The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,442
113,452
Wanabodi,
nimeishawahi kusema sana humu, na sasa narudia tena, kuwa "Kauli Huumba". Kauli ya uongo ukisemwa sana, na kuachwa na kurudiwa rudiwa, bila kukanushwa, sio kuwa uongo huo unaweza kuonekana kama ni ukweli, bali uongo huo unaweza kabisa kugeuka kuwa kweli, kwa sababu kauli nyingine zina powers na uwezo wa kuumba,
Mfano kila mtoto anazaliwa akiwa malaika, kumuita "mtoto mbaya" mara kwa mara, hizo kauli zinamuumbia ubaya, mwisho wa siku anakuja kuwa mtoto mbaya kweli.

Hivyo ukitunga uongo, ukausema huo uongo, na kuurudia rudia, usipokanushwa kuwa huo ni uongo, then mwisho wa siku, uongo huo unakuja kugeuka ni ukweli!.

Hili Jarida la The Economist, siku zote limekuwa na kawaida ya kutunga uongo juu ya Tanzania, kumtungia uongo na kumtukana rais wetu kwa majina ya ajabu ajabu na kumsingizia maneno ya uongo, mfano hai ni katika toleo lake la leo, Jarida hili limeibuka na kichwa cha habari hiki kuhusu Tanzania na kumchora rais Magufuli kwa katuni ya tingatinga!.
A dose of bullTanzania’s leader, the “Bulldozer”, runs off course
President John Magufuli hates critics, gay people and accurate statistics
1552723486512.png


Kwa wasomaji wa kizungu mnaweza kwenda kujisomea wenyewe
Tanzania’s leader, the “Bulldozer”, runs off course

Mauongo yao ni kama ifuatavyo
Wanamuta rais wetu kuwa ni Bulldozer, wadai anawachukia wakosoaji, hivi ni kweli rais Magufuli ana chuki na wakosoaji?, hivi kuna mtu alikuwa mkosoaji mkubwa wa serikali kama Dr. Slaa?. Huku kwenye mitandao ya kijamii, kuna mtu alikuwa mkosoaji mkubwa kama Prof. Kitila Mkumbo?. Kwa sasa kuna mtu anaikosoa serikali kama Zitto Zuberi Kabwe?, Jee rais Magufuli anamchukia Zitto?.

Kuhusu ukosoaji, ingekuwa sikuwepo nimefanya kuhadithiwa, ningeweza kuamini, lakini kwa bahati nzuri, mimi mwenyewe ni shahidi, nilikuwepo ikulu siku rais Magufuli anazungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini, alisema wazi kuwa hachukii kukosolewa, bali ukosoaji huo ufanywe kwa nia njema na kwa lugha ya staha, tena akasisitiza anapenda challenge, sasa hii chuki ya rais Magufuli kuchukia kukosolewa ni chuki ipi hii?.

Hata swali langu mimi nililomuuliza ni swali la ukosoaji, lakini alijibu kwa kicheko na hata kuingizia utani wa maana ya jina langu, sasa hizi chuki za kukosolewa ni chuki zipi hawa The Economist, wanaozizungumzia?!.

Kama hoja ni ukosoaji wa Mhe. Tundu Lissu na kilichokuja kumtokea kwa vile shumbulizi lile limefanywa na watu wasiojulikana, hakuna uthibitisho kuwa Lissu ameshambuliwa kwa sababu ya ukosoaji
Tuacheni Ramli Chonganishi: Tusihukumu, Tusije Tukahukumiwa!. "Karma Ndio Pekee Hutoa Hukumu ya Haki Hapa Duniani!. - JamiiForums

Katika toleo hili, limekuja na kubwa ya mwaka, sio tuu kumsingizia Rais Magufuli kuwa ametamka kufuta vyama vingi, na kuirejesha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja ifikapo mwaka 2020, bali pia wamemnukuu na kumlisha maneno kwa quotation kuuaminisha ulimwengu kuwa maneno hayo ni kweli rais Magufuli ameyatamka wamedai na hapa ninanukuu,
Mr Magufuli, says, is “determined that by 2020 there will be no political opposition in Tanzania. Essentially he wants to return it to one-party rule as it was before 1992", mwisho wa kunukuu.

Japo mimi sio mfutiliaji wa karibu wa kila hotuba za rais Magufuli, lakini ni msomaji mzuri wa kila kinachoandikwa kuhusu nchi yetu na kumhusu rais wetu, hivyo sikumbuki kuwahi kumsikia rais Magufuli akisema maneno haya ya The Economist, aliyatamka lini na wapi!.

Kama kuna mtu yoyote kati yetu aliwahi kumsikia Rais Magufuli akisema atafuta upinzani na vyama vingi Tanzania mwisho ni 2020, naomba anisaidie, maana hakuna mtu anaweza kuwa amesikia kila kitu kinachosemwa na rais wetu, labda kama kazi yake ni kumsikiliza tuu rais kutwa kucha!.

Kama huu ni uongo mwingine wa Jarida hili la The Economist, kama kawaida yao na mauongo yao kuihusu nchi yetu Tanzania na Rais wetu Magufuli, lazima tufike mahali sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali uongo huu kuhusu nchi yetu, uongo kuhusu rais wetu na sometimes hadi anatukanwa, huku sisi tunakaa kimya, nchi yetu inatukanwa, tunakaa kimya, uzalendo wetu kwa taifa letu ni uzalendo gani?!. Uongo kama huu unapoachwa bila kukanushwa na ukweli ukasemwa, utakuja kugeuka ukweli na tukaanza kumtafuta mchawi!.

Hebu kwanza jisomee mwenyewe mauongo ya The Economist, nimekuwekea kila walicho andika, nikikuwekea kipi ni ukweli na kipi ni uwongo, tena nimeweka in number format.

  1. daily newspaper, the Citizen, had the cheek to mention that the Tanzanian shilling’s value at the unofficial exchange rate had been sliding. Though this was plainly the case, it flouted the country’s bizarre Statistics Act, whereby no figure may be disseminated without verification or publication by the official organs of state. Hapa wameiita sheria yetu ya Takwimu ni bizarre, jee kweli sheria yetu ya takwimu ni bizarre?, ina maana bunge letu pia ni bizzar kupitisha sheria bizarre? na rais wetu ni bizarre kuisaini sheria bizzare?. Huu ni uongo!.
  2. These days Mr Magufuli, known in Swahili as Tingatinga (the Bulldozer), tries to squash anything that gets in his way:Jee ni kweli rais anafahamika kwa jina la Tingatinga?-Huu ni uongo!, jee ni kweli rais Magufuli anapondaponda kila kinachokatiza mbele yake?. Huu ni uongo!.
  3. “I would like to tell media owners: be careful, watch it.” hapa ni kweli rais wetu alitamka haya na mimi mwenyewe nilimsikia. Jee kuna ubaya gani kuwaambia media be careful watch out?.
  4. The charge of sedition is more frequently invoked. Last week the leader of the biggest opposition party, Freeman Mbowe, was released from prison on bail after four months behind bars. But he and eight other politicians are still due to be tried for sedition for attending a banned meeting the government says incited a riot. True.
  5. According to Zitto Kabwe, another prominent opposition figure who has been arrested several times, no fewer than 17 of his colleagues face—or have recently faced—prosecution, also mainly for sedition. Four, including Mr Mbowe, have served time in prison. But the politician who most rattles Mr Magufuli may be Tundu Lissu, a member of parliament who had been arrested at least six times (including for the sin of insulting the president) before he was shot 16 times in broad daylight shortly after leaving parliament in the sleepy capital, Dodoma, over a year ago. No one has been arrested for the crime. True
  6. After a week in a coma followed by a string of operations in neighbouring Kenya and in Belgium, Mr Lissu is back in full cry, with well-aired performances at Western think-tank forums and on television abroad. He has yet to return home, but insists he will do so. True
  7. Mr Magufuli, is “determined that by 2020 there will be no political opposition in Tanzania. Essentially he wants to return it to one-party rule as it was before 1992,” Hapa ndio na mimi nimeuliza, jee hii ni kweli au ni uongo?. Nimeuliza kama kuna mtu yoyote aliyesikia atuthibitishie!.
  8. when the ruling Chama Cha Mapinduzi (ccm), or Party of the Revolution, allowed multiparty democracy. The ccm, which evolved out of the party that took over at independence from Britain in 1961, has ruled longer without a break than any other party in Africa-True
  9. A leading (but necessarily anonymous) journalist in Zanzibar, a semi-autonomous part of Tanzania, says: “There’s no more investigative journalism. Huu ni uongo, sii kweli kuwa Tanzania hatuna investigative journalism, ipo na inafanyika!.
  10. People are afraid to give you information, especially people in government. Huu ni uongo, kila siku watu wanamwaga nondo na maofisa wa serikali wanajibu hoja!.
  11. The media these days is more controlled.” huu ni ni uongo, sema tuu media imekuwa na nidhamu!.
  12. The Citizen, which is owned by Kenya’s Nation Media Group, part of the Aga Khan’s stable, may, he thinks, be sold to a Middle Eastern bigwig friendly to Mr Magufuli. This is news to me. kumbe the Citizen is up for sale?!.
  13. The office of a leading human-rights lawyer, Fatma Karume, a granddaughter of Zanzibar’s first post-independence ruler, has been bombed. Kweli ofisi za Fatma zilipigwa bomu ila sii kweli kuwa Fatma ndio the leading human right lawyer, then kina Kibatala utawaweka wapi?, tena badala ya kumtaja Fatma Karume ni mtoto wa rais wao wamemtaja kama mjukuu wa rais wakati ukweli, Fatma Karume ni mtoto wa rais na mjukuu wa rais!.
  14. Aidan Eyakuze, who runs the country’s top independent research group, Twaweza, was harassed last year when he published the results of an opinion poll that showed Mr Magufuli’s once sky-high popularity to be falling fast. True
  15. Under Mr Magufuli a raft of legislation, including on the media, cybercrime and political parties, makes it harder, often illegal, to criticise him. Huu ni uongo, kwanza sii kweli kuwa sheria zetu ni raft legislation, hakuna sheria yoyote inayosema ni illegal to criticize the president!. Sisi humu jf kila siku tunamkosoa na tunadunda!.
  16. Live television coverage of parliamentary debates, where Mr Magufuli is still castigated, has been barred. Japo ni kweli matangazo ya Bunge live yamezuiwa lakini sio kwa sababu rais Magufuli alikuwa castigated, kwa sababu matangazo hayo yalionyesha Bunge live na rais Magufuli, japo ni sehemu ya Bunge lakini sio mbunge!.
  17. The government urges citizens to redirect their anger at gay people, whom Mr Magufuli says “even cows” should condemn. Huu pia ni uongo, ni lini serikali ili tuhimiza wananchi tuwachukie mashoga?. Sikubahatika kumsikia rais Magufuli akisema hata ngombe walaani ushoga!.
  18. Western donors, who have indulged Tanzania for many decades, at one point paying for more than a quarter of its annual budget, are losing patience. The head of the European Union mission, Roeland van de Geer, had to quit his post late last year. The Danes and the eu have withheld tranches of aid. Mr Magufuli is looking to the Middle East and China for less conditional help. True
  19. The president has been foolish in economic matters too. Hapa wamemtukana rais wetu kuwa ni ...(sijalirudia tukano ili na mimi nisiwe nimetukana)!.
  20. The effect of his closure of the Citizen was the opposite of what he intended. Huu ni uongo, serikali ilipofungia the Citizen, hakuna kitu ili intend to gain zaidi ya kutoa funzo kwa the citizen to be more carefull!.
  21. The shilling’s true rate dipped further. True
  22. After Mr Magufuli’s row with the paper, capital is reckoned to have fled to Kenya, which Mr Magufuli views as an adversary. Foreign-exchange controls are widely said to be imminent. Huu ni uongo, eti mitaji imehamia Kenya kwa sababu tuu the Citizen lilifungwa kwa wiki moja!.
  23. Two years ago Mr Magufuli appalled investors by demanding that the country’s biggest mining company, Acacia Mining, a subsidiary of Barrick Gold, based in Canada, should pay the absurd sum of $193bn in back taxes—about four times Tanzania’s gdp—for allegedly undervaluing its gold exports. Si kweli uamuzi wa kuwadai Acacia uli wa appalled investors, kiwango sio $193bn ni 191bn. Kiwango hicho ndicho walichotuibia na sio absurd!.
  24. Acacia’s gold exports have since dipped sharply. True
  25. Several past and present Acacia officials were arrested last year. True
  26. The World Bank says foreign investment since 2014 has more than halved. Huu ni uongo, investments zinapaa, Tanzania ndio tunaongoza nchi za EAC.
  27. “A lot of us are jittery,” says a businessman in Dar es Salaam, the commercial capital. Ni kweli vyuma vimekaza!.
  28. “But it’s the unpredictability that really scares us.” huu ni uongo, kuna unpredictability gani?!.
Uongo kama huu unapoachwa, na kuendelea kurudiwa rudiwa, sio tuu utapelekea dunia kuuona kama ni ukweli, bali utakuja kugeuka ndio ukweli wenyewe!, na wakati huo ukifika uongo huu ukageuka ukweli, ndio kuna watu watajifanya kushangaa!. Muda huo ukifika, nitakacho kifanya mimi ni kuwakumbusha tuu!.

My Take
Kuhusu Magufuli na Vyama Vingi Tanzania as far as 2020 is concerned
Baada ya ujio wa rais Magufuli, niliuliza
Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani Makini? - Prof. Kitila Mkumbo - JamiiForums

Rais Magufuli alipoanza kuchapa kazi kwa kasi kuleta maendekeo, nikauliza Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums

Kufuatia kazi nzuri inayofanywa na Rais Magufuli, wapinzani wao wenyewe kwa ridhaa zao wakaamua kuunga mkono juhudi za rais Magufuli, hivyo nikashauri
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja? - JamiiForums

Na kitu mimi ninachokumbuka kusikia ni kuwa CCM itatawala milele, hivyo nami nikawahimiza watu humu
Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!. - JamiiForums

Hivyo ikitokea uwongo huu wa Rais Magufuli kuua upinzani, na Uchaguzi Mkuu wa 2020 kuirudisha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja, CCM kutimia, hili litatokana na hayo niliyoeleza kujumlisha na uongo kama huu ulioumbwa kwa kauli zenye nguvu ya uumbaji, na kuithibitisha ile kauli ya "lisemwalo lipo, kama halipo linakuja!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Rejea za Mauongo Mengine ya The Economist kuhusu Tanzania na rais wetu.

Tanzania yaitwa Rot!, Wapinzani Wahongwa Milioni 60! Zitto Tishio kwa JPM, Wasomi Wetu Waitwa "Sycophantic Academics"!, is This True?, Is it Fair?. - JamiiForums

The Economist kuhusu Tanzania: Jarida linaona mapungufu tu kuihusu Tanzania!, Hivi kweli Tanzania hakuna mazuri yotote ya kuyaangazia?!. - JamiiForums

Uzalendo wa Ajabu wa Watanzania, Nchi Yako Inatukanwa!, Rais Wako Anatukanwa!, Tumenyamaza!. Huu Ni Uzalendo Gani?!. - JamiiForums

‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist" - JamiiForums

Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli? Kama si kweli, Tusiukubali Uongo huu, Tuukanushe! - JamiiForums

Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu Magufuli kuwa ni Dikteta! - JamiiForums

Jarida la The Economist ladai uchumi wa Tanzania unaporomoka, lahamasisha Rais Magufuli adhibitiwe kwa vikwazo kiuchumi - JamiiForums

Rais Magufuli ametukanwa tena na Jarida la Economist. Tukiendelea kunyamaza, itafika siku Uongo huu utageuka Ukweli! - JamiiForums

Huku sio kudhalilishwa kwa Rais wetu na Media za Nje? Je, watanzania tukubali, Tukae kimya? - JamiiForums

Kumbe Jarida La The Economist Sometimes Linaweza Kuandika Jambo Jema Kuhusu Tanzania!, Lamsifu Ifakara Health Institute Kwa Utafiti wa Malaria Afrika. - JamiiForums
 
Wanabodi,
Hili Jarida la The Economist, kama kawaida yake, kila likiandika kuhusu Tanzania, kwanza lazima limtukane rais wetu, pili lazima litunge vitu vya uongo kuhusu Tanzania, tatu lazima litunge uongo kumsingizia Rais Magufuli jambo lolote na kutangazia ulimwengu.

Katika toleo lake la leo Machi 16, limekuja na kubwa ya mwaka, sio tuu kumsingizia Rais Magufuli kuwa ametamka kufuta vyama vingi, na kuiresha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja ifikapo mwaka 2020, bali pia wamemnukuu na kumlisha maneno kwa quotation kuuaminisha ulimwengu kuwa maneno hayo ni kweli rais Magufuli ameyasema.

Japo mimi sio mfutiliaji wa karibu wa kila hotuba za rais Magufuli, lakini ni msomaji mzuri wa kila kinachoandikwa kuhusu nchi yetu na kumhusu rais wetu, hivyo sikumbuki kuwahi kumsikia maneno haya ya The Economist, aliyatamka lini na wapi?.

Kama kuna mtu yoyote aliwahi kumsikia Rais Magufuli akisema atafuta vyama vingi, mwisho ni 2020, naomba anisaidie.

Kama huu ni uwongo mwingine wa Jarida hili la The Economist, kama kawaida yao na mauongo kuhusu nchi yetu Tanzania na Rais wetu Magufuli, lazima tufike mahali sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali, rais wetu anatukanwa, tunakaa kimya, nchi yetu inatukanwa, tunakaa kimya
Kwa anayoyafanya Jiwe si lazima atangaze redioni, ukatili anaofanya dhidi ya vyama, viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani ni sawa na tangazo la kuvifuta. Labda kama wewe unaangalia kwa makengeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Pascal haya mambo yalishajadiliwa sana hapa jukwaani.... hata kama si kwa kauli thabit lakini hata matendo wakati wa chaguzi ndogo za madiwani na wabunge zimedhihirisha hivo. ...
Bado manunuzi ya Jumla na reja reja....
Huitaji degree kujua ukwel huo...
 
Wanabodi,
Hili Jarida la The Economist, kama kawaida yake, kila likiandika kuhusu Tanzania, kwanza lazima limtukane rais wetu, pili lazima litunge vitu vya uongo kuhusu Tanzania, tatu lazima litunge uongo kumsingizia Rais Magufuli jambo lolote na kutangazia ulimwengu.

Katika toleo lake la leo Machi 16, limekuja na kubwa ya mwaka, sio tuu kumsingizia Rais Magufuli kuwa ametamka kufuta vyama vingi, na kuiresha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja ifikapo mwaka 2020, bali pia wamemnukuu na kumlisha maneno kwa quotation kuuaminisha ulimwengu kuwa maneno hayo ni kweli rais Magufuli ameyasema.

Japo mimi sio mfutiliaji wa karibu wa kila hotuba za rais Magufuli, lakini ni msomaji mzuri wa kila kinachoandikwa kuhusu nchi yetu na kumhusu rais wetu, hivyo sikumbuki kuwahi kumsikia maneno haya ya The Economist, aliyatamka lini na wapi?.

Kama kuna mtu yoyote aliwahi kumsikia Rais Magufuli akisema atafuta vyama vingi, mwisho ni 2020, naomba anisaidie.

Kama huu ni uwongo mwingine wa Jarida hili la The Economist, kama kawaida yao na mauongo kuhusu nchi yetu Tanzania na Rais wetu Magufuli, lazima tufike mahali sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali, rais wetu anatukanwa, tunakaa kimya, nchi yetu inatukanwa, tunakaa kimya

Kaka paskali unajua kuna wakati mwingine kauli zetu za kisiasa huwa zinaweza kuleta mkanganyiko kwa wale ambao huwa wanazitransilate kwa wakubwa huko duniani

Hilo gazeti huwa alizushi kitu ni either kiliongelewa au kiliandikwa kwenye magazeti hata kama hiyo kauli maybe haikuwa na madhara wakati inatamkwa

Mfano leo mtu wa ngazi ya juu wa ccm akisema tunataka chama kimoja, sisi wabongo tutajua ni kauli hazina madhara Coz zipo kila siku ila baloz akiuliza kwa shushu wake kuwa huyo kiongozi wa juu amesemaje? Atajibiwa amesema wanataka chama kimoja

Hapo sasa ndio shida inakuja
 
Unajua ndugu yangu Pasco unapoteza kabisa focus linapokuja suala la The Economist na matokeo yake hivi sasa umeamua kuwazulia uongo!

Walichoandika The Economist ni hiki:-
After a week in a coma followed by a string of operations in neighbouring Kenya and in Belgium, Mr Lissu is back in full cry, with well-aired performances at Western think-tank forums and on television abroad. He has yet to return home, but insists he will do so. Mr Magufuli, he says, is “determined that by 2020 there will be no political opposition in Tanzania. Essentially he wants to return it to one-party rule as it was before 1992,” when the ruling Chama Cha Mapinduzi (ccm), or Party of the Revolution, allowed multiparty democracy. The ccm, which evolved out of the party that took over at independence from Britain in 1961, has ruled longer without a break than any other party in Africa.
Hapo kwenye BLUE wameweka hadi quotation mark kuonesha hiyo sio kauli yao bali kuna mtu wamemnukuu!

UKiangalia hapo juu, utaona The Economist wamemnukuu Tundu Lissu ambae ni kweli alitamka hayo maneno!

Na ukisoma hiyo nukuu, Tundu Lissu hajasema Magufuli anataka kufuta vyama vya upinzani lakini maoni ya Tundu Lissu yametoakana na uhalisia wa kisiasa hapa nchini!!

Ni Rais Magufuli ndie alitangaza kupiga marufuku shughuli za kisiasa at national level! Marufuku hii inatekelezwa barabara dhidi ya upinzani lakini CCM na serikali yake bado wanaendelea kufanya siasa katika ngazi ya kitaifa!!!

Sote tumeshuhudia assassination attempt dhidi ya TL let alone unknown whereabouts za mtu kama Ben Saanane!

Hivi kuna mjadala kuhusu manyanyaso wanayopitia viongozi wa upinzani?! Sote tumeshuhudia Mheshimiwa Mbowe akifanyiwa fitina na kuwekwa ndani kwa zaidi ya miezi 3 huku akifutiwa dhamana!!

Haina sababu ya kurudia kuelezea matukio! Kila mwenye kutaka kufahamu anafahamu ugumu wa upinzani kurudi bungeni hapo 2020! Itakuwa ngumu sana si kwa sababu CCM na utawala wake wamegeuka kuwa bora bali kwa sababu kuna jitihada za makusudi za kuhakikisha wapinzani hawafurukuti.

Nitakuwa mwehu nikijifanya siioni nia ya Magufuli ya kutaka bunge litakalopiga mihuri kila agenda yake pasipo na kuhoji!!

NI nini basi tafsiri ya hali hiyo kama sio nia ya Magufuli kutotaka upinzani?! Hivi kweli hata wale wana-CCM wasiopenda unafiki wa kisiasa hawaioni nia hii ya utawala wa Magufuli?!
 
Maongo sana hayo maEconomist, Rais wetu mtukufu,mtakatifu,mungu mtu na kiongozi wa malaika hajawahi sema atavifuta vyama vya siasa ila alisema kufikikia 2020 atahakikisha hakuna vyama vya upinzani Tanzania........sasa hatujui atatumia njia gani ila tunaona VIONGOZI WA UPINZANI WAKIPIGWA RISASI,WENGINE MAGEREZANI MIEZI MITATU ETI WAMEKWEPA DHAMANA,WENGINE WANAUAWA,WENGINE WANAPOTEA WENGINE WANATEKWA, MaEconomist yaache uongo kwani kufanya hivyo ni kufuta vyama vya upinzani
CCM OYEEE
MAENDELEO HAYANA CHAMA.
 
Wanabodi,
Hili Jarida la The Economist, kama kawaida yake, kila likiandika kuhusu Tanzania, kwanza lazima limtukane rais wetu, pili lazima litunge vitu vya uongo kuhusu Tanzania, tatu lazima litunge uongo kumsingizia Rais Magufuli jambo lolote na kutangazia ulimwengu.

Katika toleo lake la leo Machi 16, limekuja na kubwa ya mwaka, sio tuu kumsingizia Rais Magufuli kuwa ametamka kufuta vyama vingi, na kuiresha Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja ifikapo mwaka 2020, bali pia wamemnukuu na kumlisha maneno kwa quotation kuuaminisha ulimwengu kuwa maneno hayo ni kweli rais Magufuli ameyasema.

Japo mimi sio mfutiliaji wa karibu wa kila hotuba za rais Magufuli, lakini ni msomaji mzuri wa kila kinachoandikwa kuhusu nchi yetu na kumhusu rais wetu, hivyo sikumbuki kuwahi kumsikia maneno haya ya The Economist, aliyatamka lini na wapi?.

Kama kuna mtu yoyote aliwahi kumsikia Rais Magufuli akisema atafuta vyama vingi, mwisho ni 2020, naomba anisaidie.

Kama huu ni uwongo mwingine wa Jarida hili la The Economist, kama kawaida yao na mauongo kuhusu nchi yetu Tanzania na Rais wetu Magufuli, lazima tufike mahali sisi Watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali, rais wetu anatukanwa, tunakaa kimya, nchi yetu inatukanwa, tunakaa kimya
Wewe habari ya kuunga juhudi huifahamu? Wapinzani wote wanakesi mahakamani wewe hujui? niko mahali nimesimama nakuona kama vile unajiotesha wakati ndiyo hali halisi inayoendelea nchini kwa hivi sasa, democracy hakuna vyombo vya habari vimezibwa mdomo ukiwa kama mwana habari huru kama unavyojiita leo hii hii habari uliyoandika ingekuwa ni yakuponda wala I'D yako hapa isingekuwa pascal Mayalla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom