Barabara za Dar ni Machinjio Usiku

Barabara za Dar ni Machinjio Usiku

Nyingi za ajari hizo husababishwa na shetani pombe.
Wee!,wee!,weee!;Acha kabisa kuyasingizia Maji matamu kabisa ya Ilala!, ajali haina kinga,na nyingine ni uzembe na kutokuwa makini barabarani.
 
Ajali nyingi zinatokana na sababu hizi

Ulevi

Usingizi

Kuwahi papuc.i, ( kifupi haraka )

Vimbwanga vya usiku

Kutumia simu wakati unaendesha, unakuta mtu yuko speed 100 na ki vitz yuko busy anatuma msg

Chura....gari zinaingia sana mitaroni
 
Niliwahi kukutana na jamaa mmoja yupo kwenye kamati ya usalama barabarani, akaniambi ukiona statistics za ajali zinazotokea kwenye junction zenye taa kwa mwezi unaweza usitembee usiku. Yale 'mawe' ya barabara ya Mwenge mpaka makumbusho yalikuwa yanachukua uhai wa watu sio chini ya ishirini kwa mwezi maana wengine hawa report.......Achana na junction ya Tazara, Tabata na Mwenge.
 
Huu Uzi safi sana ila maisha ya Dar na purukushani zake hizi lazima ajali ziwe nyingi maana usingizi sio Wa kutosha MTU kalala SAA sita kaamka SAA kumi yaani bado wengi wanalala kwenye magari .

Ukichanganya na stress nuingine za maisha Kuna haja ya kuwa na traffic officers 24/7
 
Vijana wa DSM wanaotumia vyombo vya moto ni watumiaji wa HOVYO sana wa barabara nyakati zote tu. Sasa usiku ukichanganya na balimi + hakuna askari ndio mtu anaendesha utafikiri yupo Somalia kusiko na sheria. Tunahitaji elimu na kutii sheria iwe UTAMADUNI. Wengi wanadhani kutii sheria ni kwa ajili ya kuwaridhisha askari barabarani pekee.
Mhh! Ndugu hapo kwenye balimi kama unanisema mimi! Maana nikizitandika hizo usiku halaf ndo nimechelewa kurudi hm usiku nikiingia na ki corolla changu barabaran utafikiri barabara yote yangu halafu maroli mwee!
 
Ukiwa kama mwanadsm na Mtanzania unayependa maslahi ya nchi yako unashauri nini kifanyike kutatua tatizo hili?
Dah....mie ningependekeza magari yote binafsi iwe mwisho kuingia barabarani saa 11 jioni [emoji41]
 
Back
Top Bottom