Baraza jipya la Mawaziri: Tanzania Mpya tuliyoitegemea imeanza kuyeyuka..!

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Ndugu zangu kama sio unafiki ni madharau yaleyale yanaendelezwa mbele ya macho ya watanzania tukiwa tunaona.

Nilianza kuwa na imani na Rais kwamba kwa kuwa ameanza kuonyesha mfano mzuri kwa utendaji kwa mwezi huu mmoja basi atatuletea watu wenye mwenendo mzuri na background yao ni safi.

Kitendo cha kutuletea Mwigulu aliyekuwa naibu waziri wa Fedha ili awe waziri kamili huku akiwa na makashfa kibao ya wizara yao kushindwa kukusanya kodi ni madharau.

Mwakyembe aliyeweka wezi waliofukuzwa siku chache zilizopita kule bandarini na kila siku tunasoma kwenye magazeti jinsi alivyotuletea mabehewa feki leo anarudishwa eti ni msafi anaweza kazi, hayo ni madharau kwa watanzania.

Huyu Makamba naye hana sifa yoyote ya kuwa Waziri ndani ya nchi yetu kwa uwezo wake mdogo na kashfa kibao za majungu na kupepeta maneno hatutaki mtu kama huyu.

Huyu Muhongo aliyerudishwa Nishati si ndiye yuleyule aliyefukuzwa serikali iliyopita kwa kushindwa kazi? Leo hii anarudishwa tena mkifikiri tumesahau hasara aliyotuingizia?

Nilianza kuwa na imani kwa mbaali na huyu Rais japo yupo CCM nilianza kidogo kumuamini lakini sio kuamini chama chake.

Nilikuwa nasubiri nione ni watu gani ataleta ili wawe wasaidizi wake sasa basi kama ndio hao imani yangu imekufa moja kwa moja na huniambii tena kitu mara hii, tusubiri tuone.

Watanzania wenye uwezo na wasomi mbona wapo wengi, mpaka Nape unampa Uwaziri? Kweli upo serious au unatutania?

Sitaki tena kumuamini huyu Rais.

[SUB]Ndugu wana JAMII,

Naandika post hiii kwa masikitiko makubwa kuhusu serikali mpya ya Rais wetu MAGUFULI. Wengi wamekuja na hoja tofauti tofauti hasa kuhusu lipi tunaweza kutegemea kwenye serikali ya Magufuli, lakini pengine kila mmoja wetu anaweza kuwa na mawazo tofauti na vile tunavyoona mambo kwa jicho la tatu.

Binafsi, kuhusu baraza jipya la Magufuli. Haiwezekani kuwa Rais Magufuli alichukua muda mrefu kuchagua watu kama hawa ambao wanajulikana kwa majina, tabia, utendaji na hulka katika majukumu yao ya muda mrefu ndani ya serikali zilizopita. Binafsi naona kuwa Rais alikuwa na njia mbadala na watu mbadala tofauti na hawa waliotajwa na siku kadhaa zilizopita kikao cha wanaccm walikaa chini; kile kilichoongelewa nadhani Rais Magufuli ndio anajua na serikali yake.

Watanzania wenzangu, mimi bado nina Imani sana na Rais Magufuli na nia yake juu ya hii nchi. Rais Magufuli hawezi kuibadili hii nchi akiwa ndani ya CCM. Hilo lazima lieleweke na lituuingie ndani ya vichwa vyetu. CCM ndio imeshika remote control na anayecontrol haya mambo na ideas za kipuuzi hizi naamini zinatoka kwa JK; Ndio maana JK baaada ya kikao cha chama alitoka na kifua sana, kujionyesha onyesha kuwa bado anashika nchi na ana-influence kubwa sana ndani ya serikali na ndani ya chama. JK ni mtu hatari sana kuliko mnavyodhania.

Nawapa pole sana wale wana mabadiliko na pole wale waliokutwa na panga la Magufuli iwe kwa haki au bahati mbaya. Mabadiliko mtasikia kwenye bomba.

Wachina walishapewa gesi yao na MUHONGO karudishwa kulinda maslahi yake. Muhongo ni nani, kwani hakuna wasomi Tanzania nzima, je na wale walioko nje ya nchi, Je? Hatuwezi kuendelea kuwa wajinga kiasi hichi.

Mungu ibariki Tanzania.


[/SUB]
 
kwa nini hukugombea wewe urais ili uweke watu unaowataka. acha u ashki majinun! sisi hatuna shida na mtu shida yetu ni utekelezaji wa ahadi ambazo rais ametoa. usikurupuke kama umetokea chooni jiheshimu na mheshimu rais aliye chaguo la wengi. kwenda zako kule.
 
Kabla hujaleta hili andiko, ulipaswa kujiuliza wewe kwanza ni jambo gani umeifanyia Tanzania? Huenda wewe ni miongoni mwa majipu yanayosubiri kutumbuliwa au umeshatumbuliwa. Hata wewe kwenye familia au ukoo wako sidhani kama unayofanya na kuyaamua yanapokelewa na wote kwa mtazamo chanya. Watu wa aina yako hawakosi katika jamii na kwa namna yoyote maisha lazima yaendelee.
 
Haitwi Mulungo anaitwa Professor Muhongo!

Kwakuwa unakimbilia kuandika bila utafiti wa kina unafikiri una point. Prof. alijihudhuru na wala hakufukuzwa, kazi aliyofanya kwa kipindi chake kila mtu aliiona.
 
Kuna watu bado hamjui nguvu ya chama?
Magufuli kapewa order tangaza baraza...
na kaambiwa awe makini na kufukuza watu

Walimwita kumfunga speed gavana ya majipu. Ninajiuliza iweje mwenyekiti wa chama hajakabidhi madaraka kwa rais? Ukumbuke wale wawili ni wanajeshi pia.
 
Cant keep on commenting on this post ambayo haina chembe ya uchambuzi......walifanya kazi zao na kuwasilisha panapotakiwa ulitaka wanyeje zaidi ya hapo....
 
Back
Top Bottom