Mzee Masatu,
Ndesamburo alipeleka kesi yake, na Spika alipeleka kesi yake, ninacho kitabu maalum kilichotolewa na bunge hivi karibuni kuhusu hii kesi, ninaweza kukutumia ukitaka at anytime nitakufanyia kopi, na yote ninayoyasema yamo,
baaada ya kutoa uamuzi ndani ya kamati ya bunge, Spika aliipeleka kesi hiyo PCB, kuhusu wabunge waliokula rushwa, na kesi nzima kwa ujumla,
kwangu the big question ni kwa nini Spika hakumwajibisha Malima, baada ya kukubalika kuwa alikuwa amelidanganya bunge la taifa?
Sasa ninaomba niseme, kuwa mimi binafsi mimi nilifikiri wa-Tanzania na hasa wasomi tutaiangalia hii kesi kwa mapana na marefu, na ku-appreciate kuwa at least Tanzania tunaanza kwenda mbali, nani alitegemea kuwa ingekuja siku wa-Tanzania tungeyaona haya? Sasa mambo kama haya ndio yanaweka historia kwa ajili ya taifa letu huko kesho, na hasa katika nyanja ya sheria za bunge, kesho na keshokutwa itakapotokea kesi ya namna nyingine inayofanana na hii hakutakuwa na tatizo,
I do not see the problem ya Malima kwenda CCM, yeye ni mbunge wa CCM, na mwanachama wa CCM, kuna mapungufu ya hiyo kesi ambayo kwake yanahitaji kupelekwa ndani ya chama chake, kwa kuwahusisha wabunge wa chama chake, na hapa ndipo hasa hisia za Mwalimu kutaka mwenyekiti wa CCM awe ndio rais zinapoonekana, kama Malima hawezi kuchukuliwa hatua kama mbunge, basi mwenyekiti wa CCM anaweza kumchukulia hatua Malima, kama mwanachama wa CCM, na ndio njia iliyotumika kuwaondoa Mbilinyi na Simba, toka kwenye uwaziri ilikuwa ni chama baada ya njia zote za serikali kushindikana, Mwalimu aliwaondoa Jumbe na Seif kupitia hicho hicho chama CCM, sasa kwa nini leo Malima kwenda huko iwe tatizo?
what is wrong with that? Mpaka ku-create all this fuss? I mean mzee Clean, heshima mbele kwa clear and cut on the ishu, Mbunge Malima analindwa na sheria ya kutomuhukumu kutokana na maneno atakayoyamka akiwa ndani ya bunge, unless akisema nje kwenye viwanja vya bunge hapo kisheria hana kinga, hiyo ni kwa sheria ya jamhuri, but Spika anao wajibu kisheria za bunge kumuwajibisha mbunge aliyepatikana kuvunja kanuni za bunge na kamati inayohusika ya bunge,
Sasa nilifikiri the fuss ingekuwa kwa nini Mbunge Malima hakuwajibishwa, na mapungufu ya sheria yetu ya bunge na uimara wake, lakini hasa tungelenga kwenye mapungufu ili kuwasaidia wananchi wa taifa la kesho,
Haya ni mawazo yangu tu!