Bank teller alivyotapeliwa

Bank teller alivyotapeliwa

Kumbe siku hiyo na wewe ulikuwepo? Mimi ndio nilifika nataka kutoa pesa nikamtajia kiasi nachotoa. Akazitoa azihesabu, alichokikuta ni siri ya wengi.

Halafu kalikuwa kabishi sana tunakaambia piga simu customer care waambie umekosea namba, kakaanza kutuuliza "mnanifundisha kazi?" Utadhani polisi. Basi bwana kakasema MIMI NI WAKALA NIMEMTUMIA MTU PESA LAKINI AMENIPA KIASI PUNGUFU, BADALA YA LAKI SITA AMENIPA LAKO NA NUSU. Voda wakamwambia MUONGOZO UNAMKUTAKA KUHAKIKI KIASI KABLA YA KUMUHUDUMIA MTEJA, ASANTE. Nilicheka kama mazuri vile, hii ilikuwa Mwanza mwaka 2015 hv
Hii imetokea pia dodoma juzi Kati tu hapa. Mdada Kala hasara ya zaidi ya laki 6 kwa style hiyo. Matapeli sio watu wazuri
 
Stories ya kutunga haiwezekani. Yani upewe kibunda bila kuzifungua.
Otherwise tuambie ilitokea wapi?
Ilimtokea mfanyakazi wangu Mpesa. Kapewa laki sita, mara ghafla imegeuka laki moja. Buku mbili mbili tupu. Unapewa unahesabu, anaziomba ukimpa anarudisha sio zile za kwanza. Ukiwa mzembe imekula kwako
 
Iko hivi..

Jamaa mmoja alikuwa na Dola za kimarekani elfu kumi (kama milioni 20 za kitanzania). Akafika bank na kwenda dirishani moja kwa moja.

Baada ya kufika dirishani akampa pesa hizo dola ili abadilishe na kuwa pesa za kitanzania. Yule teller akapokea na kuzihesabu pamoja na kuhakiki kama ni halali. Baada ya kuridhika nazo kuwa zipo sawa wakati anataka kuanza kuhesabu za kitanzania yule jamaa akauliza exchange rate ipo vipi?

Akatajiwa akasema ndogo sana naomba dola zangu. Akarudishiwa akajifikiria kama sekunde kadhaa akamrudishia tena yule teller basi nipe hivyo hivyo tu.

Yule teller bila hata kuzikagua tena zile Dola akapokea na kuanza kumuhesabia jamaa pesa zake na kumpatia.

Jamaa akaondoka, kufika muda wa kufunga hesabu anafungua zile dola anakuta ya juu na ya chini ndio pesa halisi. Yaliyobaki yote makaratasi.

Maoni yangu:
Matapeli wawe wanachomwa moto maana wanaharibu maisha ya watu fikiria pesa zaidi ya milioni ishirini unaenda kumtapeli mwenzio ni sawa na kutaka kumuua.

Nawasilisha.
Hugo teller in mzembe , hela ikitoka dirishani hata km hazijafunguliwa ,ajirudisha tena lazima uhesabu......ajali kazini
 
Mingine inakuwa ni michongo wanafanya hao tellers...

Unapanga tu na mtu mchezo mzima, ushaidi utaonesha umetapeliwa kumbe ni sehemu ya igizo...
Utailipa tu,segerea inakusubiri
 
kwani siku hizi bank teller wanakaa ndani ya vioo vyenye tinted

visivyoonyesha hata mteja anachofanya nnje ya kioo?
Wale huwa wamejipanga mapema, hafanyii mchezo wake pale.

Zile halisi zinakuwa peke yake na fekelo peke yake.

Kitendo cha kumrejeshea, ndani ya sekunde tayari kamaliza kitendo cha ubazazi.

Ni vilevile kama wafanyavyo Kariakoo, unaoneshwa kitu halisi, kwenye kukabidhiwa ndo mchezo unapochezwa, ingawa hao lazima wawe wawili, lakini kwa teller mtu anaonekana kuanzia tumboni halafu anachofanya chini haukioni, hata wewe mkuu ungelizwa tu!

Dawa yake pale ni kuhakiki bila kuchoka, hapo tapeli yangelimfika ya shingo, utasikia linaanza kujitetea kijingajinga....'kaka nthamee'...!
 
Ilimtokea mfanyakazi wangu Mpesa. Kapewa laki sita, mara ghafla imegeuka laki moja. Buku mbili mbili tupu. Unapewa unahesabu, anaziomba ukimpa anarudisha sio zile za kwanza. Ukiwa mzembe imekula kwako
Hivi huyo mbwa ukimbainia kama hapo benki si atajidharau mwenyewe!
 
huyo teller ni mzembe kwa nini asingehesabu
Don't trust a customer yule teller ni mzembe, ile ni kazi yake alitakiwa ajiridhishe kwa kutumia mashine kujua kama zimetimia USD 10,000 na hapo hapo angegundua kuwa ni fake.Yeye kapokekea mzigo na kuuweka bila kuhakiki.Hili liwe funzo kwa ma-teller wengine.
 
Hawa mpaka siku waibiwe wao ndo wataelewa uwa watu wanaibiwa vipi
Wizi kama anaosimulia uliwahi kutokea mwaka 2008 branch mojawapo ya Dar, tena ya benki kubwa tu hapa bongo. Yaani ilikuwa hivyo hivyo ila wale walikuwa na begi liko chini miguuni waliporudishiwa wakainama na kuchukua mzigo feki then wakasema tupatie tu kwa hiyo rate. Baada ya uchunguzi wa CCTV kamera ikabidi asamehewe tu, wizi mdogomdogo unatokea sana ndani ya mabenki na hutosikia kwa vyombo vya habari.
 
Iko hivi..

Jamaa mmoja alikuwa na Dola za kimarekani elfu kumi (kama milioni 20 za kitanzania). Akafika bank na kwenda dirishani moja kwa moja.

Baada ya kufika dirishani akampa pesa hizo dola ili abadilishe na kuwa pesa za kitanzania. Yule teller akapokea na kuzihesabu pamoja na kuhakiki kama ni halali. Baada ya kuridhika nazo kuwa zipo sawa wakati anataka kuanza kuhesabu za kitanzania yule jamaa akauliza exchange rate ipo vipi?

Akatajiwa akasema ndogo sana naomba dola zangu. Akarudishiwa akajifikiria kama sekunde kadhaa akamrudishia tena yule teller basi nipe hivyo hivyo tu.

Yule teller bila hata kuzikagua tena zile Dola akapokea na kuanza kumuhesabia jamaa pesa zake na kumpatia.

Jamaa akaondoka, kufika muda wa kufunga hesabu anafungua zile dola anakuta ya juu na ya chini ndio pesa halisi. Yaliyobaki yote makaratasi.

Maoni yangu:
Matapeli wawe wanachomwa moto maana wanaharibu maisha ya watu fikiria pesa zaidi ya milioni ishirini unaenda kumtapeli mwenzio ni sawa na kutaka kumuua.

Nawasilisha.
Kwa ujinga wake mwache atapeliwe ili wajinga na wazembe wazidi kupungua!!
 
Ilimtokea mfanyakazi wangu Mpesa. Kapewa laki sita, mara ghafla imegeuka laki moja. Buku mbili mbili tupu. Unapewa unahesabu, anaziomba ukimpa anarudisha sio zile za kwanza. Ukiwa mzembe imekula kwako
Kuna kua na mafungu mawili ya pesa! Fungu A linakua kamili na ndiyo unapewa ili uhakiki ukisha hakiki tu lazima afanye jambo lolote lile litakalo mfanya uumpe zile pesa tena na ukisha mpaa tu hapohapo anakwambia ok poa tufanye biashara na hapohapo ana kupa fungu B ambalo ndiyo kanjanja na ukiwa mvivu wa kuhakiki kwa mara ya pili ndiyo imekula kwako hiyo!!
 
Back
Top Bottom