Nikiwa kama mtanzania mpenda mabadiliko sina budi nami kutia neno katika uhamuzi wa Dr.Wilbrod Slaa kususa siasa za CHADEMA tena katika kipindi ambacho mwali ameishaingia chumbani na tena kavua nguo zote
Nakili kuwa ni haki yako kabisa kuchukua uhamuzi aliouchukua lakini pia nikili kuwa ulipaswa kutafakari kwa kina na kama kiongozi uliyetazamiwa kupewa nchi haukupaswa kujifungia muda mrefu kutafakari bali siku moja au mbili zingekutosha kuueleza umma maamuzi yako badala ya kuzira kimyakimya!
Taswira uliyoijenga kama kiongozi shupavu na jasiri na hata kutuaminisha kuwa ulifaa kupewa nchi sasa inatufanya tuwaze vinginevyo. Kumbe siku moja ukiwa rais ungeweza kususia kushirikiana na viongozi wenzako wa mataifa ya Afrika, America, Ulaya na hata Asia kisa rais Kagema amepinga au amekusema vibaya..au Nkurunzinza kalazimisha kugombea mhura wa tatu kinyume na makubaliano ya Arusha! Ungekuwa rais wa ajabu kwelikweli.
Siku za nyuma kidogo, niliandika nikipongeza hotuba ya Mwenyekiti Mbowe nikidiliki kusema kuwa itachukua miaka mingi kusikia tena hotuba kama hiyo. Katika hotuba yake mbowe aligusia umuhimu wa kutokaa na madonge moyoni ambayo hayawezi kutusogeza mbele kimaendeleo bali kusahau ya nyuma na kusonga mbele akisisitiza kuwa katika siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu.
Aliongeza kuwa jamii yote ingemshangaa kama mwenyekiti wa chama kumkataa Lowasa, mtu mwenye mtaji mkubwa wa wapiga kura kisa hisia tu zilizojengwa juu yake kuwa utajiri wake ni wakifisadi. Siku zote adui wa adui yako ni rafiki
CCM tayari wameweka uadui na Lowasa kwa kumkata jina bila sababu za msingi kama alivyothibitisha Prof. Mwandosa, Kingunge, Nchimbi na wengineo.
Wakati huu ambao CHADEMA imeunganisha nguvu na vyama vya CUF, NLD na NCCR Mageuzi ni wakati ambao haujawahi kutokea katika historia ya vyama vyingi vya siasa hapa nchini. Kwa tabia hii ya Slaa inaonesha si tu kumkataa Lowasa bali pia hata kama Prof. Lipumba angepitishwa kupeperusha bendera ya UKAWA angesusa au anatuma salamu kwa wagombea wa chadema wa majimbo na udiwani kuwa kwa kuwa wameshiriki kukijenga chama basi kama wakikatwa na nafasi zao kupewa wagombea wengine wa UKAWA basi nao wasuse!
Katika hotuba yake ya kumkaribisha Lowasa, Mbowe alisema kuwa hatuwezi kujenga chama cha viongozi, aliyejiunga leo, jana ana haki sawa na mwasisi wa chama hicho
tusiwakatae wageni kisa nafasi zetu, CHADEMA siyo chama cha kugawana vyeo bali majukumu na hiyo ndiyo demokrasia. Tusijiwekee hati miliki kwenye vyama ambavyo tunadai ni vya wananchi, amabao waamefanya vyama mali yao binafsi kama akina mzee Cheyo, Mrema, Mtikila na wengineo tunaona uimara wa vyama hivyo.
Dr. Slaa kubali kuwa siasa ndivyo zilivyo
tuwe na mtizamo mpana wan chi badala ya maslahi binafsi, nafasi yoyote inayolenga kuongeza nguvu katika mapambano itumie. Siyo kwamba CUF na wenzao ni wajinga bali wameweka mbele maslahi taifa kwanza badala ya ruzuku, viti maalum, uimara wa vyama vyao badala ya uchaguzi ili kwanza lengo la kuiondoa CCM madarakani litimie na mengine yatajadilika daadae.
Kama Dr. Slaa anaamini ndugu Edward ni mwizi/fisadi basi apeleke ushahidi huo mahakamani na kama hana ushahidi basi arudi washirikiane kuondoa mfumo unaowawezesha watu kufanya ufisadi. Lazima tukubali, kama mfumo unatoa magepu ya kupiga hata mimi nikiingia lazima nipige coz opportunity ipo!
Kinachonishangaza kwa Dr. Slaa; kapiga chenga uwanja mzima..kabaki na kipa
kipa amekaba upande wake na kuacha goli wazi na kwa bahati nzuri anatokea mchezaji mwenzake anaomba pasi amalizie anashindwa kumpasia kisa mchezaji huyo hampendi.
Mwisho nakuomba Dr. piga moyo konde..rudi jeshini tumalizie mapambano, kumkomboa mtanzania siyo mpaka wewe uwe rais. Fanya kama walivyofanya wanamapinduzi wengine akina Che Guevara n.k
Abiiiingeeee...