Baridi kali yaua watu 50 Taiwan

Baridi kali yaua watu 50 Taiwan

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
160124140048_taiwan_512x288_bbc_nocredit.jpg

Watu zaidi ya 50 wamefariki nchini Taiwan kutokana na wimbi la baridi kali ambalo limeathiri maeneo ya Asia Mashariki.

Watalii zaidi ya 60,000 pia wamekwama Korea Kusini kutokana na kibaridi hicho.

Vyombo vya habari nchini Taiwan vinasema vifo hivyo vimetokana na kushuka sana kwa kiwango cha joto mwilini na wengine wakafariki kutokana na maradhi ya moyo.

Hii ni baada ya viwango vya joto kushuka ghafla wikendi.

Hayo yakijiri, theluji nyingi imesababisha kufungwa kwa uwanja wa ndege katika kisiwa cha Jeju nchini Korea Kusini, ambacho ni maarufu sana kwa watalii.

Safari za ndege zimekatizwa.

Wimbi hilo la baridi limeathiri sana Hong Kong, Uchina kusini na Japan.

Walioathirika zaidi Taiwan ni wazee wanaoishi maeneo ya kaskazini kama vile Taipei, Kaohsiung na Taoyuan.

Katika baadhi ya maeneo ya Taiwan, viwango vya joto vilishuka hadi nyuzi 4C (39F) siku ya Jumapili.

Hong Kong, hali ilikuwa mbaya zaidi, baadhi ya maeneo yakishuhudia vipimo vya joto vya nyuzi 3C, kikiwa ndicho kiwango cha chini zaidi kushuhudiwa eneo hilo katika kipindi cha miaka 60.

Chanzo: BBC
 
Kwa hakika Mungu ametupendela sana watanzania. Katupa joto la wastani binadamu kuishi kwa salama; katupa mvua za wastani mimea pori na wanyama mwitu waishi kwa amani nasi tupande na kuvuna bila tatizo. Ila kwa katunyima kitu kimoja; uwezo wa kutumia mazingira yetu aliyotujalia kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
Elimu ndio itawasaidia zaidi.
 
Mbeya nyuzi joto iliwahi kushuka na kufikia 4°c lakini hatukusikia habari za vifo.
 
Kuna baadhi ya nchi wanaishi kwa mashaka mno ndio maana nasema mara nyingi pepo iko Afrika na kule ni jehanam
-baridi kali wao
-Joto kali wao
-vimbunga wao
-matetemeko wao
-dhoruba wao
 
Kuna baadhi ya nchi wanaishi kwa mashaka mno ndio maana nasema mara nyingi pepo iko Afrika na kule ni jehanam
-baridi kali wao
-Joto kali wao
-vimbunga wao
-matetemeko wao
-dhoruba wao
Kutokana na majanga hayo thats why wako very prepared katika disaster compared to us, na jitihada zao hizo zimeweza kuzuia vifo vitokanavyo na baadhi ya matukio, ajali zinapoteza idadi ya watu kwetu ukilinganisha na wao vitu kama ajali ni nadra tena labda za ndege,mvua tuu zinazonyesha Taiwan na baadhi ya nchi za Asia kila siku kwa Tz au most part of Africa ingekuwa mafuriko daily, hapo sijazungumzia suala la magonjwa yanayotumaliza Africa, serikali na viongozi wetu,rushwa, so point yako ya kuwa Africa ni peponi na Asia ni Jehanam sidhani kama umekuwa na mlinganisho mzuri
 
Nimezungumzia kwa hayo majanga ya kiasili ambayo kwa namna yoyote ile hayazuiliki
Hivi vitu kama magonjwa ajali na vita ni man made disasters, ambavyo hatuwezi kuviweka kwenye kundi moja na majanga ya kiasili
 
In that case i got you, hiyo iko wazi cse geographically Africa is on top of rocks so tumependelewa kwa kiasi fulani
 
Back
Top Bottom