Baraza jipya la Mawaziri: Tanzania Mpya tuliyoitegemea imeanza kuyeyuka..!

Baada ya jana Rais John Pombe Magufuli kutangaza Baraza lake la Mawaziri, mapya yameibuka ndani ya CCM. Makada waandamizi wa CCM, waliozungumza nami na kuomba kutotajwa popote, wameniambia kuwa wameshtushwa na Baraza la Magufuli na kuguswa kwa namna hasi yenye kasi na ukakasi.

Wamesema kuwa Rais Magufuli, kulingana na uteuzi wa jana, amekianika chama kama kilichoishiwa watu waadilifu na wachapakazi. Hii inafuatia hatua ya Rais Magufuli kuacha nafasi za Mawaziri wanne wazi akidai kuwa bado anatafuta wa kushika nafasi hizo. Makada hao maarufu na waandamizi Dar es Salaam na Dodoma, wamenidokeza kuwa nafasi wazi ni aibu kwa chama.

'Rais anasema kuwa anatafuta wa kuwa Mawaziri wa Fedha,Uchukuzi, Elimu na Maliasili, anawatafuta kutoka wapi zaidi ya ndani ya chama? Kwani ndani ya CCM wamekwisha? Huu ni udhalilishaji kwa chama na unapaswa kukemewa na uongozi' alisema kada mmojawapo ambaye ameukosa Urais na hata Uwaziri.

'Chama kina hazina ya viongozi. Kwanini nafasi zibaki wazi?' alihoji mwenyeji huyo wa jiji. Hatua ya Rais Magufuli kuacha wazi nafasi za mawaziri wanne na kusema kuwa bado anawatafuta ndiyo hasa inayowakereketa makada na viongozi waandamizi chamani ingawa hakuna aliyejitokeza na kusema hadharani. Walalamikaji wote ni CCM maslahi.

Lakini, hali si shwari chamani. Inahojiwa: kweli CCM imeishiwa wa kushika Uwaziri wa Fedha, Uchukuzi, Elimu na Maliasili? Siasa siasani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mtoa mada na hao wanaolalamika ni mapandikizi ya Lowassa.
Na mtaanikwa mwaka huu!
 
et wamekuomba usiwataje...who ar u!
 
Rais Magufuli hatafuti makada wa chama. Anatafuta mawaziri watakaofanya kazi kwa manufaa ya Watanzania wite. Rais wetu si mkurupukaji na hataki kufanya makosa ya kiuteuzi
 
Hata hao aliyo wachaguwa bado wanapwaya ccm wameishiwa kweli
 
Labda bado anaomba ridhaa kwa kina Mangula ili awaweke kika Zitto na Lipumba
 
umesema kada mmoja aliogombea urais na hakupata hilo ndilo kawaida ya sisi waafrika akikosa lazima amchimbe aliopata kama wamavyofanya chadema hivi sasa kuandika uzushiuzushi
 
Ule usemi wa Nape kuwa ccm ina hazina ya viongozi umedhihirika kuwa ni uongo mtupu.
 
n
NIKWELI CCM INAHAZINA YA VIONGOZI LAKINI WENGI SI WASAFI.WALIOWENGI NI VIONGOZI MASLAHI NDO SHIDA INAPOANZIA.
 
Kweli hii ni aibu kwa chama maana wabunge wote walioshinda pamoja na wa viti maalum bado Magufuli anateua watu wawe wabunge kisha kuwa mawaziri!?
 
Ule usemi wa Nape kuwa ccm ina hazina ya viongozi umedhihirika kuwa ni uongo mtupu.
Hivi wewe hukuona jinsi Chadema walivyokopa toka kwenye hiyo hazina? Ngoja basi nikukumbushe kidogo: Lowassa, Kingunge, Sumaye, Msindai, Mgeja, Masha n.k. Upo hapo?
 
Rais Magufuli hatafuti makada wa chama. Anatafuta mawaziri watakaofanya kazi kwa manufaa ya Watanzania wite. Rais wetu si mkurupukaji na hataki kufanya makosa ya kiuteuzi

Umejibu vyema mkuu, kula like mia.
 
Hamna jipya hii ni serikali ya awamu ya tano ni mabadiliko kwenda mbele sasa unashangaa nini, hii ni mbinu ya kuvuruga ccm jamani wanaccm tuwe macho mwacheni Magufuri afanye kazi wananchi wanataka mabadiliko ya kweli tukifanya mchezo wa kuadanganya wananchi basi tuseme baibai ccm2020
 
Rais Magufuli hatafuti makada wa chama. Anatafuta mawaziri watakaofanya kazi kwa manufaa ya Watanzania wite. Rais wetu si mkurupukaji na hataki kufanya makosa ya kiuteuzi

we ni mpuuzi sana iv makada si akna nape january mwigulu na kairuki unataka tena makada akna nan zaid ya hao magufuli ovyo tu
 
Back
Top Bottom