Baraza la mawaziri Tanzania halina uzalendo !!


Tango73

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Messages
1,678
Likes
44
Points
135
Tango73

Tango73

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2008
1,678 44 135
Ndugu watanzania!
Mumegundua kuwa baraza la mawaziri la tanzania halina uzalendo? Yaani hawajali kabisaa kuipeleka nchi na watu wake katika malisho mema. Hii ni hatari sana maana kila waziri kageuza wizara yake ni chimbo la nguvu la madini. Ukianzia wizara ya nishati na madini, huko kuna sikititisha kuona kuwa waziri na katibu wake hawajui hata kuokoa wananchi ili wapate umeme wa kutosha.

Kashfa ya kuwahonga wabunge ili wasiohoji bajeti ya wizara ya madini, ni kitendo kisicho cha kizarendo kabisaa. Ukija wizara ya utalii, ndiko utazania inamilikiwa na waarabu. Maana kitendo cha taifa la kiarabu kuingia hapa nchini na kubeba twiga 133 si cha kizalendo kabisaa. Ukija wizara ya mambo ya nje, utaona wanamkemea balozi wa Libya, eti kapandisha bendera ya NTC badala ile ya utawala wa Gadafi!

Jamani Gadafi huyu aliyeshirikiana na Iddi amini kuwauwa Watanznaia haswa ndugu zetu wa kihaya, leo waziri wa mambo ya nje , kakataa kabisaa kuitambua serikali ya wananchi wa libya waliompindua gadafi! tena kamkemea balozi wa Libya kwa kupandisha bendera ya NTC!

hiki si kitendo cha kizarendo kabisaa! Ukija wizara ya elimu, huko ndiko kunanuka uozo wa mawaziri wasiojali kabisaa kushuka kwa elimu ya vijana wetu. Division VI na O zikizidi 40% lazima waziri wa elimu awajibishwe, lakini hawa mawaziri ndio walaa, . hiki nacho si kitendo cha kizarendo! Jamani nisaidieni na vingine , haswaa huko Sheria walikowachiwa wauza unga kutoka pakistani! Wizara ya mabo ya ndani kuruhusu raia wengi wa kigeni kupata vibali vya kazi za wazawa!

Hii ni hatari kubwa sana , maana tunaonekana kama vile tupo katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, wakati nchi ni ya amani na utulivu. Uganda na Kenya , ndio haooo, wanatuacha kwa kasi ya duma! Jamani ni lini nyie mawaziri mutachukua moyo wa sokoine? Jamani nayo hiyo inataka elimu ya juu kiasi gani?
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
13,391
Likes
2,292
Points
280
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
13,391 2,292 280
Nimesoma nikapita.
 
Mupirocin

Mupirocin

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
1,601
Likes
44
Points
145
Mupirocin

Mupirocin

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
1,601 44 145
Mawazo mazuri, na kuna ukweli ndani yake kikubwa tufanye maamuzi magumu wabongo. Shida yetu tunanidhamu ya woga any way Mungu atuhurumie
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
81
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 81 145
Uzalendo wapi Matumbo Njaa? Mlikubali wapindishe Azimio la Arusha kwa kuzaliwa Azimio la Zanzibar

Sasa Mnataka Mzalendo wa nini?
 
kiroba

kiroba

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Messages
324
Likes
5
Points
35
kiroba

kiroba

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2011
324 5 35
Nimekuelewa mkuu. Lakini ujue huu uzalendo unaousema wewe ni kweli unatakiwa sana katika ustawi wa taifa. Mimi ningependa kuelezea sehemu fulani fulani hivi ili nigusie suala la uzalendo kwa nchi yetu

1.Mwananchi wa kawaida
Huyu anatakiwa awe na uzalendo wa hali ya juu sana kwa kuwa yeye ndio mlengwa mkubwa wa ustawi wa taifa. Utakuta mtu eti anashawishiwa kufanya jambo ambalo lina athari kwa taifa eti kwa kuwa amepewa kitu kidogo. Vile vile ili tupate viongozi wanaeweza tukawaita wazalendo hapa yatubidi tuwe makini sana kwa wale wanaotumia pesa kupata uongozi.

2.Viongozi
Hawa ni watu muhimu sana katika suala zima la uadilifu na uzalendo kwa nchi na raia wake kwa jumla. Hapa ndipo panapokuwa kama kioo vile kwa kuwa kama hawa viongozi hawataonyesha matendo mazuri basi hata uzalendo hawatakuwa nao. Hii inapelekea taifa kama taifa kukosa imani na viongozi hawa na pia uzalendo utaanza kutoweka kidogo kidogo.

3.Usalama wa taifa
Hapa ndipo panapokuwa na umuhimu wake kwa taifa. Hawa wanatakiwa watende kazi zao kwa moyo wa uzalendo wa hali ya juu bila kujali maslahi ya chama gani wanachoshabikia. Hapa pamepoteza sana sifa kwa vile kwa sasa hii idara imeegemea sana upande mmoja wa chama tawala. Imekewa kama vile ni waajiriwa wa chama tawala. Wako radhi wauvue uzalendo kwa nchi yao ili wakitetee chama chao. Kiufupi hapa pana dosari sana bila kuchukua hatua madhubuti tutatumbukia shimoni.
 
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Messages
5,536
Likes
994
Points
280
Nyalotsi

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2011
5,536 994 280
tatizo walivyopewa madaraka walitegemea kuvuna,wakasahau kwamba hawakupanda. Wamefika hawajakuta mazao sasa wanauza hata majembe,mbegu,powatila,mashamba mwakani watatuuza na cc
 

Forum statistics

Threads 1,237,463
Members 475,533
Posts 29,289,419