Barack Obama: Mfumo dume kumuathiri Clinton

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,634
30,000
Obama alisema hayo mapema jana Jumapili wakati akiendelea kuwashawishi wamarekani wamchague Bi Clinton awe rais.

Obama alisema kuwa kwa miaka na miaka hawajawahi kuwa na rais mwanamke na hii inatokana na tatizo la kihistoria na la muda mrefu katika jamii ya taifa hilo kuhusu mtazamo kwa wanawake wenye nguvu. Obama alionya kuwa tatizo hilo bado lipo na litaathiri kampeni za Clinton mwaka huu.

Obama anaendelea kuimarisha kampeni za Clinton katika wapiga kura na maeneo ambayo yanaonekana kusita kumuunga mkono Clinton.

Juzi aliwataka watu weusi wajitokeze kwa wingi kumpigia kura Clinton kama kweli wanataka kumuaga vizuri wakati atakapoachia madaraka ya urais na aliwaambia itakuwa ni udhalilishaji katika misingi aliyoiweka yeye ikiwa watu weusi hawatamuunga mkono Bi Clinton.

Michelle Obama nae anatumia ushawishi wake mkubwa na kupendwa kwake na Wamarekani kuendelea kumpigia kampeni Hillary Clinton na anaendelea kuwahamasisha watu weusi wajiandikishe kwa wingi zaidi.
 
Unafiki wa wanasiasa!

Huo mfumo dume anauona sasa hivi tu na 2008 hakuuona?

Na kwanini anawapembejea weusi kumpigia HC? Hapandikizi mfumo mwingine wa ubaguzi? Yeye in mweusi lakini ni rais wa wamarekani wore. Kama ulivyouliza, anaweza vipi kuuelezea umma kwamba mfumo dume anaoukosoa haukuwepo 2008?

Zanzibar Baby:):):):)
 
Trump akienda kwa Wazungu wenzie na kuwahimiza wajitokeze kwa wingi kumpigia kura unadhani ataonekanaje?

Yaani siasa bana...full unafiki tu.

Huyo huyo Obama na team yake mwaka 2008 waliwaita Bill na Hillary kuwa ni wabaguzi wa rangi....

Leo hii eti ndo anampigia debe ili awe mrithi wake.
 
Kuna rafiki yangu mtaalam wa haya mambo ya siasa aliwahi kuniambia "Politics is worse than prostitution"
 
Back
Top Bottom