GITWA
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 1,505
- 1,711
Je umetumwa au uko serious na unachosema,maana akiniingii akilini. Jimbo linaweza kuwa wazi mpaka 2015 kutokana na mizengwe ya ccm.Unakua kama huwajui ccm au kweli huwajui? Labda nikukumbushe kuwa ndo wenye dola. Luten yuko sahihi.Hakuna kitu hapa. Huyo jamaa katumwa na CCM. Rufaa ni muhimu kuliko mbio za kutaka kushika jimbo. Je, wakitumia polisi kutangaza mshindi mgombea wa CCM mtasemaje? Ni muhimu chama kikakata rufaa ili haki itendeke.
Sijaisoma hukumu kamili, ispokuwa nimeongea na mawakili wa CDM, Kimomogoro, Marando, Lissu na Profesa Safari, wote wanaona kuwa kuna haja ya kukata rufaa. Nami nakubaliana nao na napingana na wote wanaosema CDM wasikate rufaa.
Uwezkeno wa rufaa kushinda unatokana na Jaji kushindwa kueleza kasoro za ushahidi. Kushindwa kwa Bartida kufika mahakamani; kushindwa kwa Lowassa kufika mahakamani kuliathiri vipi kesi ya msingi na ushahidi.
Hoja hapa siyo Lema kuwa mbunge, hoja hapa kwa nini Lema aenguliwe kwa mambo ya kijinga?
Pili, kwa hukumu ile Lema atalazimika kulipa gharama za kesi karibu Sh. 50 milioni. Sasa awalipe wahuini Sh. 50 milioni ili iweje?
Tatu, hata kama CDM hawataka rufaa, CCM watakata rufaa kwa kuwa hawataki kuendelea na uchaguzi mdogo. Watakatia yale mambo mengine mawili ambayo hayakuamuliwa.
CDM msikubali ushauri wowote wa kutokata rufaa. Kwanza, hiyo kesi itakwisha kabla ya mwaka huu kwa kuwa sheria inasema, "Rufaa ya kesi za uchaguzi zinatakiwa kumalizika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja" tangu hukumu ilipotolewa.