Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 507
- 487
Wakati mataifa mengi duniani yanapigana kujenga uchumi kupitia miundombinu ya kisasa ni muhimu kwa sisi Watanzania kutambua kuwa uwekezaji katika barabara si anasa wala matumizi ya kawaida ya serikali bali ni msingi wa maendeleo ya taifa lolote lenye maono ya mbele.
Hakuna nchi iliyoendelea kwa maneno matupu siasa za migogoro wala propaganda za kupinga kila jambo kama wafanyavyo chadema.
Mataifa makubwa duniani yalijengwa kwanza kwa kuunganisha watu wake kupitia barabara reli bandari na huduma za usafiri.
Leo hii China imekuwa nguvu kubwa ya kiuchumi kwa sababu iliwekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu.
United States ilisimama kiuchumi kupitia mtandao mkubwa wa highways uliounganisha majimbo yake.
Hata ndani ya Afrika Rwanda imekuwa mfano wa namna barabara zinavyobadilisha maisha ya wananchi na kuvutia wawekezaji.
Tanzania nayo ipo kwenye njia hiyo ya maendeleo.
Ujenzi wa barabara vijijini na mijini umeanza kuleta matokeo makubwa
Wakulima wanapata masoko kwa urahisi, Watoto wanafika shule salama,
Wagonjwa wanafikishwa hospitali kwa wakati,
Biashara zinakua
Uwekezaji unaongezeka
Ajira zinapatikana
Ni jambo la kushangaza kuona baadhi ya wanasiasa au vyama wakibeza uwekezaji wa miundombinu bila kutoa mbadala wa maendeleo.
Wananchi wanahitaji kuona hoja zinazojenga taifa si siasa zinazokatisha tamaa juhudi za maendeleo.
Kukosoa ni sehemu ya demokrasia lakini ukosoaji wenye tija unatakiwa uje na suluhisho maono na uzalendo.
Taifa haliwezi kuendelea kwa kupinga kila mradi wa maendeleo unaolenga kuwakomboa wananchi kiuchumi.
Barabara nzuri zina maana kubwa sana kwa mama anayesafirisha mazao yake kutoka kijijini kwenda sokoni kwa mwanafunzi anayekwenda shule kipindi cha mvua kwa mfanyabiashara anayesafirisha bidhaa zake na kwa mgonjwa anayehitaji huduma ya haraka hospitalini.
Maendeleo ya kweli huonekana kwenye maisha ya wananchi na moja ya alama zake kubwa ni miundombinu bora.
Tunahitaji siasa za ushindani wa hoja na maendeleo si siasa za kubeza kila hatua ya ujenzi wa taifa.