Elections 2010 Baregu na Chadema msikurupuke

JAYJAY
hongera kwa kupost.
ngeu ni sehemu ya maisha ya shujaa anayeamini haki hulipiwa gharama
 
Kuna Prof. Maji marefu aliyeshinda Ubunge jimbo la Korogwe vijijini. Kikwete alimnadi kuwa ni Prof.safi watu wamchague.
CV yake:
  1. Darasa la 7.
  2. Mganga wa kienyeji.
Hakika CCM ina majuha watupu. Sijui kwanini Watanzania wengi hawalioni hili na wanaendelea kuchagua mijitu ambayo haijaenda hata shule.
Kazi kwelikweli.

Guys, inaelekea hamjui hata kuwa mlikuwa na mgombea mwenza muuza samaki wa darasa la saba....Acheni kudhihaki wa wengine wakati wenu mnaona aibu hata kumtaja.......

Usomi sio uongozi bali ni nyenzo inayohakikisha upeo mpana wa kimawazo na kimtazamo wa kiongozi. Lakini pia kumbukeni kuwa academic credentials ni ushahidi tu wa kuonyesha mapungufu uliyonayo katika weledi wa masuala mbalimbali na hivyo sio cheti cha kukufanya udharau wasio navyo......

Lakini pia, unapomkejeli asiyesoma ama mwenye elimu ya msingi tu ujue kuwa unakajeli zaidi ya watanzania asilimia themanini ambao ndio ngome ya wenzenu......
 
Mmefanya vizuri kutoa tamko leo NEXT STEP kesho na si kesho kutwa njooni na matokeo kamili at least ya jimbo moja mmwape waandishi wa habari na external observers.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom