Baraza la usuluhishi la kata linaweza kutoa talaka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la usuluhishi la kata linaweza kutoa talaka?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Polisi, Mar 31, 2012.

 1. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wakuu naomba nitoe case study ya kesi ya ndoa ambayo imeamuliwa jana na baraza la usuluhishi la kata
  Taarifa muhimu
  - ndoa ya kimila
  - wamekaa zaidi ya miaka 7
  - wana watoto watatu, wawili wana chini ya miaka 5. wawili wanakaa na mume, mmoja ananyonya na yuko na mama
  yake
  - wana nyumba 2, moja walikuwa wakiishi
  - Gari 2
  - Wana duka la consumables
  - mke aliondoka mwaka jana kwenda kutibiwa kwa mganga wa jadi kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua na
  kipindi hicho alikuwa mjamzito
  - mume hakwenda kumwona tena mke hata alipojifungua
  - Huku nyuma mume alioa, akauza gari na nyumba akaipangisha

  Maamuzi: Talaka imetolewa na baraza la usuluhishi la kata kwa kuwa wao kwa pamoja mke na mume wamekubaliana kwa kuzingatia MKE ALITOROKA.

  MGAWANYO WA MALI NA WATOTO
  1. Duka, mume alipewa mtaji na kaka yake, hivyo mke hana chake
  2. nyumba ni ya watoto MKE hana chake
  3. Gari moja liliuzwa kwa kuwa lilikuwa la mkopo na liliopo pia ni la mkopo mke hana chake
  4. Nyumba moja imepangishwa (waliyokuwa wanaishi)
  5. Nyumba ya pili anakaa na mke wake mpya
  6. Atapewa cherehani moja, sh. 275,000 za kuanzia maisha, kabati na vyombo vya ndani
  7. Atakuwa anapewa sh. 10,000 kila mwezi excluding matibabu

  NAOMBA USHAURI KUHUSU UHALALI WA BARAZA LA KATA KUTOA TALAKA NA VIGEZO VYA KUGAWA MALI VILIVYOTUMIKA KAMA NI HALALI
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mkuu Polisi wewe ni Polisi wa Tanzania au FBI Polisi wa Amerika ? Polisi mzima sheria za Jamii forums huzijuwi kwanini?Hii thread uliyeanzisha hapa sipo mahali pake umekosea sana hapa ni mahali pa J.F. Doctor sio mahali pa kuanzisha mambo yanayohusiana na sheria Mkuu inaonyesha wewe huzijuwi sheria za Jamii forums? hii Thread yako ingelifaa kuwekwa kwenye jukwaa la sheria hapa hebu bonyeza Jukwaa la Sheria (The Law Forum) Samahani kama nitakukwaza.
   
 3. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mkuu MM niwie radhi ndugu nilipitiwa. Nadhani wahusika wataipeleka mahali husika
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  itabidi huyo mke wa zamani atafute petroli safi yani ile super ambayo haijachakachuliwa halafu ani pm nimpe mbinu za kuhakikisha kunapatikana usawa.
   
 5. K

  Kacharimbe JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hangover ya gongo noma sana
   
 6. M

  Mtoa Mada New Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa ufupi tu ni kwamba hakuna sheria yoyote inayotoa mamlaka kwa baraza la usuluhishi kutoa talaka kwa ndoa ya aina yoyote ile, ila kwa mujibu wa sheria ya ndoa sura ya 29 ya sheria kuu za Tanzania kama ilivyorudiwa mwaka 2002, kifungu cha104(5) cha sheria hiyo kinalipa baraza mamlaka ya kufanya usuluhishi tu na kama kuna uhitaji wa talaka ina maana mahakama hutaarifiwa na bodi kwamba usuluhishi umeshindikana na mahakama hapo ndio inayoamua kama itoe talaka au la.
   
 7. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ok. Sasa hili ilmetokea. Baraza la kata limeridhia wanandoa watengane na limetoa 'talaka ya hiari' kwa tafsiri kuwa wanandoa wao wamekubaliana kwa hiari na kwamba hakuna mabishano kuhusu mtoto wala mali. Baraza pia likafanya mgawanyo wa mali. Katika hali kama hii endapo mke anaona hakutendewa haki achukue hatua gani?
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tatizo kubwa hapa wala si jinsi walivyogawana mali, bali ni hilo baraza la kata lilivyojichukulia mamlaka ambayo si yake. Kisheria, Baraza la usuhishi la Kata halima mamlaka ya kutoa talaka. Kama lilivyo jina lake, kitu ambacho baraza hili linapaswa kufanya ni kusuluhisha wanaogombana. iwapo itashindikana, linapeleka shauri hilo mbele-mahakamani.
  Baraza haliwezi kuvunja hati ya ndoa ambayo halikuitoa
   
 9. M

  Majamba Jr Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu hilo ni baraza la usuluhishi na co baraza la talaka. Tafsiri yake ni nini basi!Sheria ya Ndoa ya1971 ambayo imefanyiwa mapitio mwaka 2002 chini ya Kifungu cha 104(5)kinatoa mamlaka kwa baraza la usuluhishi la ndoa kuwapatanisha kwa kusuluhisha tatizo la ndoa yao. Kama wanandoa watapatana hapo baraza litakuwa limefanikiwa malengo yake. Inapotokea baraza hilo kushindwa kuwasuluhisha wanandoa kama ambavyo imetokea hapa hata kama wanandoa wamekubaliana kuachana baraza haliwezi kutoa TALAKA bali litatoa cheti cha usuluhishi ambacho ndani yake wateleza kuwa wameshindwa kuwapatanisha wanandoa husika na kwamba wenyewe wanasisitiza ndoa ivunjwe. Kwa mujibu huo baraza linapendekeza suala liende mahakama husika kwa madai ya kuvunja ndoa on the ground that the marriage is irreperably broken down. Upon instituting such a claim b4 a compitent court and upon issuing the certificate frm the Marriage Concilliation body,the court shall intertain the matter and grant a divorce order and finally divorce decree.

  MATRIMONIAL PROPERTY
  Baraza la usuluhishi halina mamlaka ya kugawa mali za ndoa kwa namna yoyote ile.Mahakama pekee ndo inavigezo vya kuzingatia ktk ugawaji wa matrimonial properties hasa pale ambapo wanandoa wametofautiana ktk kugawana mali hzo.

  KWAHIYO
  Katika tatizo hili;
  -Namshauri mwanamke aombe cheti cha usuluhishi toka Baraza la Usuluhishi.
  -Baada ya kupata cheti,aende akafungue kesi ya kudai talaka mahakamani

  AU

  Aende akachallenge Talaka ilotolewa na hilo Baraza kwenye compitent court.Obviously the court will quash and declere such a divorce decree void,if divorce decree is declered void then this will automatically quash the property distribution order granted by the Marriage Concilliation Body.

  Thats all i know brother.
   
 10. m

  mchangia mada New Member

  #10
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala linalofuata hapo ni kwamba mlalamikaji, ambaye ni mwanamke anaweza kwenda mahakama ya mwanzo kupinga maamuzi ya baraza kwa 7bu limeamua mambo yaliyo nje ya mamlaka yake kisheria..
   
 11. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #11
  Jan 15, 2015
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Je inawezekana Mahakama kutoa talaka bila wahusika kupitia baraza la usuluhishi?

   
 12. D

  Dunia Tabu Member

  #12
  Jan 16, 2015
  Joined: Jun 25, 2014
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kisheria hii tunaita ULTRA VIRES.
  hilo baraza limevuka mipaka yake kiutendaji. kama walivyoshauri wengine, cha msingi huyo mwanamke akafungue kesi mahakamani kupinga mahamuzi hayo ya baraza. mahakama itatupilia mbali maamuzi ya baraza kutoa talaka na kugawa mali na itaamuru hilo baraza litoe cheti cha kushindwa kuwapatanisha wanandoa. then mahakama itaamua kutoa talaka au laa. na kama itatoa talaka basi mali za wanandoa zitagawanya kwa sheria ya kimila ambayo wanandoa waliitumia kufungia ndoa.
   
 13. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2015
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Baraza la Usuluhishi la Kata halina uwezo/mamlaka ya Kutoa Talaka.

  Bali linaweza kushiriki katika hatua za awali za kusuluhishana, muhafaka usipofikiwa ndipo inashauriwa kwa ambaye hajaridhika kupeleka shauri lake kwenye iliyojuu ya Baraza la kata(Mahakama) kwa uamuzi, vigezo na masharti ni kwa jinsi wajumbe walivyokwisha eleza.
   
 14. T

  THE LEARNED COUNSEL Member

  #14
  Jan 22, 2015
  Joined: Nov 24, 2014
  Messages: 57
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  1/ni kweli kabisa kuwa mamlaka ya balaza la kata ni ya usuluhishi tu, balaza linamamlaka ya kusuruhisha ndoa ambazo zina migogoro kwa lengo la kujaribu kupatanisha ili kuepusha kuvunja ndoa. katika hatua hii kama litashindwa kusuruhisha basi hutoa certificate kwa mahakama kuitaarifu kuwa limeshindwa kusukuhisha hivyo kushauri mahakama kutoa talaka.
  2/ migogoro yote ya ndoa lazma ianzie ktk mabalaza ya usuruhishi kama hatua ya awali kabla ya kupelekwa mahakamani. hivyo mahakama hairuhusiwi kutoa talaka bila kuwa na hati kutika balaza la usuruhishi inayoonesha kuwa wameshindwa kupatanisha. hata hivyo kuna manzingira yanayo weza kuruhusu mtu kwenda mahakamani bila kupitia balaza la usuruhishi.
  3/kama balaza la kata halina uwezo wa kutoa talaka basi automatically haalina uwezo wa kugawa mali za wadaawa. hii ni kutikana kuwa sheria inataka mahakama inayotoa talaka pia kuamua juu ya mgawanyo wa mali na matunzo ya watoto. kutoa talaka na kushindwa kugawanya mali ni kosa kisheria.
  4/ mgawanyo wa mali za wadaawa hufanyika katika mali za pamoja. mali inayo milikiwa binafsi haita husika katika mgawanyo.
  5/ mdaawa pia anahaki ya kupata mali kutoka ktk mali binafsi ya mwenzake iwapo alichangia katika kuiendeleza moja kwa moja ama kimazingira.
  6/ mgawanyo wa mali za pamoja huzingatia mchango wa kila mtu katika upatikanaji wa mali hiyo na kuiendeleza.
  7/ ktk talaka hakuna mali ya mtoto, watoto hupata mgao kama ni mambo ya urithi sio talaka. malizote hugawanywa miongoni mwa mke na mme.
   
 15. Apologise lady

  Apologise lady JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2015
  Joined: Sep 16, 2013
  Messages: 6,007
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Huo mgawanyo wa mali mimi sijauelewa kabisaaa, Yaani mume wangu akipewa mtaji hata na baba yake ajaja tukafanya biashara wote, mimi sina changu????? huyo mama kama ameishi na huyo baba miaka 7 kwanini asipeweb hata nyumba moja????? hapo nilichoona huyo baba kadili na hao wajinga ili wamnyime haki huyo mama.
  Lakini huyo mama nae kwa mganga anakaa mwaka mzima jamani wanawake hii mbona haijakaa sawa.
   
 16. The Don

  The Don JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2015
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 3,455
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  mali za wanandoa zipo zile zinazomilikiwa na kila mmoja kipekee/separate property s.58 na 60,s.59 imeeleza mali za pamoja za familia ikiwa ni zile walizochuma pamoja kipindi cha ndoa,juhudi za pamoja hujumuisha hata kazi za kina mama wa nyumbani hivo ana haki ya kugaiwa mali kama talaka itatolewa kiusahihi,refer Bi hawa mohammed v ally seif(1983) TLR
   
Loading...