Wandugu
Kitu ninachopenda hapa JF ni watu wanavyokuwa wanaacha ushabiki na kuzungumzia FACTS. ule ushabiki wa wanaosema ndiyo waseme ndio, ndioooooooooo nknk , i.e. ushabiki wa Simba na Yanga hapa JF si MAHALI pake
The Content of the material tells the fact kwamba Mh Malima alisema UONGO period. other than that ni USHABIKI ambao ni waste of time kama ambavyo sasa huyu kid kilaza anajitahidi kufanya (kwenda kwa Makamba). and afterall ITV sio TVT!!!
kwa mabye hakuona hebu soma hapa chini..................
SPIKA ALISEMA---Kauli ya Mhe. Malima kwamba:-
Nimewahi kushuhudia mimi Rais wa Jamhuri ya Muungano ana habari nzito kwenye taarifa ya habari ya saa mbili anapewa dakika moja na nusu, Waziri Mkuu anataka kuzungumzia njaa anapewa dakika moja na nusu, watoto wa Primary wanakuja kutoka Zanzibar kutembelea Kiwanda cha Coca-Cola wanapewa dakika kumi. Mmiliki wa TV anakwenda kuongea na watoto wa Madrasa Msasani kwa ajili ya kugombana na Sheikh mmoja anapewa dakika kumi.
SPIKA AKAENDELEA, "Inadhihirisha wazi na kushawishi kuwa Mhe. Malima alikuwa anatoa taarifa ya jambo alilolishuhudia yeye mwenyewe.
Katika kauli yake, Mhe. Malima alikuwa anazungumzia kitu cha kitaalam, yaani muda wa kurusha matangazo hewani (Air time), ambapo muda hupimwa kwa sekunde. Kamati ilifanya uchunguzi kwa kuangalia kanda za televisheni za matukio yote yaliyokuwa yametajwa Bungeni na Mheshimwa Malima. Imedhihirika kwamba, kanda za pande zote mbili yaani za Bw Mengi na alizoziwasilisha Mhe Malima. Imebainika kuwa, si kweli kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipewa dakika moja na nusu, watoto wa Primary kutoka Zanzibar waliotembelea Kiwanda cha Coca-Cola walipewa dakika kumi na Mmiliki wa ITV alipokuwa anaongea na watoto wa Madrasa Msasani alipewa dakika kumi.
Katika ushahidi wa kanda iliyowasilishwa na Bw. Mengi, tukio la Bw. Mengi kutembelea Madrasa ya Msasani lilirushwa hewani kwa dakika 4.21, tukio la ziara ya watoto wa Laurent International ya Zanzibar kutembelea ITV Mikocheni lilirushwa hewani kwa dakika 3.17, tukio la Waziri Mkuu akizungumzia njaa lilirushwa hewani kwa dakika 5.04 na tukio la ziara ya Rais Msumbiji lilirushwa hewani kwa dakika 3.31.
7.2.6 Katika ushahidi wa kanda iliyowasilishwa na Mhe. Malima, tukio la ziara ya Rais Msumbiji lilirushwa hewani kwa dakika 3.20, tukio la Waziri Mkuu akizungumzia suala la njaa lilirushwa hewani kwa dakia 4.28, na matukio ya Bw. Mengi kutembelea Madrasa ya Msasani na lile la watoto wa Primary ya Zanzibar kutembelea ITV na Coca-cola yalirushwa hewani kwa dakika 5.50 kwa ujumla wake.
7.2.7 Matokeo hayo ya uchunguzi wa Kamati hiyo ya Bunge yanaonesha wazi kuwa, matamshi ya Mhe. Malima hayakutimiza masharti niliyoyataja kwenye aya ya 5.4.2.1 hapo juu, yaani kwamba, yamevunja na kukiuka masharti na matakwa ya Kanuni ya 50(1) ya Kanuni za Bunge (Toleo la 2004) ambayo, pamoja na mambo mengine, inapiga marufuku Mbunge yeyote kusema Uwongo Bungeni."
Kwa uelewa mzuri, Kanuni hiyo inatamka kwamba:-
Ni marufuku kabisa kusema uwongo Bungeni. Kwa sababu hiyo, Mbunge yeyote anapokuwa akisema Bungeni, atawajibika kuwa na hakika kwamba, maelezo anayoyatoa ni sahihi, na siyo mambo ya kubuni au ya kubahatisha tu;
Ukweli huo unatusaidia kujibu hoja ya pili kwamba, kutokana na kukiuka masharti ya Kanuni ya 50(1) ya Kanuni za Bunge, matamshi ya Mhe. Malima aliyoyatoa Bungeni hayana kinga inayotolewa na Ibara ya 100(1) ya Katiba na Kifungu cha 3 cha Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, 1988.