uhusiano gani na kumsaidia Livingstone au hiyo barua yake aliyoandika?
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Sijaona bado unataka kusema nini unamuonea huruma au?????????? Nenda muesum za Bagamoyo na Ujiji. Kilichofuata baada ya biashara ya utumwa ni kama biashara hiyo hiyo hiyo lakini kwa utaratibu mwingine.
   
 5. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Jaribuni kusoma autobiography ya Tippu Tip muone kama alikuwa anafanya biashara ya utumwa au ya pembe za ndovu?

  Yeye alikuwa akifanya biashara ya pembe za ndovu, shanga, vitambaa na vitu vyengine ambavyo vilikuwa na thamani kwa wakati ule. Alikuwa akichukuwa biashara hizo kutoka kwa wahindi Zanzibar na kupeleka huko mabara mpaka Congo na (enzi zile) Ruanda - Urundi.

  Sikuona kwenye kitabu chake akiandika habari ya kuuza watumwa ijapokuwa aliwataja akina Livingstone na Stanley na Wabelgiji wa kipindi kile.
   
 6. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2010
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bimkongwe, heshima yako ndugu yangu. Japo kuwa Tipp Tipu hakuuza watumwa ( Labda; sina uhakika kuhusu hili) Wachukuzi wa mizigo yake walikuwa kaka zetu weusi, sasa sijui kama waliajiriwa na Tipp Tipu au walikuwa watumwa au manamba au vip[i. Kwa hali yoyote ile wale wachukuzi walinyanyasika na kuumia vibaya sana hebu fikiria kubeba pembe ya ndovu toka kigoma kwenda pwani ya Tanzania, na hatimaye kwenda kuyapakua unguja au uarabuni. Sijafika uarabuni, bali naambiwa kuwa kuna watu wengi tu weusi kama sisi na nywele zao kipilipili, nadhani hawa ni masalia ya wapagazi hao masikini.

  Nakubaliana na wewe kuwa sio kila kitu kichambuliwe kwa mtazamo wa kidini, na kwa kweli sikuona sababu ya mwanzisha mada kuandika kuwa alisaidiwa na waisilamu
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  This is what we read from this article..

  Labda mueke source za hizo habari za Tip Tip kutokufanya biashara ya utumwa, ilhali hiyo nickname inasemekana alipewa kufuatia ukatili wake na mlio wa bunduki yake.

  Just enlight us please..
   
 8. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hapa ninachotaka uelewe kwanza ni kuwa uislamu ulitangulia kwa mbali kufika Afrika mpaka ndani Kongo.Wakati mara nyingi kuna dharau kwa waislamu na hujuma za kila aina kumbe wakristo wa mwanzo Afrika walifikia mikononi mwa waislamu.Nyinyi hamna shukrani kabisa!.
  Kuhusu mada ya biashara ya utumwa humu imejadiliwa mara nyingi lakini nakuhakikishia walion'gang'ania uzushi unaouamini wewe walishindwa na kukimbia.Zamani mwaka 2008 na karibuni kabisa.Kabla hujaamua kuendeleza ubishi wako angalia kule https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/62222-waarabu-wenye-asili-ya-kiafrika-6.html#post934898
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Wewe bana acha kutetea ujinga.

  Unaonekana hata hukusoma hiyo article ulioileta.

  Article inasema Livingstone alienda kutafuta msaada kwa Waarabu walokuwa wakifanya biashara za utumwa (yaani kuuza watu kama kuku) ingawa yeye (Livingstone) alikuwa abolitionist. Hii haijustify chochote kwa waarabu wale na biashara zao za kishenzi.
   
 10. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Lunanilo na Abdulhalim, source ya kitabu ni "Maisha ya Hamed bin Muhammed El Murjebi - Tippu Tip, kwa maneno yake mwenyewe (1959), kimefasiriwa kwa kiingereza na W. H. Whitley

  Ni kweli wabeba mizigo walikuwa ni weusi, lakini hiyo ilikuwa kwa kupatana kwa majora ya vitambaa na shanga. Na wengine walikuwa wanakimbia wakiona kazi nzito ijapokuwa walikuwa wameshapewa malipo. Kwa hivyo yalikuwa mapatano ya kibiashara ingawa sisemi kwamba yalikuwa mapatano ya kihalali au la.

  Na ni kweli walikuwa wanapigana na bunduki mpaka akapata jina la Tippu Tip, na kwa enzi zile ilikuwa "ua nikuue", yaani mule wanamopita na misafara yao walikuwa wanapigana na wenyeji na wao kupigwa na hata kunyang'anywa hizo biashara.

  Vile vile hata hao wazungu waliokuwa wanakwenda huko ndani Tanganyika walikuwa wanachukuwa wapagazi hao hao weusi, unadhani wengine wangetoka wapi? Angalia kitabu cha "Safari za Mwinyi Mtoro" ambacho nilikipata humu humu na kukidownload na kukisoma. Mjerumani Von Weissman alichukuwa wapagazi kutoka Zanzibar, Bagamoyo na sehemu nyengine, na wengine aliwachukuwa kutoka Comoro. Na hao akina Livingstone pia walichukuwa wapagazi kutoka Bagamoyo na maeneo ambayo alikuwa anapita. Na maiti yake ilibebwa na "Susi na Chuma" kutoka Kigoma mpaka Zanzibar na sio mtu mweupe.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Bitimkongwe,

  Hicho kitabu cha Tip tip kiliandikwa na nani mpaka huyu mzungu (I presume) kuja kukitafsiri?
   
 12. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hiyo ni "autobiography", yaani aliandika mwenyewe Tippu Tip. Kiswahili chake kwa kweli ni kile chenye asili ya kiarabu na kwa sasa wengi wanaweza wasielewe baadhi ya maneno. Ila ile version ya Kiingereza (ya Whitley) ndio rahisi kusomeka.

  Kitabu chenyewe page moja ni kwa maneno yake na opposite page ndio iko kwa kiingereza.
   
 13. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  usiwe mwepesi wa kuhamaki, harafu mgumua kufikiri, kama usingelikuwa na pupa ungelijua kwanini nimesema tatizo la ilimu madrassa, usikurupuke tu kupost ishu juu ya ulikisoma hata kama hujakielewa. pole lakini kama umekwazwa na hiyo, tafuta elimu na ilimu
   
 14. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  uko sahihi mkuu kuna eneo moja pale Oman linaitwa Zanzibar, na warabu wa pale ni warabu weusi kama waha kabisa, na uarabu wao ni kwa ajili wamezaliwa pale tangu zama, kwa hiyo ni kweli kabisa kuwa hawa ni masalia ya wale waafrika wa kipindi hicho cha utumwa wakajikuta wako settled maeneo yale na kupaita Zanzibar
   
 15. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Soma kipande kimoja cha maelezo ya Tippu Tip.Ikiwa kuna sehemu hujaelewa nitakusaidia.Ukipenda nitakuletea vipande zaidi.


  ╞ Nalipopata miaka thenashara ,nalishika safari za karibu.Hafanya biashara ya sandarusi pamoja na ndugu yangu Muhammed bin Masud el Wardi na mjomba wangu Bushiri bin Habib wa Abdallah bin Habib el Wardijan.Nachukua bidhaa kidogo,maana kijana.Nao wao ndugu yangu na wajomba wangu wakichukuwa bidhaa nyingi kidogo.Hafanza biashara ya sandarusi mwaka mmoja╡ (12)
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  haya yatamfanya mtu aelewe nini, ama ni mafumbo tu?
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  ....and HOW ON EARTH hii inajibu swali langu???

  Kama huelewi posts zangu tafwadhaal zione kama kituo cha polisi.
   
 18. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hili jibu la nani aliandika autobiography ya Tippu Tip lilikwishajibiwa na BintMkongwe hapo juu.Baina ya post yake na yako ni 4posts.Kama wewe ni mtu madhubuti usingepaswa kunijibu mimi tena wala kuniuliza wala kushangaa kwamba hujajibiwa.
  Wasioelewa post zako humu JF sio mimi peke yangu.Nimeona mara nyingi ukibezwa bezwa.Na kwa kweli hueleweki ndio maana ikawa hivyo.Mimi post zako huwa naziona kama jalala sio kituo cha polisi tu, na huwa nazikwepa kuzijibu.Lakini pale niliona kidogo labda umeuliza cha maana na ukijibiwa utaelewa imekuwa yale yale.
  Kwenye hii mada post no.7 umesema."Labda mueke source za hizo habari za Tip Tip kutokufanya biashara ya utumwa, ilhali hiyo nickname inasemekana alipewa kufuatia ukatili wake na mlio wa bunduki yake."
  Kwani mlio wa bunduki ya Tip tip ndio ushahidi kuwa yeye alifanya biashara ya utumwa?.Wewe Abdulhalim tukisikia unalia kwani lazima iwe umefiwa.Yawezekana umezomewa tu kwa upuuzi wako.
   
 19. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ni rahisi. Nadhani mleta hoja alikusudiwa kwamba ingawa Livingstone ambaye alikuwa mkristo alitegemewa kusaidiwa na waumini wenzake, alijikuta msaada wa maana anaupata kutoka kwa wenye imani tofauti na yake. Labda hilo linatufundisha kwamba tangu kale haukuwapo ubaguzi kama huu tunaoujenga kwa bidii zama hizi kidini. Mwenye akili na alielewe jambo hili kwa kina na kumsaidia. Kwa misingi hiyo ndio maana waisla na wakristo wanakaa mtaa mmoja majirani na hata kupanga nyumba moja wakisaidianaa kwa kila hali. Sasa wanaoshabikia udini wa kutugawanya wasitupotoshe kumbe hata mamisionari hawakulenga kutugawanya. Tippu Tip aliliona hilo, naye aliangalia maslahi na sio imani zisizo na tija. Ama sivyo angemfanya Livingston adui nambari moja kwa kukataza utumwa. Japo unanifumbua macho leo kwamba Tippu Tip hakuuza watumwa, that is likely kwa sababu aliwatumia watumwa kama malori ya kusomba mizigo yake na sio kama bidhaa.
   
 20. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli hakuwatumia kama malori ya kusomba mizigo,bali aliwalipa kwa kupatana nao.Na wengi walikuwa wakibeba masafa maalum na kurudi makwao kutumia pesa zao.
   
Loading...