Baraza la Maaskofu wa Pentekoste lakutana ghafla kuhoji kwanini halina mwakilishi Bunge la Katiba

Status
Not open for further replies.
Haya makanisa mengine hayana P O B OX ,kuwa na wajumbe ni kaz halafu hawapatan wao wenyewe kwa wenyewe.
 
wewe angalia ----- hili kundi lina wafuasi kalibia robo ya watanzania wote tanzania,
wana haki ya kupata hata mtu mmoja wa kuwawakilisha.

sasa ni dhahili kikwetu ni mdini .............................. .

hii ni hatari

wadungu ni vyema tukajadili jambo hili kwa uadilifu sana , huwezi kuacha kundi lenye watu wengi ,robo ya watanzania ukaliacha,

habari ya udini ilikuwa walao imeisha, kwa hali hii?, hili ni fukuto jipya

na ni hatari sana, tuwe makini.

haiwezekani watu million kumi wakakosa hata mwakilishi mmoja?.

haiwezekani, haiwezekani...................................................????????????????????????????

hebu malizia

walokole milioni 10

wasabato milioni 10

Yehova milioni 10

Angican milioni 10

walutheli milioni 10

wapagani milioni 10

shia milioni 10

hamadiya milioni 10

Bakwata milioni 10

Answari milioni 10

Katoliki milioni 10

wengine wote milioni 10

watanzania milioni 45
 
Hivi hawa wahuni wametoka wapi wanao taka kuchafua mchakato wa kupatikana katiba?
Hivi kama kila mtu anataka kuwa na muwa kilishi kwenye bunge husika kweli patatosha?

Hivi hawa wapentekoste si wakristo? Mbona wana leta vurugu?
Hivi hawajui kuwa na waislamu nao wapo makundi mengine lakini wamekubali walio chaguliwa wawa wakilishe?

Kwa mpango huu hata makonda, wapiga debe watataka wawe na wawakilishi.

Hawa wana lao jambo si bure.
Wahuni wakubwa hawa.
Nasikia kesho Umoja wa Mafundi Mwashi wakiongozwa Yericko Nyerere watatoa tamko nao wanalalamika hawana muwakilishi.
 
Last edited by a moderator:
Na sisi mashahidi wa jehova tutakutana kesho.

Nasikia Wabahai, wahindu, wasabato, zion church na jeshi la wokovu nao wanakutana

Bila kusahau chama cha maseremala, mafundi bomba, umoja wa wakwezi, umoja wa wauza ulanzi nk... mwisho wake kila mtu atataka awemo

Kama hoja ni kusikia tu hata mimi nasikia na wewe kesho unakutana mwenyewe kutoa tamko unataka uwemo
 
shida ni posho ya tsh 70000 nitawawakilisha mimi bila hata posho

Acha utahila,............ shida siyo posho', shida ni tasisi yenye wafuasi millioni kumi
kukosa mwakilishi, hapo kwanza tuelewane,xx

Habali ya posho hiyo ni ziada tu, hata hivyo hizo ni kodi zetu kama nchi hii tuko milion
45 harafu kundi moja tu, lina robo ya wanaotafuta hizo kodi bila shaka wana haki .

ya kuwa na mwakilishi wao
 
Ngoja na mimi niitishe press ya waandishi wa habari, maana familia yetu haina mwakilishi kwenye bunge la katiba!
 
Na mie kabila langu lazima lipate muakilishi la sivyo patachimbika.
 
Umeshawahi kusikia ibada ya krismasi imefanyika kitaifa katika kanisa fulani la Pentekoste. Au ibada ya pasaka itafanyika kitaifa katika kanisa fulani la pentekoste. Jibu ni hapana, mara zote hufanyika kwenye makanisa ya CCT (Anglikana na KKKT) au TEC (Catholic) Mahali zinapofanyika sherehe hizi, vyombo vya habari vya kitaifa hurusha hewani ibada husika.

Lakini umeshawahi kuona hiyo TBC (ambayo inayoendeshwa kwa kodi za watu wa dini zote wakiwemo wapentekoste na wale wasio na dini) ikionyesha kipindi cha jumapili ibadani kutoka katika kanisa la kipentekoste? jibu ni hapana.

Swali la kujiuliza: Kwanini wapenteKotse wanadharauliwa na serikali ya CCM?

Hapa kuna nadharia kama tatu ambazo maklala hii itazijadili: Nadharia ya kwanza ni uchache mtu ataweza kujipa ujasiri feki na kuseam "hawadharauliwi ila ni wachache sana, yaani wapo kiduchu kama wafuasi wa ile dini ya marastafarian" au ile dini ya Bhai, au hadhi na idadi yao ni sawa tu na kundi la Bongo movies ambao idadi yao haijai kwenye kiganja cha mkono"

Hata hivyo hoja hiyo hapo juu ni hoja dhaifu kwani makanisa yaliyochini ya PCT(Pentecostal Coiuncil of Tanzania) yapo 10,000 nchi nzima na wanachama 10,000,000 TZ.

Nadharia nyingine ya Wapentekoste kutengwa tunaweza kusema labda ni ile tabia yao ya kutokunywa pombe na kuhubiri na kushawishi mno watu waache pombe na hatimaye wanasababisha serikali ya CCM kukosa mapato yatokanayo na kodi ya vileo. Nadharia hii inaweza kuwa na ka- ukweli fulani ingawa si ya msingi sana.

Nadhari nyingine inaweza kuwa mtazamo wa serikali kuwa Wapentekoste ni watu wapole, wanafuata misingi ya kibiblia bila uchakachuaji wowote, hivyo hata wakipunjwa au kuonewa hawana noma yaani kwa lugha ya kibiblia " akupigaye shavu la kulia mgeuzie na la kushoto amalize hamu ya kukupiga" serikali ya CCM inawatambua kuwa ni washamba na ni mamburura tu wasio na madhara yoyote. Hii inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya CCM kutowajali na kuwapuuza Wapentyekoste.

Kilele cha yote ni uteuzi wa Rais katika Bunge la katiba, amewadharau.

WITO: HIMAHIMA WAPENTEKOSTE TUUNGANE TULIANGUSHE HILI ZIMWI LINALOITWA CCM MWAKA 2015, KURA 10,000,000 ZINATOSHA KUCHAGUA RAIS ASIYE NA UBAGUZI.

GREAT THINKER TU WANARUHUSIWA KUJADILI
Tujikumbushe Uteuzi - TAASISI ZA DINI
1.Waislamu-kuna wajumbe-10
2.TEC kuna wajumbe-4
3.CCT kuna wajumbe-5
4.Maaskofu binafsi-2
5.PCT- Hakuna mjumbe hata mmoja.
 
Umeshawahi kusikia ibada ya krismasi imefanyika kitaifa katika kanisa fulani la Pentekoste. Au ibada ya pasaka itafanyika kitaifa katika kanisa fulani la pentekoste. Jibu ni hapana, mara zote hufanyika kwenye makanisa ya CCT (Anglikana na KKKT) au TEC (Catholic) Mahali zinapofanyika sherehe hizi, vyombo vya habari vya kitaifa hurusha hewani ibada husika.

Lakini umeshawahi kuona hiyo TBC (ambayo inayoendeshwa kwa kodi za watu wa dini zote wakiwemo wapentekoste na wale wasio na dini) ikionyesha kipindi cha jumapili ibadani kutoka katika kanisa la kipentekoste? jibu ni hapana.

Swali la kujiuliza: Kwanini wapenteKotse wanadharauliwa na serikali ya CCM?

Hapa kuna nadharia kama tatu ambazo makala hii itazijadili: Nadharia ya kwanza inaweza kujengwa kwenye uchache. Mtu ataweza kujipa ujasiri feki na kusema "hawadharauliwi ila ni wachache sana, yaani wapo kiduchu kama wafuasi wa ile dini ya marastafarian" au ile dini ya Bhai, au hadhi na idadi yao ni sawa tu na kundi la Bongo movies ambao idadi yao haijai kwenye kiganja cha mkono"

Back
Top Bottom