BARA ZAmani, leo ni sLAa aMA WAZIRI

nimie

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
525
104
Nchi hii bana, hadi natoa povu hapa nilipo! Angalia huyu alivyopinda, wenzie wakaona wamkandamize ngoma ikifika duru la pili, hadi analialia, kosa lake kayaanza mwenyewe. We thought he was sir Accurate especially in Public relation, but we were wrong, kuna huyu naye ana haraka kama makinda ya ndege kwa hamu ya posho ya jioini! Vururuvururu tu, siuliona na yule ambaye amelowa sasa? Yule aunt naye ni ghasia tupu! hawa jamaa bana, kama yule anayependa posho utafikiri kakosa mia! Kuna mwingine yule kapigana hadi kaingia ikulu kuvila vinono, hahaha nampenda yule yuko kama mwa_ri wa moto, unaripuka na kuzima hapo hapo mitaani. Mwingine huyu kaingia humu kwa majaliwa tu, ila mkuu lo! yeye bajeti yake taabu tupu. Acha sasa huu uwekezaji wa siku hizi mwenzenu nagutuka. Kama hivi ndivyo si heri na mie ningeteuliwa?

Duh hadi nimemkumbuka kocha albeto Pereira wa brazili, maana tunapigwa chenga tu. Si unaona huyu naye kaletwa toka kwao na waliomleta nasikia waliambiwa mkimfikisha msirudi, kisa alikuwa anapenda kuvua Indian ocean na boti anayopanda nahodha akaa nje! Kha, mis u so much mbona unasumbukaga shekifu?

Komba ni mnyama mvurugaji, anayemtunza akataka kupigaseli na katiba yetu, kwi kwi. Ndo mana nilitaka nimchome mbele za watu tena nje hadharani kwa unafiki wake! Anaimba taarabu kwa mahadhi ya sindimba! Afadhari huyu dogo haumwi, nyimbo zake ndo utafikiri mgonjwa yaani taratibu, huko mbele huenda akawa na mashabiki kibao. Hebu niulize swali wajameni, hivi mifugo tunaweza kuiona ngorongoro?

Teknologia hii nayo, hadi watoto wanajua mengi, nimemsikia mtoto eti “mama mi taka enda Maka menyewe”, kumbe aliona kwenye TV waendao hijja. Babaye kashindwa kutumia teknologia, mtu mzima nimemkuta akitwanga, na sina hakika kama dadae ana tiba ya tatizo la ardhi na makazi hapa home. Nilitaka niumueleze kielimu kuwa wanyama wanaibiwa, akasema igeni wazungu tu, hii bongo mtakoma!

Nikamuuliza yule dogo, hivi pale Moro mto ngelengele jamani hatuwezi kupata nishati! Akanijibu eti maadam unataka kutumia huo mto nenda kapande malimao! Si nikatoka hoi, mara namkuta dokta barabarani kalewa pombe chakali, makufuli ya salawili open na maneno anayotoa mdomoni balaa! Mara akapita kuli anayedili na uchukuzi wa mizigo wallah hadi katoka nundu, nikajiuliza is that human nature? Angekuwa wa Iringa huyu saa hizi tungejua ni mtafutakamba akafanye ile shughuli. Nikawaza niaje viwanda vyetu kila kukicha migogoro tu na vinakufa as a result biashara zote kama za viraza, “roma haikujengwa siku moja” ndivyo wanavyotupumbaza, mbona wachina wametekanyara, ndururu zote zenda kwao? Watoto nao wanafeli, mhusika anaimba “nashukuru, akawambwa msalabani Yesu” hivi kweli inahuu? Nikasogea shule ya jirani na kuchungulia maabara namwona mwalimu anapima pH ilipofikia kujua kama ni alkali, nikasema simlaumu, Lugome ndo kijijini kwao.

Nikamkuta mwana wa mkulima analalamika eti “daktari wa afya huwa haji Mpanda”, mie sikushangaa sana because even at Mtera there is a maximum mark for water, si ndo nikakumbuka hata jamaa wamempiga alama asigombee unyerere! Mdomoni natabasamu, eleweni tu, ila sitaki tena sipendi mambo haya yaendelee bongo wala EA!

Nawasilisha.
 
Big up, JK angekuwa mbunifu kama wewe tungekuwa tumeendelea zamani sana.
 
Nimuhimu kujiliwaza ukiwa kwenye nchi ya stress kama hii!!
Umeona eeh, ndo hivo sasa. Unaumwa uko wodini maumivu kibao halafu madaktari wamegoma. Itabidi tu ujifanye Nguza Viking!
 
Big up, JK angekuwa mbunifu kama wewe tungekuwa tumeendelea zamani sana.

Aminia babaake, nasikia anampango wa kuachia ngazi njiani maana chombo kinakwenda mrama. Nashukuru kujua nina kura ya pili ya uhakika baada ya ile ya kwangu!
 
kama kweli umebuni mwenyewe.huna mpinzani we ni mkali.ila usiache kipaji chako kikaja potea bure.
 
kama kweli umebuni mwenyewe.huna mpinzani we ni mkali.ila usiache kipaji chako kikaja potea bure.

Mwana nashukuru, ila umenishtua kuita kipaji. Ni changamoto fulani, ngoja tuone. Again thanks!
 
Back
Top Bottom