Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Kwenye kukigawa Chama hapo kina point. Kama hawatakata rufaa na Lema akawa amezuiwa kuna dalili za kukigawa Chama.Hapa hakuna dawa nyingine, zaidi ya kukata rufaa. Lazima tuone HAKI inatendeka. Afadhari jimbo libaliki wazi kwa mwaka moja(wote tukose kuwa na Mbunge) kuliko kukimbilia uchaguzi huki tukikigawa chama. Kura 56,000 alizopata Lema ni nyingi sana. Hatua ya kwanza iwe ni kulinda HAKI ya wapiga kura hao wengi.
Tafadhari sana ndugu zanguni, hapa kitu cha kwanza kabisa ni kukata RUFAA.
Time Limitation ya rufaa: Rufaa ya uchaguzi inatakiwa isikilizwe ndani ya mwaka moja. Mwaka huo mmoja utaisha kabla ya 2015. Lazima tuwe principled ktk kulinda na kutetea HAKI, kuliko kukimbilia uchaguzi.
Note well: Tukumbuke kuwa hii HUKUMU isipotenguliwa na mahakama ya juu, basi itakuwa PRECEDENT ambayo itatumikaa kung'oa wabunge wengi wa upinzani hapo baadaye.