Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,494
- 113,590
Wanabodi,
Kwanza naomba nianze kwa pongezi za uteuzi wa baraza dogo, sina uhakika sana na umakini, lakini Katika kulitafakari baraza hili jipya la mawaziri, nimenote kuna sheria, taratibu na kanuni zinaweza kuwa zimekiukwa katika uteuzi huu!. JMT ni nchi ya Muungano kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, au Tanzania Zanzibar, hivyo baraza la Mawaziri linapaswa kuwa na mawaziri kutoka Zanzibar wakiongozwa na Rais wa Zanzibar ambaye anapaswa kuwa waziri asiye na wizara maalum akiwakilisha maslahi ya Zanzibar ndani ya Baraza, sikusikia kama rais halali wa Zanzibar, akiteuliwa uwaziri!. Hivi katiba inasema juu ya hili?!.
La pili katika wizara zote za muungano, kwa mujibu wa sheria na kanuni, lazima ziongozwe na mawaziri kutoka pande zote za muungano!, yaani waziri akitoka upande mmoja, naibu waziri lazima atoke upande wa pili wa muungano, hili sikufanikiwa kuliona katika wizara zote za muungano, hili limekaaje?!.
Wiza hizo ni
WIZARA
Ofisi ya makamu wa Rais, muungano na mazingira: Waziri ni January Yusuf Makamba, naibu Luhaga Mpina-Hii ni wizara ya Muungano, waziri na naibu wake wote ni kutoka upande mmoja!.
Ujenzi, uchukuzi na mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri mhandisi Edwin Ngonyani. Ujenzi ni ya bara tuu, Uchukuzi na Mawasiliano zina mwelekeo wa ki muungano kupitia TCRA, TAA na POSTA hivyo hapa amnasubiriwa Mzenj?!.
Fedha na mipango: Waziri bado tunamtafuta, naibu waziri ni Ashantu Kizachi, kama huyu sii Mzanzibari, then Waziri anapaswa awe Mzanzibari.
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa: Waziri ni Augustine Philip Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.- Hii ni wizara ya muungano, waziri na naibu wote ni kutoka bara!.
Ulinzi na kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Ali Mwinyi-Hii ni wizaa ya muungano, kushikwa na Mzanzibari ni haki yake!.
Mambo ya ndani: Charles Muhangwa Kitwanga-Hii ni wizara ya muungano, iliyakiwa ikishikwa na Mbara, lazima iwe na naibu kutoka up
Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya-Hapa pia Waziri anatakiwa kutoka Zanzibar kwa ajili ya Elimu ya Juu ambayo ni ya muungano!.
Japo Magufuli ana lengo zuri la kubana matumizi, jee ubanaji huo, ni lazima uzingatie sheria,taratibu na kanuni?!, au kwa vile lengo ni kubana tuu, tumwache abane namna yoyote ile atakayoona vile inafaa?!. Swali ni Baraza Jipya la Mawaziri: Huu Uundwaji wa Baraza Dogo, Jee Rais Magufuli Hajakiuka Sheria, Taratibu na Kanuni?!, au kwa vile jamaa ni mbabe fulani, hakuna yoyote wa kumwambia kitu?!, hata sisi jf pia tumuogope?!, au tumuheshimu ila ukweli tumuambie?!.
NB. Mtanote sijaitaja kifungu chochote cha sheria yoyote, taratibu yoyote au kanuni yoyote, kwa sababu sio kila sheria lazima iandikwe, zipo taratibu nyingine ni kama sheria, ukikiuka unakuwa kama umevunja sheria na sio mpaka ziandikwe!. Uingereza ina katiba yake lakini haijaandikwa popote!.
Tangu tumepata uhuru wetu, marais wa Tanzania wamekuwa wakipokezana kati ya Mkristu na Muislamu, Alianza Julius, akafuatia Ali, akafuatia Benyamini, akafuatia Mrisho na sasa ni Yohana!, haijaandikwa popote lakini huu ndio utaratibu wetu, tena akiwa Mkiristu, ni lazima awe kutoka...mkubali mkatae huo ndio uhalisia wa mambo bila kuandikwa popote, bali hupangwa iwe hivyo by a premeditated moves japo wengine huona kama just a coincidence!, hivyo sitarajii kama bado kuna watu wataniuliza sheria gani, taatibu gani na kanuni gani?!.
Pasco