Mkuu ukitaka kujua ukweli tafuta sababu walizotoa Vatican kupiga marufuku Mkatoliki yeyote kujiunga na hawa jamaa! Sura yao kwa nje wanajifanya watu wa upendo lakini ndani ushetani mtupu.usiombe kuingia mkuu!
Mkuu Mtazamo, kwanza ndio leo nimejua kuwa kumbe sisi Wakatoliki haturuhusiwi kujiunga Freemason!.
Kwenye hizi secret societies, sisi Katoliki pia tuna mambo yetu. Mimi nilibahatika kutembelea pale St. Peter's Basilicca, lile dungu la mviringo, sphere kule juu ni pure gold, find out ilitoka wapi?. Ile fimbo ya Pope nayo ni pure gold, find out historia yake.
Kisha tafuta kitu kinachoitwa Wicca, ujue Kanisa Katoliki liliwafanya nini watuhumiwa wa Wicca, lakini kitu cha ajabu kabisa, chini ya kanisa kuna underground library iliyoshehenezwa vitabu vyote vya Wicca na vitabu vingine vyote vilivyopigwa marufuku na Kanisa Katoliki. Kufika huku kuna open passage na pia kuna secret passage!. Find out hiyo secret passage ni ya nini na kwa nini vitabu hivyo vimehifadhiwa?!.
Kwenye ibada zetu, tunafukiza ubani, tunakunywa divai, tuna paka maji ya baraka, tuna mafuta ya upako wa mwisho, ndani ya makanisa yetu tuna sanamu za Yesu, mapadri wetu wanavaa misalaba mikubwa, maaskofu wetu, wanavaa pete na misalaba minene ya pure gold!. Vitu vyote hivi vinatoka Roma, Italy hawana dhahabu, find out thahabu ya Kanisa Katoliki inatoka wapi?, and read a bit, who really funds the Pope, zaidi ya fedha za sadaka, na hao wanao fund the church, hizo fedha wanapata wapi na wana biashara gani?!.
Ukiishapata majibu ya maswali hayo, ndipo utagundua kwa nini Kanisa Katoliki limepiga marufuku waumini wake not only kujiunga na freemasons tuu, bali ni marufuku kwa Mkatoliki kujiunga na secret societies zozote!.
P