Bank ya NMB tawi la Mbezi Beach ina shida gani?

Bank ya NMB tawi la Mbezi Beach ina shida gani?

Cash Generating Unit

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
13,284
Reaction score
39,513
Ndugu zangu habari zenu.

Bank ya NMB tawil la mbezi Beach pale Africana limekua likihusishwa na matukio mengi ya ajabu kama utapeli, uwizi na matukio ya kijambazi.

Ijumaa nimepigwa na kitu kizito pale NMB nimepigwa 400,000/= taslimu na teller. Ilikua hivi nilikua na haraka sana nawai mtu kariakoo kuna pesa alikua ananidai ndo kupitia pale bank ili nitoe pesa dirishani nilitoa 3,500,000/=. Na hii yote kuepuka makato ya kutoa kwa wakala.

Jamaa alinipa zile hela bunda 4 ( bunda za elfu 10 zilikua 3 na bunda la elfu5 lilikua moja) hata sikuhesabu nikachukua bunda moja la elfu10 nikaweka mfukoni zingine nikatia kwenye bag nikachukua boda mpaka kariakoo.

Nilipofika karikaoo nikatoa pesa mfukoni nikachomoa 780,000/= nikampa jamaa ilobaki nikatia mfukoni sababu jamaa alikua dukani kwangu. Sikukaa dukani palepale nikasepa nikaweka bag langu kwenye kiti cha mbele cha gari mpaka home sikupitia sehem yoyote.

Home nikatoa pesa zikaweka kwa droo, sasa leo asbh nikahesabu zile pesa nikakuta bunda1 la elfu10 kuna pungufu ya 300,000 na bunda ya elfu5 kuna pungufu ya 100,000 jumla nimepigwa 400,000/=.

Baada ya tukio hili nikalink na matukio ya nyuma niliyosikia au kuambiwa.

Mamdogo wangu mwakajana alipigwa 700k palepale mbezi Beach alikwenda kutoa pesa za kampuni yeye ni mhasibu alitoa 35,000,000/= akakutana na shoti ya 700k.

Na mshikaji wangu mwingine alipigwa 200,000 hapohapo mbezi naye alitoa pesa akakutana na hio short.

Hapa home na jirani yangu mwanasheria baada ya kumchana hii ishu akanambia hapo mbezi ni pabaya sana kila mtu analalamika kuna baadhi ya wafanyakazi sio waadilifu.

Nafanya miamala ya pesa mingi sana na CRDB personally na ofisi lakini sijawai kuta hata shoti ya elfu10. Hizo pesa kuna mtu nilifanya naye biashara ndo akaomba afanye malipo kwa NMB (transfer).
Kwa mtu anayefanya biashara hio pesa ni kubwa sana ukitegemea biashara zilivyo ngumu kwa sasa.

Lengo la uzi ndugu zangu tuwe makini sana tunapofanya miamala ya pesa iwe bank kwa mawakala. Hata ahesabu mbele yako kwa mashine rudia tena kuhesabu mamdogo wangu alipigwa 700k na alikua anashuhudia zinahesabiwa kwa macho yake lakin alipigwa.

Kuna jambo nitalifanya kwa mateller wezi kama hawa subirin mrejesho tu.
 
Pole sana mkuu ....Bora kutoa hela kwa wakala unakua na uhuru wa hat kuzihesabu ...Bank sometime kutokana na Ile foleni ya watu ...wengi wanakua na hofu kuwa anawachelewesha wengine .....Afu pia hii ya kuhesabiwa pesa kwenye vile vi machine bado haitoshi coz wanatabia baada ya kuzihesabu anaakuangalia km umeconcentrate kwake akikuta unaangalia pembeni au kwenye simu anaweza akadondosha hata 50k chap afu akaifunga ile hela ....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi sana aseee [emoji1373]
 
Kuna mizigo kazi kuhesabu, inabidi uwaamini tu. Uneenda toa 300millions unawaamini tu
 
Niliwahi kunusurika kupigwa 100,000 CRDB. Ilikuwa hivi, nimekwenda kuweka fedha, nikampatia mhudumu 300,000, akaweka 200,000. Nilipoangalia ile karatasi ya kuweka fedha nikagundua haikuwekwa pesa yote, nikamuuliza imekuwaje? Akasema amepitiwa, akaweka 100, 000. Unaweza pigwa wakati wa kuweka na kutoa, kuweni makini, hakiki kabla haujaondoka.
 
Kwenye pesa hakuna uaminifu, that's why wanakwambia count your money before leaving the counter! Hii huwa ina maana kubwa mno! Huna wa kumlaumu. All blames on u brother! Imani na haraka vinawaponza wengi counter
 
Back
Top Bottom