Barbara Gonzalez CEO wa Simba SC nakukubali kiutendaji, ila acha kumdharau Senzo Mazingisa kwani hujafikia hata 15% tu ya uwezo wake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,925
BARBARA AMKATAA SENZO "sio Type Yangu"

Kuhusu kufananishwa na yule bwana wa upande wa pili nisingependa kujibu kwa sababu haina tija, Mimi sisumbuliwi na propaganda za watu kabisa.

Nimesimama imara, najiamini kwenye uwezo wangu, Kama mtu anatafuta sehemu ya kuji-brand, namuona mtu huyo ni mwepesi. Sisumbuliwi hata kidogo.

Mimi ni mweledi, najua uwezo wangu na huwezi kunifananisha na mtu ambaye hana ‘class’ yangu ( Senzo is not my type)

Chanzo: cloudsfmtz na simba_breaking_news

Mimi ni Simba SC Mwenzako ila sijazoea Unafiki na hupenda kuwa Mkweli hata kama 'nitawaudhi' Watu. Barbara Gonzalez CEO wa Simba SC bado una mengi hasa ya 'Kiutendaji' ya 'Kujifunza' kutoka Kwake Senzo Mazingisa aliyeko kwa Watani zetu sasa Yanga SC. Kiburi chako cha Pesa na kuwa karibu na 'Mwekezaji' Mo Dewji hasa 'Kimahusiano' yenu kusikufanye nawe ujione ni Tajiri Afrika. CV ya Senzo Mazingisa haitishi tu hapa Tanzania bali hata huko CAF na FIFA pia anatambulika na kuheshimika pia.

Barbara Gonzalez ifuatayo hapa chini ni sehemu ya Uzoefu wa Kiutendaji wa aliyekuwa CEO wa Simba SC Senzo Mazingiza ili ujue kuwa haumpati

1. 2010 South Africa World Cup Coordinator
2. FIFA Confederation Cup 2009 Event Coordinator
3. South Africa Tournament Director
4. PSL Ticketing and Security Committee Director
5. CAF Symposium Delegate Director
6. General Manager at Platinum Stars Football
7. Orlando Pirates Director of Administration
 
Ni nani anamiliki hiki chombo bwana popoma?

Utani.

Sema huyu dada ana uswahili sana ndani yake..

Huo "uswahili" sio lafidhi (accent) tu bali hata vijimichambo vyake.
Mwenye CV yake aweke link tafadhali
 
Nakumbuka huyu dada alikuwa anapigiwa simu na waandishi wa habari hapokei, alikuwa muoga, Sasa ashaanza kujanjaruka, tutampima vizur kwenye kipindi kigum Cha team, saiv atatamba sana kwa sabab hamna matatzo kwenye team na Mo yupo nyuma yake, hapo yupo Kama shadow tu
 
Usimfananishe Marina na Barbara Marina alikuwa Kama assistant kwa miaka 10+ pale the blues kabla ya kuwa top..
Sijamfananisha kwa experience au uwezo..nimesema walikotokea wote wanafanana..walikuwa wanafanya kazi tofauti kwa hao mabosi kabla ya kuingia kwenye mpira
 
Naona umetoka kifungoni na wenge!! Hivi una uhakika kuwa CEO ana mahusiano na mwekezaji wa Simbasc?!! Au umeamua tu kuchafua jina la mwekezaji?!! Uyo mr Mazingira una uhakika CV yake inaendana na utendaji wake?!!
 
BARBARA AMKATAA SENZO "sio Type Yangu"

Kuhusu kufananishwa na yule bwana wa upande wa pili nisingependa kujibu kwa sababu haina tija, Mimi sisumbuliwi na propaganda za watu kabisa.

Nimesimama imara, najiamini kwenye uwezo wangu, Kama mtu anatafuta sehemu ya kuji-brand, namuona mtu huyo ni mwepesi. Sisumbuliwi hata kidogo.

Mimi ni mweledi, najua uwezo wangu na huwezi kunifananisha na mtu ambaye hana ‘class’ yangu ( Senzo is not my type)

Chanzo: cloudsfmtz na simba_breaking_news

Mimi ni Simba SC Mwenzako ila sijazoea Unafiki na hupenda kuwa Mkweli hata kama 'nitawaudhi' Watu. Barbara Gonzalez CEO wa Simba SC bado una mengi hasa ya 'Kiutendaji' ya 'Kujifunza' kutoka Kwake Senzo Mazingisa aliyeko kwa Watani zetu sasa Yanga SC. Kiburi chako cha Pesa na kuwa karibu na 'Mwekezaji' Mo Dewji hasa 'Kimahusiano' yenu kusikufanye nawe ujione ni Tajiri Afrika. CV ya Senzo Mazingisa haitishi tu hapa Tanzania bali hata huko CAF na FIFA pia anatambulika na kuheshimika pia.
Mtoa post unaonekana kumfagilia Senzo sana.
 
Babra amemzidi Senzo elimu, hana elimu ya kuungaunga kama kina sisi.
Hivi mliwahi jiuliza kilichomtoa huyo Senzo huko kwao mpaka aka apply kazi Simba?
Senzo is Overrated, amekuwepo simba hatukuona maajab yoyote simba ilibaki kuwa ile ile.
Kuhusu senzo kuwa na CV kubwa, je hiyo CV ndo inayofanya kazi?
Kwasababu senzo ana CV kubwa ina maana watu wengine hawaruhusiwi kujenga CV zao?
Hivi Unadhani kuwa Assistant wa bilionea ni kitu rahisi? Lazima ana uwezo mkubwa ila atapingwa sana sababu ya jinsia yake.
 
Back
Top Bottom