Bank ya NMB tawi la Mbezi Beach ina shida gani?

Haya mambo kumbe yapo aisee.
Kuna siku pale UDSM kuna mama mmoja nikaona anang'ania kuhesabu upya kama milioni 6 hivi. teller akawa anamwambia mashine haikosei, hesabu ipo kamili. Mama akasema hapana lazima ahesabie coz kuna benk alishawahi kupigwa kizembe. Ikabidi wamwingize kuna kichumba alienda kuhakiki mzigo wake kule.
 
Kwani 300M si unaomba private room(bulk) ili ujiridhishe mkuu. Yaani sababu ni pesa nyingi ndio uondoke bila kujiridhisha! Anyway, labda sababu tunavuja jasho kwa njia tofauti.
Kuanza kuhesabu 300M inawezekana kwa machine. Ila wachache hufanya hivyo.
 
Ata urudi kwa mkurugenzi nakuhakikishia hupati, coz wameweka tangazo wazi kuwa please count your money before leaving the counter, so kama una haraka zako na hujahesabu ukipiga hatua tano tu ukagundua imepungua inakuwa imekula hyo.

Juzi nilikwenda kufanya transactions nyingine nikamcheki manager akanambia mfuate yuleyule jamaa ongea naye. Nimekwenda kwa jamaa nikaongea naye kirafiki sana akaomba vocha ya muamala akatoa kopi nikampa na namba ya simu ila jamaa anaonekana alinipiga coz hajiamini kabisa
 
nm.bb magomeni ndo hatari zaidi. kipindi nafanya kazi udart kwenye kudeposit mauzo ya tiketi lazima upigwe, ukimstukia analeta fundi wa IT aje kufix money counter machine as if ilikua mbovu.

kwa mawakala nako ni hatari ..always chek confirmation sms ndo uondoke, nlitoa laki nne sms ikaja laki nne mara mbili. nikamwambia why umetoa hio pesa two times kwa ukali..akaanza kutetemeka anasema bro ni mtandao tu.
Mtandao huwa unazingua kweli huenda hakudhamilia kutoa 2 times
 
kama mnavyosemaga Dirisha za huduma ziko sita wahudumu wawili ukippesa zako sogea kwenye dirisha ambalo hakuna muhudumu hesabu hela zako taratiiibu jiridhishe ndo usepe nasema usogee kwenye dirisha lisilo na mtu kwasababu kuna security cam ambazo zinamlinda yule muhudumu na mteja hivyo ukihesabu hata zikipelea watareview security cam ya dirisha hilo na wataona ila habar za kuleta haraka kisa uoga kijinga m sina
alaf kwan kuhesabu 30m ni dakika ngapi mzee wangu mpka useme utachelewa uwe na harak kias hiko
 
Ndugu zangu habari zenu.

Bank ya NMB tawil la mbezi Beach pale Africana limekua likihusishwa na matukio mengi ya ajabu kama utapeli, uwizi na matukio ya kijambazi.

Ijumaa nimepigwa na kitu kizito pale NMB nimepigwa 400,000/= taslimu na teller. Ilikua hivi nilikua na haraka sana nawai mtu kariakoo kuna pesa alikua ananidai ndo kupitia pale bank ili nitoe pesa dirishani nilitoa 3,500,000/=. Na hii yote kuepuka makato ya kutoa kwa wakala.

Jamaa alinipa zile hela bunda 4 ( bunda za elfu 10 zilikua 3 na bunda la elfu5 lilikua moja) hata sikuhesabu nikachukua bunda moja la elfu10 nikaweka mfukoni zingine nikatia kwenye bag nikachukua boda mpaka kariakoo.

Nilipofika karikaoo nikatoa pesa mfukoni nikachomoa 780,000/= nikampa jamaa ilobaki nikatia mfukoni sababu jamaa alikua dukani kwangu. Sikukaa dukani palepale nikasepa nikaweka bag langu kwenye kiti cha mbele cha gari mpaka home sikupitia sehem yoyote.

Home nikatoa pesa zikaweka kwa droo, sasa leo asbh nikahesabu zile pesa nikakuta bunda1 la elfu10 kuna pungufu ya 300,000 na bunda ya elfu5 kuna pungufu ya 100,000 jumla nimepigwa 400,000/=.

Baada ya tukio hili nikalink na matukio ya nyuma niliyosikia au kuambiwa.

Mamdogo wangu mwakajana alipigwa 700k palepale mbezi Beach alikwenda kutoa pesa za kampuni yeye ni mhasibu alitoa 35,000,000/= akakutana na shoti ya 700k.

Na mshikaji wangu mwingine alipigwa 200,000 hapohapo mbezi naye alitoa pesa akakutana na hio short.

Hapa home na jirani yangu mwanasheria baada ya kumchana hii ishu akanambia hapo mbezi ni pabaya sana kila mtu analalamika kuna baadhi ya wafanyakazi sio waadilifu.

Nafanya miamala ya pesa mingi sana na CRDB personally na ofisi lakini sijawai kuta hata shoti ya elfu10. Hizo pesa kuna mtu nilifanya naye biashara ndo akaomba afanye malipo kwa NMB (transfer).
Kwa mtu anayefanya biashara hio pesa ni kubwa sana ukitegemea biashara zilivyo ngumu kwa sasa.

Lengo la uzi ndugu zangu tuwe makini sana tunapofanya miamala ya pesa iwe bank kwa mawakala. Hata ahesabu mbele yako kwa mashine rudia tena kuhesabu mamdogo wangu alipigwa 700k na alikua anashuhudia zinahesabiwa kwa macho yake lakin alipigwa.

Kuna jambo nitalifanya kwa mateller wezi kama hawa subirin mrejesho tu.
yan kwenye million itolewa 300k na usi jue tuwe serious kidogo labda ushiki ela mala kwa mala
ila pia wa tz asimili kubwa ni wez kuna jmaa wangu teller alikosea akamzidishia 100k jmaa aka kausha tu dadeki na anatamba ety jmaa kajichanganya
 
Back
Top Bottom