Baraza la madiwani Arusha lashindwa kukaa tena

MALUMBANO ya kisiasa bado yanaendelea kulitesa Jiji la Arusha, kwa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kukwama kupitisha bajeti ya Jiji hilo kwa Mwaka wa Fedha 2011/12. Hali hiyo ilitokea Ijumaa baada ya madiwani 11 wa Chadema kukataa kusaini kitabu cha mahudhurio ya kikao hicho kilichatarajiwa kupitisha bajeti hiyo, licha ya wajumbe wawili wa TLP kusaini kitabu cha mahudhurio.

Akizungumzia hali hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomih Chang'a, alisema wajumbe 14 wa CCM walisaini kitabu hicho. Hata hivyo, Chang'a alifafanua kwamba kutokana na kushindwa kufikiwa kwa idadi ya theluthi mbili ya wajumbe, kikao hicho kililazimika kuvunjika. Chang'a alielezea masikitiko yake kuhusu hatua ya wajumbe wa Chadema kukwamisha maendeleo ya wananchi kwa maslahi yao kisiasa, badala ya kujali zaidi maslahi ya wananchi.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema Jiji linasubiri mwongozo wa waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika, wa namna ya kuendesha halmashauri katika hali hiyo yenye mvutano wa kisiasa. Alisema Jiji la Arusha lina wajumbe wapatao 32 hivyo akidi inayotakiwa ili kikao hicho kifanyike wajumbe 21, hata hivyo katika kikao cha jana wajumbe 16 tu ndio waliojisajili.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema pamoja na madiwani hao kugoma kupitisha bajeti hiyo, mchakato wake ulishaanza katika ngazi ya kata na kupitishwa na kamati za maendeleo za kata (WDC) kwa mujibu wa sheria ya fedha ya serikali za mitaa namba 9 ya mwaka 1982 kifungu namba 43(1).

Kifungu kicho kinaitaka kila halmashauri kuhakikisha inapitisha bajeti yake miezi miwili kabla ya mwaka mpya wa fedha kuanza, kwa ajili ya mwaka wa fedha unaofuata. Alisema katika Jiji la Arusha, mchakato wa bajeti hiyo ulifuata taratibu zote kuanzia ngazi ya kata na pia kujadiliwa na kamati za huduma kwenye halmashauri.

Bajeti hiyo ilikwishajadiliwa na kamati ya uchumi ya halmashauri, kamati ya mipango miji na mazingira na kamati kuu yaani ya fedha ambayo juzi ilipitisha bajeti hiyo. Kwa mujibu wa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, George Kitunga, kwa mwaka 2011/12 zinatarajiwa kutumika zaidi ya Sh bilioni 48.14 kati ya fedha hizi Sh bilioni 5.65 zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya Jiji hilo.

Aidha, Kitunga alieleza kwamba Sh bilioni 24.98 ni ruzuku kutoka Serikali Kuu, Sh bilioni 17.4 kutoka mashirika ya maendeleo na mchango wa wananchi ni Sh milioni 96. Kuhusu matumizi ya Jiji hilo kwa mwaka 2011/12, Sh bilioni 17.78, sawa na asilimia 37 ni kwa ajili ya mishahara, Sh bilioni 5.74, sawa na asilimia 12 matumizi ya kawaida. Mweka Hazina huyo alifafanua kwamba Sh bilioni 24.6 sawa na asilimia 51 zitatumika kwa maendeleo ya wananchi kupitia miradi mikubwa ya elimu na barabara, zitakazojengwa kwa kiwango cha lami.

Mgogoro wa kisiasa Arusha ulianzia wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2010 na baadaye kuhamishia katika uchaguzi wa meya wa Jiji ambao baadaye ulisababisha mauaji ya watu watatu wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na Chadema kupinga Gaudence Lyimo wa CCM kuwa Meya, licha ya kushinda katika uchaguzi uliosusiwa na wajumbe wa chama hicho cha upinzani.

Habarileo
 
MALUMBANO ya kisiasa bado yanaendelea kulitesa Jiji la Arusha, kwa kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kukwama kupitisha bajeti ya Jiji hilo kwa Mwaka wa Fedha 2011/12.

Hali hiyo ilitokea Ijumaa baada ya madiwani 11 wa Chadema kukataa kusaini kitabu cha mahudhurio ya kikao hicho kilichatarajiwa kupitisha bajeti hiyo, licha ya wajumbe wawili wa TLP kusaini kitabu cha mahudhurio. Akizungumzia hali hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Estomih Chang'a, alisema wajumbe 14 wa CCM walisaini kitabu hicho.

Hata hivyo, Chang'a alifafanua kwamba kutokana na kushindwa kufikiwa kwa idadi ya theluthi mbili ya wajumbe, kikao hicho kililazimika kuvunjika. Chang'a alielezea masikitiko yake kuhusu hatua ya wajumbe wa Chadema kukwamisha maendeleo ya wananchi kwa maslahi yao kisiasa, badala ya kujali zaidi maslahi ya wananchi.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema Jiji linasubiri mwongozo wa waziri mwenye dhamana na serikali za mitaa (TAMISEMI), George Mkuchika, wa namna ya kuendesha halmashauri katika hali hiyo yenye mvutano wa kisiasa. Alisema Jiji la Arusha lina wajumbe wapatao 32 hivyo akidi inayotakiwa ili kikao hicho kifanyike wajumbe 21, hata hivyo katika kikao cha jana wajumbe 16 tu ndio waliojisajili. Kaimu Mkurugenzi huyo alisema pamoja na madiwani hao kugoma kupitisha bajeti hiyo, mchakato wake ulishaanza katika ngazi ya kata na kupitishwa na kamati za maendeleo za kata (WDC) kwa mujibu wa sheria ya fedha ya serikali za mitaa namba 9 ya mwaka 1982 kifungu namba 43(1). Kifungu kicho kinaitaka kila halmashauri kuhakikisha inapitisha bajeti yake miezi miwili kabla ya mwaka mpya wa fedha kuanza, kwa ajili ya mwaka wa fedha unaofuata.

Alisema katika Jiji la Arusha, mchakato wa bajeti hiyo ulifuata taratibu zote kuanzia ngazi ya kata na pia kujadiliwa na kamati za huduma kwenye halmashauri. Bajeti hiyo ilikwishajadiliwa na kamati ya uchumi ya halmashauri, kamati ya mipango miji na mazingira na kamati kuu yaani ya fedha ambayo juzi ilipitisha bajeti hiyo.

Kwa mujibu wa Mweka Hazina wa Jiji la Arusha, George Kitunga, kwa mwaka 2011/12 zinatarajiwa kutumika zaidi ya Sh bilioni 48.14 kati ya fedha hizi Sh bilioni 5.65 zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya Jiji hilo. Aidha, Kitunga alieleza kwamba Sh bilioni 24.98 ni ruzuku kutoka Serikali Kuu, Sh bilioni 17.4 kutoka mashirika ya maendeleo na mchango wa wananchi ni Sh milioni 96. Kuhusu matumizi ya Jiji hilo kwa mwaka 2011/12, Sh bilioni 17.78, sawa na asilimia 37 ni kwa ajili ya mishahara, Sh bilioni 5.74, sawa na asilimia 12 matumizi ya kawaida. Mweka Hazina huyo alifafanua kwamba Sh bilioni 24.6 sawa na asilimia 51 zitatumika kwa maendeleo ya wananchi kupitia miradi mikubwa ya elimu na barabara, zitakazojengwa kwa kiwango cha lami.

Mgogoro wa kisiasa Arusha ulianzia wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2010 na baadaye kuhamishia katika uchaguzi wa meya wa Jiji ambao baadaye ulisababisha mauaji ya watu watatu wakati wa maandamano yaliyoandaliwa na Chadema kupinga Gaudence Lyimo wa CCM kuwa Meya, licha ya kushinda katika uchaguzi uliosusiwa na wajumbe wa chama hicho cha upinzani.

Chanzo: Habari leo
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika kikao cha bunge lililopita alisema serikali iko makini sana, kama ni kweli umakini wao ungeona athari zinazoweza tokea baadaye kama hii ya kukwamisha bajeti.
 
Marekani nao Republicani usiku wa leo bado hawajaikubalia bajeti ya Obama, na sasa usiku wa manane kama hakuna suluhu basi itaweka historia nyingine ya shut down. Kisa republican wanapinga bajeti katika kipengele cha kutoa mimba
 
lol...chadema kama republicans wanavyofanya marekani saivi.. serikali imekaukiwa kisima.
 
Back
Top Bottom