Barua kwa Dr. W. Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua kwa Dr. W. Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Apr 6, 2012.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ndugu Slaa,

  Kwanza niruhusu nitoe pongezi zangu za dhati kabisa kwako binafsi na kwa chama chako cha CHADEMA kwa mafanikio mliyoyapata kwa kipindi kifupi. Natambua kazi mnayoifanya ni nzito na ya hatari maana wengi wanatamani kuwa kama ninyi lakini wanaogopa kutangulia ila nyie mmesema mnatangulia wengine watawakuta mbele ya safari. Kwa hilo hongera sana.

  Bila kupoteza muda kutaja mafanikio mliyoyapata naomba nijikite moja kwa moja kwenye kiini cha barua hii.

  Kabla sijasahau naomba chama kisikate rufaa kwa kesi ya Lema.

  Naomba nikukumbushe tu kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 CCM hawakutaka si tu nyie mshinde bali msiongeze wabunge wa kuchaguliwa. Utakumbuka matamshi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM ndugu Makamba alipowaambia wanachama wa CCM kwenda kutafuta sababu yeyote ile wafungue kesi kupinga ushindi wa wabunge wa Chadema na chama kitagharamia kesi? Yanayotokea sasa ni utekelezaji tumjiandae kwa makubwa.

  Utekelezaji wa hukumu ya Lema ni mwanzo tu ya mipango mingi ya CCM kuihujumu Chadema. Mpango ulikuwa trh 1-4 washinde Arumeru Mashariki halafu trh 5-4 ushindi wa Lema utenguliwe na sherehe kubwa yakupongezana ilikuwa ifanyike weekend hii mjini Arusha. Najua hilo limeshindikana.

  Hukumu ya kupinga ushindi wa Lema si kwamba Jaji kajichanganya ni mtego wa makusudi ili nyie mjichanganye waendelee na plan B,C. Lengo lao ni kuikamata Arusha kwa hali yeyote kwa vile wanajua fika hawawezi kuikamata kwa kutumia sanduku la kura, kwa hiyo njia iliyobaki ni kutumia mahakama na pingamizi. Narudia tena msikate rufaa.

  Lema amehukumiwa kwa kifungu 108 ‘Illegal Campaign’ kinachomruhusu kugombea lakini kwenye majumuisho ya hukumu imeandikwa kahukumiwa kwa kifungu 114 “Illegal Practice” kinachomuzuia kugombea kwa miaka 5. Wanataka mkate rufaa au muombe ku review case na hapo itacheleweshwa mwisho mtaambiwa muda ni mfupi wa kuitisha uchaguzi.

  CCM imeanza kuhaha baada ya kuona hamna mpango wa kukata rufaa, wanachosubiri ni Lema ateuliwe kugombea wamuwekee pingamizi, believe me or not lazima ataondolewa hata kama mtakuwa na hukumu mkononi.

  Ndugu Slaa, CCM wameshafanya kosa wanajishauri endapo waingie kwenye uchaguzi ama la. Ushauri wangu ni kuwa, whatever the case, nendeni kwenye uchaguzi hata kama Lema hatogombea najua mtapata mgombea mwingine makini. Kama chama kitaona Lema asigombee, apewe kazi makao makuu ya kukiimarisha chama, akusaidie kuzunguka nchi nzima hasa katika kuimarisha matawi tayari kwa uchaguzi wa ndani na wa serikali za mitaa.

  Nawatakia mafanikio mema katika ukombozi, najua kadritaabu zinavyozidi ndivyo ukombozi unavyokaribia.

  Luteni.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru luteni kwa barua yako yenye maneno murua...
   
 3. d

  deecharity JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 831
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  upo sahihi...
   
 4. k

  kanganyoro Senior Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 22, 2011
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  In such ni ushauri mzuri, lakini busara yapaswa kutumika, hili jambo la Arusha si dogo kama jinsi watu wanavyoweza kufikiria, inaweza ikaipeleka nchi pabaya.
   
 5. H

  HisiaZAkweli Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Luteni wewe ni Jembe.
   
 6. D

  Dadayangu Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushauri mzuri...
   
 7. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kadiri taabu zinavozodi ndivo ukombozi unavokaribia. hilo nalo neno.
   
 8. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ushauri mzuri.
  Cdm isikate rufaa, Lema apewe kazi ya kukijenga chama na kutoa elimu.
   
 9. PERECY

  PERECY Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="width: 500"]
  [TR]
  [TD]
  Barua kwa Dr. W. Slaa
  Ndugu Slaa,

  Kwanza niruhusu nitoe pongezi zangu za dhati kabisa kwako binafsi na kwa chama chako cha CHADEMA kwa mafanikio mliyoyapata kwa kipindi kifupi. Natambua kazi mnayoifanya ni nzito na ya hatari maana wengi wanatamani kuwa kama ninyi lakini wanaogopa kutangulia ila nyie mmesema mnatangulia wengine watawakuta mbele ya safari. Kwa hilo hongera sana.

  Bila kupoteza muda kutaja mafanikio mliyoyapata naomba nijikite moja kwa moja kwenye kiini cha barua hii.

  Kabla sijasahau naomba chama kisikate rufaa kwa kesi ya Lema.

  Naomba nikukumbushe tu kwamba kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 CCM hawakutaka si tu nyie mshinde bali msiongeze wabunge wa kuchaguliwa. Utakumbuka matamshi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa CCM ndugu Makamba alipowaambia wanachama wa CCM kwenda kutafuta sababu yeyote ile wafungue kesi kupinga ushindi wa wabunge wa Chadema na chama kitagharamia kesi? Yanayotokea sasa ni utekelezaji tumjiandae kwa makubwa.

  Utekelezaji wa hukumu ya Lema ni mwanzo tu ya mipango mingi ya CCM kuihujumu Chadema. Mpango ulikuwa trh 1-4 washinde Arumeru Mashariki halafu trh 5-4 ushindi wa Lema utenguliwe na sherehe kubwa yakupongezana ilikuwa ifanyike weekend hii mjini Arusha. Najua hilo limeshindikana.

  Hukumu ya kupinga ushindi wa Lema si kwamba Jaji kajichanganya ni mtego wa makusudi ili nyie mjichanganye waendelee na plan B,C. Lengo lao ni kuikamata Arusha kwa hali yeyote kwa vile wanajua fika hawawezi kuikamata kwa kutumia sanduku la kura, kwa hiyo njia iliyobaki ni kutumia mahakama na pingamizi. Narudia tena msikate rufaa.

  Lema amehukumiwa kwa kifungu 108 ‘Illegal Campaign' kinachomruhusu kugombea lakini kwenye majumuisho ya hukumu imeandikwa kahukumiwa kwa kifungu 114 "Illegal Practice" kinachomuzuia kugombea kwa miaka 5. Wanataka mkate rufaa au muombe ku review case na hapo itacheleweshwa mwisho mtaambiwa muda ni mfupi wa kuitisha uchaguzi.

  CCM imeanza kuhaha baada ya kuona hamna mpango wa kukata rufaa, wanachosubiri ni Lema ateuliwe kugombea wamuwekee pingamizi, believe me or not lazima ataondolewa hata kama mtakuwa na hukumu mkononi.

  Ndugu Slaa, CCM wameshafanya kosa wanajishauri endapo waingie kwenye uchaguzi ama la. Ushauri wangu ni kuwa, whatever the case, nendeni kwenye uchaguzi hata kama Lema hatogombea najua mtapata mgombea mwingine makini. Kama chama kitaona Lema asigombee, apewe kazi makao makuu ya kukiimarisha chama, akusaidie kuzunguka nchi nzima hasa katika kuimarisha matawi tayari kwa uchaguzi wa ndani na wa serikali za mitaa.

  Nawatakia mafanikio mema katika ukombozi, najua kadritaabu zinavyozidi ndivyo ukombozi unavyokaribia.

  Luteni.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 10. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Luten Mungu akubariki na bila shaka Dr Slaa atapita hapa.
  Lakini suala hili kunatakiwa kufanyike kitu ili serkali ijifunze, tunasubiri busara za viongozi wa cdm
   
 11. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  luteni wewe pekee umeweza kuchambua hukumu vizuri hapa JF. sas tunapata mwanga jinsi hukumu ilivyo. CDM tunasema jimbo bd ni letu tutapata mgombea makini. kamanda LEMA shujaa wetu azunguke nchi nzima kupiga kampeni ya kukitangaza chama. kupata wanachama wapya. asiwe na hofu mungu yupo nasi na si hawa wezi CCM.
   
 12. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Magamba bwana!
   
 13. L

  LAT JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  huu ushauri wa barua hii ni wa kuzingatia .... technicalities zote za hukumu hii zizingatiwe
   
 14. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja! Lakini kwa nini Lema ameandamwa sana tangu awe mbunge? Nakumbuka tangu awe mbunge amesakamwa sana why?
   
 15. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Luteni shukrani zangu zikufikie, uliyoyasema nikama vile umechungulia then ukadesa fikra zangu.. Ufafanuzi wa kisheria umenitia hamasa, thanx sana!
   
 16. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  haiwezekani kurudi mahakamani kupata uhakika wa kosa la lema?maana imejichanganya judgement report
   
 17. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  tuwaache wabaki na hukumu yao sisi turudi kwenye sanduku la kura na mgombea mpyaaaaaaaaaaaaaaaaa halfu tuwaonyeshe kazi.
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hakuna kitu hapa. Huyo jamaa katumwa na CCM. Rufaa ni muhimu kuliko mbio za kutaka kushika jimbo. Je, wakitumia polisi kutangaza mshindi mgombea wa CCM mtasemaje? Ni muhimu chama kikakata rufaa ili haki itendeke.

  Sijaisoma hukumu kamili, ispokuwa nimeongea na mawakili wa CDM, Kimomogoro, Marando, Lissu na Profesa Safari, wote wanaona kuwa kuna haja ya kukata rufaa. Nami nakubaliana nao na napingana na wote wanaosema CDM wasikate rufaa.

  Uwezkeno wa rufaa kushinda unatokana na Jaji kushindwa kueleza kasoro za ushahidi. Kushindwa kwa Bartida kufika mahakamani; kushindwa kwa Lowassa kufika mahakamani kuliathiri vipi kesi ya msingi na ushahidi.
  Hoja hapa siyo Lema kuwa mbunge, hoja hapa kwa nini Lema aenguliwe kwa mambo ya kijinga?

  Pili, kwa hukumu ile Lema atalazimika kulipa gharama za kesi karibu Sh. 50 milioni. Sasa awalipe wahuini Sh. 50 milioni ili iweje?

  Tatu, hata kama CDM hawataka rufaa, CCM watakata rufaa kwa kuwa hawataki kuendelea na uchaguzi mdogo. Watakatia yale mambo mengine mawili ambayo hayakuamuliwa.

  CDM msikubali ushauri wowote wa kutokata rufaa. Kwanza, hiyo kesi itakwisha kabla ya mwaka huu kwa kuwa sheria inasema, "Rufaa ya kesi za uchaguzi zinatakiwa kumalizika ndani ya kipindi cha mwaka mmoja" tangu hukumu ilipotolewa.
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,542
  Likes Received: 18,172
  Trophy Points: 280
  Mkuu Luteni naunga mkono ushauri wako wa CDM kisikate rufaa na kita liretain jimbo la Arusha kwa kishindo kikubwa kuliko 2010.

  Lakini kwa vile Chadema ni chama cha kutetea haki, na ile hukumu sio hukumu ya haki kisheria, nashauri Chadema wafanye yafuatayo.

  1. Kwanza Chadema iombe expert legal opinion toka kwa wanasheria nguli na mahiri.
  2.Kuangalia uwezekano wa kuomba "Stay Off Excecution Order" toka mahakama ya juu wakionyesha intention ya kukata rufaa hivyo mahakama ya juu itatoa "stay order" kwa Lema kuendelea kuwa mbunge mpaka baada ya rufaa yake kusikilizwa!.
  3. Kinachotakiwa ni kutumia nguvu za hoja kupata hiyo "Stay Order" na sio hoja za nguvu!.
  4. Wakijiridhisha kuwa hili la stay order haliwezekani ndipo waamue wasikate rufaa na wasimsimamishe Lema!. Nimemsikia mkazi wa Arusha akisema hata CCM ingemsimamisha JK mwenyewe na Chadema wakasimamisha jiwe, jiwe litashinda!.

  Pasco
   
 20. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Safi sana luteni tunaitaji ushauri wenye busara kama wako ktk kipindi kigumu kama hiki cha mabadiliko.
   
Loading...