Barabara Dar kwenda Chalinze kuwa ya kulipia

Barabara Dar kwenda Chalinze kuwa ya kulipia

Hakuna watu ambao wanatawalika bila shida hapa duniani kama wadanganyika!!!
 
View attachment 187854 View attachment 187856

Serikali inafikiria kuipa sekta binafsi barabara Dar kwenda Chalinze kuijenga upya ,kwa mujibu ya muheshimiwa Omari Issa anayehusika na uwezeshaji na utekelezaji ofisi ya rais kama alivyoongea na kituo cha ITV katika kipindi cha dakika 45, alisema sekta iyo binafsi itapewa dhamana ya kukusanya pesa kwa magari yatakoitaji kupita katika barabara iyo ya kisasa itakayojengwa.
hakuna kitu kama hicho, ila sikubishii wewe mkuu, nambishia aliyesema katika hicho kipindi cha dk 45
 
Italipiwa tu ila itaanza rasmi baada ya uchaguzi mkuu 2015
 
Heh! Dont tell me serikali imefikia hatu ya kutulipiza hadi kwenye matumizi ya barabara!! Huu ni wizi wa wazi sasa.....
 
Okay toll gate ni plani nzuri kwani nchi nyingi zinafanya hivyo...eg south africa barabara ziko chini ya makampuni binafsi wanamantain roads and charge for toll gate....zimbabwe the same...na zambia nadhani itaanza mwaka kesho au mwisho wa mwaka huu.
Lakini serikali itatakiwa iweke njia mbadala and wananchi must not be forced to use this quality road..e.g kutoka jhb kwenda boda ya zimbabwe kuna toll gate kama 6 na njia ni nzuri mzee 120 from town mpaka boda..but kuna njia nyingine mbadala ambayo utalipia only 2 toll gates and the road isn't quality na hata distance ni kama 70 km more.
Serikali yetu itatakiwa istop to charge hiyo pesa ya barabara katika petrol na waandae njia mbadala during construction period to avoid traffic...sababu kabla hatujapumzika na hii ya mabasi yaendayo kasi then tunaanza nyingine tena!!
huu ni mtazamo wangu
Hapa kidogo mkuu umenifanya nielewe sasa. As long njia mbadala inakuwepo sawa hata wale watakaoshindwa kumudu watatumia hiyo. Swali; je serikali iko tayari kutengeneza hiyo njia mbadala?
 
Watutengenezee barabara ya bure kwanza ili tupite huko na wao waendelee na ujinga wao...
 
Waliokuwa wanafuatilia enzi hizo jinsi IPTL wangeleta neema kwa 'kuondoa ukiritimba' wa TANESCO hawakujua kabisa kuwa kuna mafisadi wazawa wakiwa wamejivalisha ngozi ya uwekezaji wa kigeni wanakuja kufilisi nchi. Pia kuna issues kama Loliondo ambapo wazalendo wachache wenye upeo kama Stan Katabalo (R.I.P) iligharimu hadi maisha yao ili 'maofisa' wapate kula. Hapo hapo jumulisha na Richmond nk nk nk nk
Leo hii tusisahau pale tunaposikia deni la taifa linagonga trillion 60 huku likiongezeka kwa trillion tatu kila mwezi wadai wakuu ni kampuni za hawa hawa 'maofisa' zingine zikiwa na sura (outwardly) za kampuni za kigeni.
Sasa kwa vile wazungu wamekuwa makini na aina hii ya pesa na maeneo ya ulaji kama TANESCo yamezoeleka ndio wameona hili dili. ...mnajua watasemaje mwishowe: "wanachi hawawezi kilipia hii barabara kila wakati hivo HAZINA italipa kwa niaba yao". Haya yakishatimia ndio mtakumbuka ni kwa nini mchakato wa Katiba Mpya umevamiwa na haohao.
 
Wadau;

....

Sanjari na mradi huo [wa kujenga daraja la juu ya bahari kutoka Coco Beach hadi Aga Khan Hospital, Dar], Dk. Magufuli alibainisha kuendelea kwa mchakato wa kutengeneza barabara ya kulipia kuanzia Dar es Salaam hadi Chalinze, kupitia ubia na Sekta Binafsi (PPP).

"Tulishatangaza zabuni na kampuni 19 zilijitokeza kuwekeza katika mradi huo na baada ya mchujo tumepata kampuni 12 ila kukawa na tatizo la kupata mtaalamu mshauri.

"Sasa ameshapatikana na tutasaini mkataba hivi karibuni ...". Alisema barabara ya sasa itabakia lakini hiyo mpya itakuwa ya KULIPIA.

Kwa hisani ya Mwananchi, Nov. 19, 2014.


Wadau; hii kitu imekaaje? Wajameni, miundombinu ya barabara sio jukumu la msingi la Serikali? Haya mambo ya PPP hadi kwenye mabarabara yamekaaje? "Wenzetu" wanafanyaje?
 
soon waziri wa afya atatangaza kuwepo kwa hewa ya bure na ya kulipia, hii ya kulipia itakuwa itakuwa imechunjwa vijidudu vya tb na mafua ya ndege.
 
Isiguse ardhi tuliyopewa bure na Mungu, ipite angani na magari yapandishwe kwa winchi. Wanataka kutupeleka ambako hatujastahili hata kupafikiria kufika.

Ulaya ulaya, porini porini basi.
 
Duu.... wale wazeee wa kuazima mikoko ndio kusema watakuwa na tozo la ziada....
hakika itajulikana tu nanini nani..
 
Mi nataka lile daraja la feri kigamboni kwanzaaa!! Litakamilikaa liniii?????
 
Namshangaa magufuli...Mbona hata sasa tunalipia barabara...au wanataka kutulipisha zaidi?

Kwanza kuna ROAD LICENCE...Kulipia barabara

Pia unaponunua mafuta kuna charge ya barabara
 
Hii kuruhusu sekta binafsi kujenga barabara au reli halafu wananchi wanalipia ni serikali kukwepa wajibu wake.
 
Back
Top Bottom