Nimeangalia maelezo ya Meneja wa TANROAD mkoa -DSM ndugu Haruon Senkuku alipohojiwa na muandishi wa habari kuhusu malalamiko ya wakazi wa maeneo ya Mbezi-Msumi wanaolalamia TANROAD kutokuijenga barabara na wakihoji kuhusu mkandarasi anayejenga kakipande kasikofika hata km 1 ambapo anaifanya kazi hiyo karibia mwaka wa pili sasa ikiwa ni pamoja na kujenga kwa kiwango duni cha lami na wembamba wa barabara.
Kilichonishangaza ni pale huyo Meneja wa TANROAD kwenye kujibu hoja amesema hiyo barabara itakuwa inajengwa kwa km 1 kila mwaka. Nikajiuliza hivi kumbe kujenga barabara ya ukubwa wa km 1 inachukuwa miezi 12+, au labda anamaana itakuwa inatengewa fedha za kujenga urefu huo. Kwa maana hiyo basi kukamilika kwa barabara kutoka mbezi kwenda Msumi wakazi wa maeneo hayo wategemee miaka 8 kwa maana ya km 1 kwa mwaka x km 8(Msumi-mbezi).
Kuna haja mambo mengine Mama yetu mhe Rais ni vema akayajua maana hawa watendaji katika taasisi na wizara SIO KABISA