Barua kwa Dr. W. Slaa

Barua kwa Dr. W. Slaa

Nimekukubali Luteni. Hapa tunaaanda tu jinsi ya kufanya kampeni. Yaani hapa nilipo Sakina kila mtu ukimuuliza ni PIPOZIII kwenda mbele. Tunasubiri tuwaaibishe. itakuwa zaidi ya Arumeru na Zaidi ya 2010 maana haitaibwa kula hata moja.

Jembe
 
Viongoz wa chadema nany pitien huu ushaur wa luten. lisemwalo lipo jaman, nam nimeckia ccm watafanya kila wawezavyo wang'ang'anie jimbo.
 
HAPA KINACHOTAKIWA NI KUKATA RUFAA! kwa utaratibu ufuatao:

1.Notice of appeal
2.Stay of decree of execution pending appeal(application hii iki succeed Lema ataendelea kuwa Mbunge na kupata haki zote za kibunge, mpaka appeal yake itakaposikilizwa na kuamriwa vinginevyo).
3.Filing of memorandum of appeal

OMBI: Shauri hili linatakiwa kuangaliwa kisheria zaidi kuliko kihisia. Lazima rufaa ikatwe kwani ni haki ya kikatiba.Mimi binafsi nauhakika rufaa ikikatwa Lema atashinda, kwasababu ile hukumu ina mashimo mengi sana.Ameandikwa kisiasa zaidi kuliko kisheria.
Nawaombeni sana rufaa ikatwe, ili tuone utawala wa sheria unaoongelewa siku zote una sura gani katika nchi yetu. Je ni porojo au kweli kuna utawala wa sheria?
Kisheria rufaa ikikatwa na kama itasikilizwa kwa haki kwa mujibu wa sheria za nchi hii, lema atashinda tuu!!!!
Tafadhari sana: Tusiukimbile uchaguzi ambapo kuna uwezekano wa kumweka mbunge wao kwa kutumia mtutu wa bunduki!
hapa lazima kufikiri sana!
 
Limitation ya rufaa za kesi za uchaguzi ni kuwa inatakiwa iishe ndani ya mwaka mmoja.
 
Asante luteni kwa ushauri mzuri, ZANZIBAR ITAKOMBOLEWA NA WAZANZIBAR WENYEWE!
 
Ndugu Slaa,

Kwanza niruhusu nitoe pongezi zangu za dhati kabisa kwako binafsi na kwa chama chako cha CHADEMA kwa mafanikio mliyoyapata kwa kipindi kifupi. Natambua kazi mnayoifanya ni nzito na ya hatari maana wengi wanatamani kuwa kama ninyi lakini wanaogopa kutangulia ila nyie mmesema mnatangulia wengine watawakuta mbele ya safari. Kwa hilo hongera sana.

Bila kupoteza muda kutaja mafanikio mliyoyapata naomba nijikite moja kwa moja kwenye kiini cha barua hii.

Kabla sijasahau naomba chama kisikate rufaa kwa kesi ya Lema.

Naomba nikukumbushe tu kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 CCM hawakutaka si tu nyie mshinde bali msiongeze wabunge wa kuchaguliwa. Utakumbuka matamshi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM ndugu Makamba alipowaambia wanachama wa CCM kwenda kutafuta sababu yeyote ile wafungue kesi kupinga ushindi wa wabunge wa Chadema na chama kitagharamia kesi? Yanayotokea sasa ni utekelezaji tumjiandae kwa makubwa.

Utekelezaji wa hukumu ya Lema ni mwanzo tu ya mipango mingi ya CCM kuihujumu Chadema. Mpango ulikuwa trh 1-4 washinde Arumeru Mashariki halafu trh 5-4 ushindi wa Lema utenguliwe na sherehe kubwa yakupongezana ilikuwa ifanyike weekend hii mjini Arusha. Najua hilo limeshindikana.

Hukumu ya kupinga ushindi wa Lema si kwamba Jaji kajichanganya ni mtego wa makusudi ili nyie mjichanganye waendelee na plan B,C. Lengo lao ni kuikamata Arusha kwa hali yeyote kwa vile wanajua fika hawawezi kuikamata kwa kutumia sanduku la kura, kwa hiyo njia iliyobaki ni kutumia mahakama na pingamizi. Narudia tena msikate rufaa.

Lema amehukumiwa kwa kifungu 108 ‘Illegal Campaign’ kinachomruhusu kugombea lakini kwenye majumuisho ya hukumu imeandikwa kahukumiwa kwa kifungu 114 “Illegal Practice” kinachomuzuia kugombea kwa miaka 5. Wanataka mkate rufaa au muombe ku review case na hapo itacheleweshwa mwisho mtaambiwa muda ni mfupi wa kuitisha uchaguzi.

CCM imeanza kuhaha baada ya kuona hamna mpango wa kukata rufaa, wanachosubiri ni Lema ateuliwe kugombea wamuwekee pingamizi, believe me or not lazima ataondolewa hata kama mtakuwa na hukumu mkononi.

Ndugu Slaa, CCM wameshafanya kosa wanajishauri endapo waingie kwenye uchaguzi ama la. Ushauri wangu ni kuwa, whatever the case, nendeni kwenye uchaguzi hata kama Lema hatogombea najua mtapata mgombea mwingine makini. Kama chama kitaona Lema asigombee, apewe kazi makao makuu ya kukiimarisha chama, akusaidie kuzunguka nchi nzima hasa katika kuimarisha matawi tayari kwa uchaguzi wa ndani na wa serikali za mitaa.

Nawatakia mafanikio mema katika ukombozi, najua kadritaabu zinavyozidi ndivyo ukombozi unavyokaribia.

Luteni.

huku nakuna kitambi nasema....point!!
 
Huyu Luteni katumwa na CCM. ushauri wake niwakuiangamiza CDM na kuinufaisha CCM.
 
Kukata rufaa ni wazo la msingi, kwa maana hao [NENO BAYA] nao wana hoja zao. Tunatakiwa kupambana ili haki ipatikane. LEMA ni lazima ashiriki uchaguzi kwa maana ana haki ya msingi.
Peeeoooooopleeeeeeeeeeeeeeee........................Pooooooooooweeeeeeeeeeeer................
 
Nimeipenda hii kauli hapa kwenye haya maandishi mekundu hata CCM ingemsimamisha JK mwenyewe na Chadema wakasimamisha jiwe, jiwe litashinda!.
 
Hili swala ni nyeti sana kutokukata rufaa kutmuathili Lema na pia kutawapa mwanya ccm kuthibitisha kuwa hoja zilizotumika kufuta ubunge wa Lema ni za kweli, lakini pia hapa issue siyo jimbo wala Lema kuwa mbunge issue ni HAKI itendeke, lakini pia wananchi wana haki ya kuwa na mbunge ambaye ni chaguo lao kwanini walazimishiwe kubadili mbunge kwa nguvu na mashinikizo ya kisiasa.
 
mawazo ni mazuri sana ju ya hii issue,swala la msingi ni kusubir na kuona viongoz wetu wa chama wameamuaje juu ya hili swala maana kiukweli limeteka hisia za watu na watu wapo makkini sana kuona viongoz wa chama wameamua nini. mungu ibariki chadema,mungu ibariki tanganyika
 
Huyu Luteni katumwa na CCM. ushauri wake niwakuiangamiza CDM na kuinufaisha CCM.
Mkuu moma2k, unasema mimi nimetumwa umesahau na wewe umeishauri CDM kwenye post hii hapa chini kama mimi nilivyoishauri. Kwani wewe umetumwa na nani?

HAPA KINACHOTAKIWA NI KUKATA RUFAA! kwa utaratibu ufuatao:

1.Notice of appeal
2.Stay of decree of execution pending appeal(application hii iki succeed Lema ataendelea kuwa Mbunge na kupata haki zote za kibunge, mpaka appeal yake itakaposikilizwa na kuamriwa vinginevyo).
3.Filing of memorandum of appeal

OMBI: Shauri hili linatakiwa kuangaliwa kisheria zaidi kuliko kihisia. Lazima rufaa ikatwe kwani ni haki ya kikatiba.Mimi binafsi nauhakika rufaa ikikatwa Lema atashinda, kwasababu ile hukumu ina mashimo mengi sana.Ameandikwa kisiasa zaidi kuliko kisheria.
Nawaombeni sana rufaa ikatwe, ili tuone utawala wa sheria unaoongelewa siku zote una sura gani katika nchi yetu. Je ni porojo au kweli kuna utawala wa sheria?
Kisheria rufaa ikikatwa na kama itasikilizwa kwa haki kwa mujibu wa sheria za nchi hii, lema atashinda tuu!!!!
Tafadhari sana: Tusiukimbile uchaguzi ambapo kuna uwezekano wa kumweka mbunge wao kwa kutumia mtutu wa bunduki!
hapa lazima kufikiri sana!
 
Ili serikali ijifunze CDM inatakiwa ishinde uchaguzi wa marudio kwa kishindo, itatoa funzo kuwa mbunge ni chaguo la wananchi si la mahakama.
Hilo liko wazi, kwa arusha nakuhakikishia wala usiwe na wasi wasi... Labda huo uchaguzi uhairishwe!
 
Nimeipenda hii kauli hapa kwenye haya maandishi mekundu hata CCM ingemsimamisha JK mwenyewe na Chadema wakasimamisha jiwe, jiwe litashinda!.
Ndio kauli inayoongelewa na watu wa arusha kwa sasa. Na ni kweli wanamaanisha manake kiukweli CCM kwa arusha ni kama inajisumbua bure, haitakiwi hata kwa dawa! Tunasubiri kwa hamu huo uchaguzi, tutawatia aibu kuliko waliyoipata 2010.
 
HAPA KINACHOTAKIWA NI KUKATA RUFAA! kwa utaratibu ufuatao:

1.Notice of appeal
2.Stay of decree of execution pending appeal(application hii iki succeed Lema ataendelea kuwa Mbunge na kupata haki zote za kibunge, mpaka appeal yake itakaposikilizwa na kuamriwa vinginevyo).
3.Filing of memorandum of appeal

OMBI: Shauri hili linatakiwa kuangaliwa kisheria zaidi kuliko kihisia. Lazima rufaa ikatwe kwani ni haki ya kikatiba.Mimi binafsi nauhakika rufaa ikikatwa Lema atashinda, kwasababu ile hukumu ina mashimo mengi sana.Ameandikwa kisiasa zaidi kuliko kisheria.
Nawaombeni sana rufaa ikatwe, ili tuone utawala wa sheria unaoongelewa siku zote una sura gani katika nchi yetu. Je ni porojo au kweli kuna utawala wa sheria?
Kisheria rufaa ikikatwa na kama itasikilizwa kwa haki kwa mujibu wa sheria za nchi hii, lema atashinda tuu!!!!
Tafadhari sana: Tusiukimbile uchaguzi ambapo kuna uwezekano wa kumweka mbunge wao kwa kutumia mtutu wa bunduki!
hapa lazima kufikiri sana!

1.Hakuna muda wa kuanza kuona kama kuna utawala wa shria ,It is obvious haupo.Mahakama ni hiyo hiyo ya CCM
2.Twende kwenye Uchaguzi,Kuiba hawataweza,Wakijaribu ndo kutachimbika vizuri.Ukombozi wa damu utaanzia huko
 
Rufaa kukatwa ni lazima coz bila kufanya hivyo, inaweza kujatumika kama reference kwenye kesi nyingine. Iwe isiwe "Right delayed is the right denied"
Aluta continue, haiwezekani cdm kiwe na wanasheria zaidi ya 5 kwenye kamati kuu zen ikashindwa swala la kisheria na kuamua kunyamaza tu eti tutashinda uchaguzi, hiyo itakuwa ni kutumia vibaya fedha wa wananchi (kwenye uchaguzi)
 
1.Hakuna muda wa kuanza kuona kama kuna utawala wa shria ,It is obvious haupo.Mahakama ni hiyo hiyo ya CCM
2.Twende kwenye Uchaguzi,Kuiba hawataweza,Wakijaribu ndo kutachimbika vizuri.Ukombozi wa damu utaanzia huko
G natamani uchaguzi ungekuwa hata kesho.... Wataelewa maana ya nguvu ya uma ni nini.

Kuhusu swala la kuiba kura sahau manake za Batilda waliiba bado hazikutosha, safari hii hawataiba kura hata moja!
 
Naunga mkono hoja! Lakini kwa nini Lema ameandamwa sana tangu awe mbunge? Nakumbuka tangu awe mbunge amesakamwa sana why?

Alihojiwa siku moja baada ya hukumu na kudai kuwa jamaa wa CCM walikwishamfuata ili agombee kupitia chama chaao akakataa. Amekataa pia kumtambua meya wa ARUSHA
 
Hili swala liko complicated kwa kiasi fulani. Kuna mitego mingi ya kutegua, lakini ili haki itendeke nadhani rufaa ni muhimu na hasa iwapo rufaa hiyo itasikilizwa mwaka huu na hukumu kutoka mapema.

Rufaa isipokatwa, tunaweza kufungua milango ya kesi nyingine za kijinga zinazoendelea huko Singida, Meatu, Ubungo na kwingine ambako wabunge wa CHADEMA wamefungulia mashitaka ya ajabu ajabu ambayo hayana kichwa wala miguu. Kama CHADEMA hawatakata rufaa kwenye hii kesi, basi tunaweza kuanza kushuhudia hukumu za ajabu ajabu kwenye kesi hizi zinazoendelea sasa hivi.

Kutokata rufaa kunamnyima haki Bwana Lema ya kugombea kwa kipindi cha miaka 5, na sijui hiyo hesabu ya miaka 5 inaanza baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 au baada ya hukumu kutolewa? Kama Lema hatakata rufaa then hata 2015 anaweza kuwekewa pingamizi iwapo ataamua kugombea popote.
 
Back
Top Bottom