Arnold Kalikawe
Senior Member
- Sep 28, 2016
- 146
- 340
Hivi karibuni kumekuwa na uhaba wa sarafu ya Dollar Duniani, kitu ambacho kimepeleka pia sarafu za nchi nyingi barani Afrika kuyumba, na vitu kupanda bei bila mpangilio.
Kwa sababu mimi pia ni Admin wa page moja ya facebook inayoitwa Icon Africa ambapo humo tupo ma-Admin wengi kutoka nchi za Afrika na kila mmoja anapost mambo ya nchi yake ususani utalii. Basi nikaamua kwenda kwenye page kuuliza ni namna gani tuwaweza kuwa na pesa yetu ya bara la Afrika ili kuepuka madhara ya Dollar.
Na kama mnavyojua nchi zetu nyingi za kiafrika bado zinatumia sarafu ya Dollar kufanya manunuzi sehemu mbali ndani na nje ya bara la Afrika. Hivyo ukosefu wa sarafu ya Dollar imepelekea pia nchi nyingi kutikisika kiuchumi. lakini endapo tungekuwa na sarafu yetu ya bara la Afrika kama jinsi ilivyo sarafu ya Ulaya (Euro €), basi tutakuwa imara kiuchumi, hata kama dollar ikitikisika, sisi bado tutakuwa salama. Na pia tutaweza kufanya manunuzi ndani ya bara letu bila kutatizwa na kupanda na kushuka kwa sarafu ya Dollar.
Nimeanza kuona muitikio mkubwa wa watu mbalimbali kwenye comment za hiyo post wakipendekeza Sarafu iitwe Afro au Afric. Na muitikio ni mkubwa na kila mwafrika anatamani tuwe na sarafu yetu. Haya maoni ni namna gani yanawezwa kufikishwa Africa Union na yakafanyiwa kazi kwa haraka. Maana sidhani kama kuna nchi ya kiafrika inataka kuendelea kuikumbatia dollar