Barrick gold msitufanye mabwege! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barrick gold msitufanye mabwege!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Katikomile, May 13, 2010.

 1. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #1
  May 13, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Nimekuwa nikiona matangazo ya kazi ya Barrick Gold kwa muda mrefu katika magazeti yetu, lakini nimekuwa nashindwa kuelewa hawa jamaa wanatufanya mabwege! Wenyewe wanataka waonyeshe umma wa Watanzania kwamba ni wazelendo na ndio maana wanatangaza kazi zao (cheap posts) magazetini. Mbona post kubwa kubwa kuanzia manager na kuendelea hazitangazwi?? wanaleta watu wao toka nje au kupeana kwa mtoto wa fulani (technical know WHO!).

  Sasa kama leo kwenye gazeti la mwananchi eti inatangazwa kazi ya "Fuel Bay Attendant" jamani! jamani! hii si wangechukua tu vijana wa pale Bulyanhulu ama Kahama ili wawawezeshe kuliko kutangaza national-wide na ku-uwadaa umma eti wao ni Equal Opportunity Employer!

  Kuna kipindi kama wana posts kama tano, mara mpishi, mara mlinzi, receiptionist, fuel attendant, truck driver n.k utakuta wanatoa post moja moja kila siku ili mradi watokee wiki nzima.

  Ok jamaa wana pesa nyingi kutokana na kwamba wako kwenye stock exchange na dhahabu bwelele wanayopata hapa kwetu!

  Mageti ya mgodini kila siku yanajaa vijana na wakazi wa maeneo husika wakija kuomba kazi, nyie mnawanyima eti mnasubiri kutangaza posts national-wide! Ndio maana wananchi wanakuwa na hasira na nyie na kuwaibia, Wapeni hizo cheap posts amabazo you can train them as there are some posts which dont need someone to see the inside of the class!

  Nawasilisha!
   
 2. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  This is bongolala my dear. Wameshasoma mchezo wakaona wabongo, bongo zimelala. Tusiwalaumu wao, tatizo ni leo (hasa viongozi) kukubali upuuzi huu.
   
 3. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Alafu application unatuma kwa email! Hao fuel attendant to be, wana email address kweli?
   
 4. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Huu ni upuuzi mkubwa. Wanauzi sana kwa kwel
   
 5. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi nazani tukiwa sema sana huku JF. afu tukatoa pia magazetini watashtuka na kuogopa vitendo vyao hivyo maana wamesha tuona watanzania kama maboya vile
   
 6. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wizara ya kazi, ajira na maendeleo ya vijana haina haja ya kuwepo, waziri bongo lala, katibu usingizi, mkurugenzi na maafisa wengine sijui hawaoni haya matusi ya barrick!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sheria ya kazi umeisoma lakini????????
   
 8. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
 9. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #9
  May 14, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45

  Mkuu ulikuwa unaongelea nini hasa ama ulimaanisha nini, make nimekuwekea link ili uone hiyo sheria na kwamba nimeisoma!
   
 10. n

  nakose Member

  #10
  May 14, 2010
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdau

  Mi naona kama ungefuatilia vizuri.

  Ukitaka kazi za Barrick Gold soma zaidi Guardian na Daily news ndiko wanakotoa matangazo mengi ya kazi.

  Lat week wametangaza nafasi kama 6 hivi Moja ikiwepo Process plant training Superitendent.(Mdau hiki ni cheo cha juu sana mgodini,kama unamjua mtu yoyote ambae amesoma Mining Metallurgy muambie aaply mshahara wa kufa mtu.

  Halafu kuna nafasi 4 za Snr.Human resources Officers nazo zimetangazwa kwenye guardian kama una vigezo aplly tu mtu wangu.

  Na kuna nafasi nyingine ya mbili za Human resourses superitendent,plz aplly kama una vigezo au waambie washkaji waapply.

  Nyingine ni Communication Co-odnator zote hizi zimetangazwa a week ago,ina maana ulikua huzioni unaona tu hizo za clerks ndugu yangu.

  Mi nakushauri kama unatafuta kazi tuma maombi au kama kuna mtu anatafuta kazi muambie atume maombi.

  Nakutakia mafanikio mema na mungu akujalie uwe shortliseted kwenye hizo nafasi.
   
 11. Katikomile

  Katikomile JF-Expert Member

  #11
  May 14, 2010
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 473
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45

  Nashukuru kwa maneno yako kaka!

  Ila nikufahamishe tu as my name goes, mimi ni Mjasiriamali sihitaji kuwa MTUCTA! So nilitoa hoja baada ya kuguswa na matangazo ya Barrick.

  Kama ni matangazo ni kweli Guardian yanatoka mengi sana, lakini the subject matter of my thread kama ulinielewa ni jinsi jamaa wanavyotangaza hizo posts, post ya fuel Bay attendant inacover almost quarter of the page, maelezo lukuki utafikiri anatafutwa CEO wa TANESCO. Sasa kwa watu wa Public Relation hii kitu wanaelewa kwamba it is all about kuonesha jamii kwamba tunawapenda watanzania na ndio maana tunawapa kazi za kumwaga!

  Just imagine, posts ambazo zinaweza zikatoka kwenye page moja wanatoa moja moja kila siku, japo ndio kweli nakubaliana na wewe kuna wakati wanatoa hata hizo sita at ago, ila kuna posts nyingine zi za kutangaza gazetini hata kama wana hela! Ni kutuhadaa watanzania tu!


  Kuhusu suala la mishahara kuwa mikubwa, mambo ilishabadilika huko migodini baada ya serikali kuingilia kati na wao kusoma salary scale za TZ zikoje! Huyo anayekwambia anapata mshahara mnono kama unavyousifia mwambie akuoneshe salary slip yake uone! Wengi wanapenda kutaja mishahara mikubwa kumbe sio wanachopata!
   
Loading...