Barabara Dar kwenda Chalinze kuwa ya kulipia

Barabara Dar kwenda Chalinze kuwa ya kulipia

huyu mtu ni nyoka , sintomsahau kwa jinsi alivyochangia kwa kiasi kikubwa sana kutaka kuiua TTCL, ameingiaje IKULU......?
View attachment 187854 View attachment 187856

Serikali inafikiria kuipa sekta binafsi barabara Dar kwenda Chalinze kuijenga upya ,kwa mujibu ya muheshimiwa Omari Issa anayehusika na uwezeshaji na utekelezaji ofisi ya rais kama alivyoongea na kituo cha ITV katika kipindi cha dakika 45, alisema sekta iyo binafsi itapewa dhamana ya kukusanya pesa kwa magari yatakoitaji kupita katika barabara iyo ya kisasa itakayojengwa.
 
Huu upuuzi kabisa hamuwezi kutengeneza barabara mpaka mjibinafsishe nyie na familia zenu
road toll niliyozoea mimi kulipa
ni ile ninayoenda kwenye nchi za nje ya tanzania ambayo kila nchi ipo.
sasa hapa ni dhahiri nchi ipo sokoni na hapa mteja kaulizia
hili dili la kulipia road litakubalika au vp
Nchi kama tanzania bado hatujafikia viwango vya kuwa na barabara za kulipia huu ni ujuha tunataka kuletewa
barabara zenyewe tunajengewa chini ya kiwango kazi kulaumu malori yanabeba mizigo mizito
mzigo mzito nijuavyo mimi ni kuanzia tani 40 sisi kiwango
cha mwisho ni tani 32
iweje barabara zife kabla ya muda uliokadiriwa?!
hapa mnatupiga changa kweli kweli
nasikitika sana jinsi mnavyokula hela zetu kwa mgao wa 20% kwenye tenda za barabara
Ila kuna siku mtakuja kututambua
kuburuzwa hatutaki na mtueleze pesa zetu zilipo na mali zenu mmezipata wapi?
 
Kama nnchi imewashinda mseme tu ili wananchi tujue moja, manake ninavyoona mwisho wasiku mtataka tulipie na hewa tunayovuta.

Wildfish! duniani kote ukitia gari yako kwenye highway lazima ulipie road toll! ulaya ni hivyo, US ni hivyo na hata south africa wanalipia! tuache u local wa kupenda kila kitu dezo.
 
wildfish! duniani kote ukitia gari yako kwenye highway lazima ulipie road toll! ulaya ni hivyo, us ni hivyo na hata south africa wanalipia! Tuache u local wa kupenda kila kitu dezo.

sio kweli sio dunia nzima na sio kila highway ni lazima ulipie.....mfano uk kuna highway ya kulipia moja tu inaitwa m6 toll mind you kuna m6 ya kawaida hulipii....kulipia ni optional kama hutaki kuhangaika na foleni, na ndio watakachofanya hapo chalinze,hio ya bure itakuwepo ila watajenga ingine ku-bypass kwa watakaokuwa tayari kulipia watatumia hio....naunga mkono hatua hii
 
Wakijenga ya kulipia hiyo ya kawaida haitapewa huduma zozote ili wote muwe mnalipia.
 
sio kweli sio dunia nzima na sio kila highway ni lazima ulipie.....mfano uk kuna highway ya kulipia moja tu inaitwa m6 toll mind you kuna m6 ya kawaida hulipii....kulipia ni optional kama hutaki kuhangaika na foleni, na ndio watakachofanya hapo chalinze,hio ya bure itakuwepo ila watajenga ingine ku-bypass kwa watakaokuwa tayari kulipia watatumia hio....naunga mkono hatua hii

lazima ziwepo barabara za mbadala za bure kwanza
 
hawa wez kila lita 1 inatozwa shs 200 kwa ajili ya barabara, je wametengeneza zipi?
je kod zetu zinalipia nn..
hii nchi hii tutakuja kuonana wabaya.

HUYO ISSA hapo ikulu ni DALALI TU WA KUKUSANYA 10% HAKUNA CHA BRN WALA UPUUZI!! ALISHAFANIKIWA KUTUIBIA ttcl NA SASA ANATAKA KUMALIZIA KABLA MKWEREEEEEEE HAJANG'ATUKA!!! HILO NDIO DILI LAO WADANGANYIKA!!
 
bora maana nikienda dar nakumbwa na garama zisizo za msingi, ntakuwa siendi tena dar1 ccm oyeee! kama ni kweli
 
Watu wengine...??? Eti hata ulaya wanalipia!

Ndiyo, lakini kunakuwepo njia mbadala za kufika huko. Je, hali iko hivyo hapa bongo na hususani kwa bara bara hiyo? Je, wataweka option hiyo?

Mipango mingi utekelezaji sifuri. Yale mliyoa ahidi 2010 yamewashinda
Yale mliyokubaliana kama mipango ya Taifa 2015 hola
Yale ya 2025 implementation startegies/ preparations zero!
Kigamboni, zero!
Mipango miji Dar, sifuri
Maji mijini na kijijini sifuri
Bandari ya Bwagamoyo, sifuri
Bandari ya D'salam hola
Reli ya kati chali.... na barabara zinabomoka kwa sababu ya malori mengi kila leo mnashusha malori mapya!
Viwanja vya ndege vya kimataifa Kigoma, vipi status?
Huduma bure kwa wazee, hali ikoje?
Elimu je? au ndo mpango wa kupanua gori (BRN) ili hata kipofu (sorry) naye afunge gori???
Vipi kilimo kinacho beba watanzania over 80%, hali ikoje kwa maana ya upatikanji wa Matreacta na zana za umwagiliaji??!

Mipango ... mipango tu mdomoni! Sihasa hizi!? Shkuruni watanzania mliwanyima elimu hawajitambui!
Mkuu Ubabaishaji wa serikali hii ndio maana East africa Tanzania imetengwa Railways Kenya imeshaanza kujengwa..

Tatizo la Tanzania yaelekea waliomba 10% walipoona wenzao hawana hiyo tamaa Tanzania ikagoma na Jamaa kina Kagame,Uhuru na museven wakasepa na kuendeleza wakiwaambia Tanzania mkiwa tayari mtasema...

Kiujumla Serikali yetu ni bure... kama iko haipo vile... Nchi inajiendesha yenyewe...
 
View attachment 187854 View attachment 187856

Serikali inafikiria kuipa sekta binafsi barabara Dar kwenda Chalinze kuijenga upya ,kwa mujibu ya muheshimiwa Omari Issa anayehusika na uwezeshaji na utekelezaji ofisi ya rais kama alivyoongea na kituo cha ITV katika kipindi cha dakika 45, alisema sekta iyo binafsi itapewa dhamana ya kukusanya pesa kwa magari yatakoitaji kupita katika barabara iyo ya kisasa itakayojengwa.

Nchi zilizo endelea ndivyo zinavyofanya!
 
Hah! barabara inalipiwa kwani imekuwa uwanja wa ndege? futa kauli yako hiyo mbovu. Kwanza hii serikali imekuwa ya kihuni na wote wanoongozwa ni vipofu, vyanzo vya kodi zenu hazitoshi? mbona hamuwadhibiti mafisadi wanaongezeka kila siku?

We need truly Tanzanian Leaders sio hawa wachumia matumbo.
 
Tutalipa pesa nyingi mno.., inamaana wao wanashidwa kusimamia hiyo barabara..??!
 
Ujinga wetu ni kuiga kila kitu bila kuchunguza kwanza....Ipo toll charge kwenye barabara nchi za wenzetu lkn kunakuwa na mambo mengi ya kuzingatiwa....mfano mumejenga barabara mbadala ya kufika hapo chalinze isiyo ya kulipia...?mi nakwambia hawa wakwere mpk waondoke....tutaona mengi....

Barabara za kulipia ni chache sana, tena sio zile zinazotumiwa na watu wengi, nying ni za binafsi
 
wazo zuri sana, hiyo watu wameniwahi. proporsal yangu ya kubomoa jengo la bunge na kujenga kubwa na la kisasa likiwa na underground train ya mwendo kasi kulink dar-dom ili wabunge walale dar waibuke dodoma ndani ya 15minutes inaendelea vizuri, wabunge na watazamani wataingia kwa kiingilio kidogo tu na kitakuwa inclusive na nauli ya train. hiyo ikipita nakuja hapo magogoni hiyo ikulu ni ndogo sana, nitavunja na kujenga ikulu inayoendana na hadhi yetu, kisha mpangaji atalipia pango kidogo tu. tuchangamkieni fursa jamani.
 
Road licence tunalipa kila mwaka itafanya kazigani ??

akufukuzae akwambii toka ujue hapo wameshatuchoka
 
GDP ya mtz ni sh ngapi?je,iko sawa na wa UK,US na kwingineko tunakopenda kuiga kila kitu chao?

Kama kuna kitu kinatutafuna watz ni kukosa elimu.
 
Back
Top Bottom