Barack Obama: Mfumo dume kumuathiri Clinton

Trump akienda kwa Wazungu wenzie na kuwahimiza wajitokeze kwa wingi kumpigia kura unadhani ataonekanaje?

Yaani siasa bana...full unafiki tu.

Huyo huyo Obama na team yake mwaka 2008 waliwaita Bill na Hillary kuwa ni wabaguzi wa rangi....

Leo hii eti ndo anampigia debe ili awe mrithi wake.
Ninadhani hii ni moja ya masuala muhimu nimewahi kuona hapa JF na pengine litapita tu hivihivi. Tunapohalalisha ubaguzi wa weusi dhidi ya weupe tutarajie vivyohivyo kutoka kwa weupe. Vinginevyo tunaonekana kama watoto katika suala zima la ubaguzi wa rangi. Unaweza kufika mbali zaidi na kusema ubaguzi wa weusi dhidi ya weupe 'unakubalika' kwa sababu bado tupo kwenye malezi, tunavumiliwa, kama watoto (patronized).

Mada hii imenikumbusha nchi nyingi za Kiafrika na suala la Uhuru. Wakoloni walisema hatujawa tayari kujitawala, bado walihitaji 'kutuandaa' kwa akili kujitawala. Ubaguzi wa rangi. Mara baada ya Uhuru mashujaa wa ukombozi wakasema hawawezi kuachia madaraka kwani wananchi wao hawakuwa tayari! Nkrumah akajitangaza Raisi-wa-Maisha. Banda. Sekou Toure. Wengine hawakujitangaza hadharani ila walikaa miongo kadhaa kwa sababu kuondoka kwao nchi zingeyumba. Mfano mzuri kuhusu hili mara nyingi ni pale wanaponukuu: Mwalimu alituambia tusichimbe madini, hayaozi. Watu wake bado hawajawa tayari. Pengine alikuwa sahihi na kama hivi ndivyo, Wakoloni walikuwa sahihi.

Haikuwa dhamira yangu kuchanganya mada. Imenibidi kutokana na suala (point) muhimu sana, upande wangu, kuhusiana na hili la ubaguzi wakati huohuo tunasahau kwamba sisi wenyewe wabaguzi kupindukia mpaka imefikia hatua tunaona jambo la kawaida tu. Hata Rais 'wetu', Mweusi mwenzetu wa Marekani anaona shwari tu. Ni ubaguzi huu ndiyo unaopelekea ubaguzi upande wa pili kwani hata huko wale waliokuwa na hulka za kibaguzi wanajiuliza swali hili. Obama hakuchaguliwa na kura za weusi tu. Nyingi, kwa mara kadhaa wa kadhaa, zilikuwa kura za hao weupe tunaowabagua.

Labda hata vurugu zinazoendelea Marekani kuhusiana na suala zima la rangi ya ngozi linatokana na kukubali kuwa waathirika (victims) na hivyo kutarajia malezi kutokea kwa jamii (State)? Bila shaka, jeshi la Polisi na mfumo mzima wa utawala US ulitumika kuwanyanyasa weusi lakini hata yalipokuja mabadiliko ndani ya jamii baadhi ya weusi wanataraji malezi. Hii haimaanishi hakuna ubaguzi ndani ya mifumo, ubaguzi upo, lakini kuna ubaguzi nje ya mfumo pia.
 
Ni vema umeeleza kiundani
 
Back
Top Bottom