Banzastone taabani hospitalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Banzastone taabani hospitalini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, May 8, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  May 8, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  na Khadija Kalili

  MTUNZI na muimbaji mahiri wa nyimbo za muziki wa dansi nchini, Ramadhani Masanja ‘Le General Banzastone’, au ukiweza mwite ‘Mwalimu wa Walimu’ amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mwananyamala iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

  Habari kutoka chanzo cha kuaminika zimesema msanii huyo yuko hoi na amelazwa katika hospitali hiyo mwanzoni mwa wiki hii kwa matibabu.

  “Hali ya Banzastone ni mbaya, amedhoofu mno hali inayopelekea kuonekana kana kwamba amechanganyikiwa hivyo mipango inafanywa apelekwe katika hospitali ya wagonjwa wa akili ya Mirembo iliyoko mkoani Dododma,” kilisema chanzo hicho.

  Hii itakuwa ni mara ya pili kwa msanii huyo kuumwa na kuwa taabani, mara ya kwanza aliugua hadi akasingiziwa kuwa kafa mwaka 2006 ambapo aliibuka na albamu ya ‘Hujafa Hujasifiwa’ wakati huo akiwa ni mwanamuziki wa Bendi ya Twanga Chipopolo.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Get well soon....Banza!
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,315
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Anajidunga sana hajali afya yake......hata mwenzie Diof nae teja...
   
 4. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Get well mr Banza............labda hiyo ni celebral malaria inabidi wamchecki kwanza kabla hawajampeleka milembe...ile si hopital ya vichaaa?
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Katika hali aliyonayo wale waliofaidika(kifedha) na sauti yake wanahitajika mchango wao haraka kumsaidia, hapa nawazungumzia dada Asha Baraka na cpt. John D. Komba. Halafua hawa wauza madawa ya kulevya wanatuharibia vijana wetu kama hawa na vipaji vyao kwa nini wasiwauzia watoto wa mafisadi na mafisadi wenyewe?
  wana JF mimi naona ipo haja ya kuwataja humuhumu tuwajue wauwaji hawa wa vijana wetu kama wanavyotajwa mafisadi. I wish marehemu A.Chifupa angewataja japo wawili watz wakawajua.
   
 6. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Waandishi Wetu! Angefanya la maana zaidi kwa kukimbia mara moja hapo Mwananyamala Hospital na kutuletea taarifa from the Horse's Mouth badala ya kutegemea sana 'Chanzo cha Kuaminika'!
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Chanzo cha kuaminikina anaweza kuwa familia ya Banzastone.
   
 8. M

  Mubii Senior Member

  #8
  May 9, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 149
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Its so sad kuona kwamba Banza yupo kwenye hali hiyo. Yeye na wenzake Choki na Muumini kwa kweli wana talent ya muziki lakini inasikitisha hawana mafanikio niliyotegemea. Nadhani wamechanganya kufikiri wangeweza kumiliki ama ku-run bendi jambo ambalo ni eneo la management ambalo nadhani hawana uzoefu nao. Ingekuwa vyema watulie kwenye bendi na wahakikishe wana mkataba mzuri wa kuwapa mapato ya kutosha na ya muda mrefu. Wasingekuwa walivyo sasa hivi.
   
 9. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  ...anaweza pia kuwa adui asiyemtakia mema. Haikufafanuliwa. The best thing would have been kwa muandishi huyo kwenda kuhakikisha mwenyewe kwa macho hasa ukichukulia kuwa Mwanayamala Hospital ni 'hapo nje' tu! Mara ngapi tumeishasikia 'Vifo' vya watu maarufu jijini kutoka kwa 'Chanzo cha Kuaminika'??
   
Loading...