Mkuu haujawahi kukumbana na mikono ya tapeli namna anavyoweza kukuonesha kitu halisi, utapojipinda kuhesabu hela ya kumlipa, muda huo huo kwake ni fursa ya kupokezana na kubadilishana hicho kifaa na tapeli mwenzake?kwani siku hizi bank teller wanakaa ndani ya vioo vyenye tinted
visivyoonyesha hata mteja anachofanya nnje ya kioo?
Kumbe siku hiyo na wewe ulikuwepo? Mimi ndio nilifika nataka kutoa pesa nikamtajia kiasi nachotoa. Akazitoa azihesabu, alichokikuta ni siri ya wengi.Mawakala wamepigwa sana katika mfumo huo kuna dada alipewa laki sita akahesabu ziliporudi mara yapili zikawa laki na hamsini aliwekewa elfu mbilimbili kati
Iko hivi..
Jamaa mmoja alikuwa na Dola za kimarekani elfu kumi (kama milioni 20 za kitanzania). Akafika bank na kwenda dirishani moja kwa moja.
Baada ya kufika dirishani akampa pesa hizo dola ili abadilishe na kuwa pesa za kitanzania. Yule teller akapokea na kuzihesabu pamoja na kuhakiki kama ni halali. Baada ya kuridhika nazo kuwa zipo sawa wakati anataka kuanza kuhesabu za kitanzania yule jamaa akauliza exchange rate ipo vipi?
Akatajiwa akasema ndogo sana naomba dola zangu. Akarudishiwa akajifikiria kama sekunde kadhaa akamrudishia tena yule teller basi nipe hivyo hivyo tu.
Yule teller bila hata kuzikagua tena zile Dola akapokea na kuanza kumuhesabia jamaa pesa zake na kumpatia.
Jamaa akaondoka, kufika muda wa kufunga hesabu anafungua zile dola anakuta ya juu na ya chini ndio pesa halisi. Yaliyobaki yote makaratasi.
Maoni yangu:
Matapeli wawe wanachomwa moto maana wanaharibu maisha ya watu fikiria pesa zaidi ya milioni ishirini unaenda kumtapeli mwenzio ni sawa na kutaka kumuua.
Nawasilisha.
Boss fraud investigation ni kitengo cha polisi au hapo hapo benk kuna kitengo hikoMadogo wameajiriwa branch ya Mtwara halafu wakakbidhiwa kuoperate ATM, Branch controller naye kawaamini asubuhi anaacha kubalance akaunti ya ATM. Madogo pesa zinazobaki jana yake wanaweka pembeni wanabalance akaunti alafu wanaweka hela zingine kwa siku husika. Baada ya miezi michache washanunua magari na mishahara miaka ile ilikuwa midogo lazima uchukue mkopo ndo ununue gari. Madogo gheto limesheheni mazaga kibao. Ikabidi tuitwe wazee wa fraud investigation miaka hiyo. Wangekuwa wajanja walikuwa hawana kesi na msala ungebaki kwa controller. Madogo tumewaweka sawa na ahadi kemkem wakaingia line. Msala ukawa wao na kazi ikaisha. Sijui wako wapi siku hizi.
Zile pesa zinahesabiwa na machine,karatasi nazo alizihesabu au inakua vpSasa mimi nakwambwia hiyo ya 2008 ilitokea kabisa nakuhakikishia kwa asilimia mia, tena wale walikuwa na kama USD 20K. Tena waliokuwa wafanyakazi miaka ile walisomewa hadi email toka HQ kuwatahadharisha
Sijui benki zingine ila hiyo benki wana kitengo cha fraud kwa ajili ya matukio ambayo mengi yanahusisha wafanyakazi, mwisho wa siku ikibidi unakabidhiwa kwa vyombo vya usalamaBoss fraud investigation ni kitengo cha polisi au hapo hapo benk kuna kitengo hiko
kuwa na bundle mbili, ile ya kwanza inakuwa ni hela kweli, ili ukiwarudishia watakachokupa ndo hizo katikati makaratasi. Ni kitendo cha haraka na lile begi lililoko miguuni wewe cashier huwezi kuliona, akiinama akiinuka mzigo feki tayari mkononi.Zile pesa zinahesabiwa na machine,karatasi nazo alizihesabu au inakua vp