Bank charges ndio mapato ya Bank ambayo mwishowe hutozwa kodi. Unatozaje VAT!?

Pale benki inapochaji bank charges yaani makato kwa muamala wowote ujue ndio mapato ya benki. Pale ipochaji interest kwenye mkopo ujue ndio mapato ya benki. Makato ya namna yoyote yale kwa ujumla yafanywayo na benki ndio 'REVENUE' yake.

Mwisho wa mwaka wa mahesabu lazima mapato yote hayo yachajiwe kodi tunaita 'income tax' ama corporate tax..

Sasa serikali kama itaamua kuchaji VAT kwenye makato yoyote ya miamala ya kibenki ama taasisi ya kifedha maana yake ni kuwa hio VAT anawekewa anayekatwa. Mwisho wa mwezi benki hupeleka VAT hio TRA kwa kufanya hesabu za ulinganisho wa output na input VAT. Kila mwisho wa mwezi lazima hesabu hizo zifanyike na TRA kupata chao. Mara nyingi unaweza kukuta TRA hawapati kitu yaani wanadaiwa baada ya kufanyika mahesabu hayo ya VAT.

Sasa, serikali inapoamua kuchaji VAT kwa kila muamala wa mteja wa benki kwa namna alivyosema CG-Commissioner General maana yake ni kuwa hio sio VAT bali ni income tax yenye rate ya 18% badala ya 30% inayotakiwa kuchajiwa kwenye corporate businesses! Kwa hio hapo anachoongelea CG sio VAT bali ni income tax.!

Kwa mujibu wa kanuni za kodi za nchi yetu income tax huchajiwa mwishoni mwa mwaka wa mahesabu na VAT huchajiwa kila mwezi. Maana yake ni kwamba serikali iseme jina la kodi hio itakayokatwa kwenye muamala wa mteja lakini wasisema VAT maana sio VAT. Ama kama wamekubaliana na benki; benki wakatwe kwenye miamala wanayoyafanya basi mwishoni mwa mwaka itabidi benki ilipe corporate tax ya 12% maana 18% iliShachukuliwa kwa kila mwezi. Of which kitu kama hiki hakipo kwenye kanuni za ki kodi!

Nilichoelewa ni kwamba. Kwanza, Serikali wanataka kugawana na benki makato wanayokatwa wateja. Tatizo kubwa ni kuwa walidhani jina VAT ndio itatimiliza malengo hayo vizuri, bila kujua namna VAT inavyotakikana kuchajiwa. Pili, naona hawajaangaliana kwa kina kuhusu namna benki inavyopata mapato yake ambayo mwisho wa siku hulipia kodi. Tatu, hakuna namna yeyote ile serikali ikataka kuchaji kodi kwenye hizi miamala za kibenki halafu wananchi wasibebeshwe mzigo. HAKUNA. Nne, Naona Serikali haijabaini kuwa VAT kwenye maisha ya wananchi wa kawaida ndio inaongeza gharama za maisha. Naweza kusema kwa 'jicho la tatu' VAT inasaidia kwa kiwango kikubwa sana kudhoofisha sarafu ya Tanzania kutokana na kutundikwa kwenye bidhaa nyingi zenye watumiaji wa kawaida!

Ndio hivyo!
ungekuwa karibu ningekununulia bia, umedadavua vizuri, kama vile ulikuwa kwenye Akili yangu, hiyo Kofi lands waiite 18% withholding tax, watazuga mwishowe tutabebeshwa mzigo tu,
 
ukisoma hii mada huku umevaa ''nguo ya chama'' utaipinga kwa nguvu zote
Kwani hao wanaojifanya wafia chama cha kijani ndiyo wanakuwa exempted na hizo tozo za kodi?

Wawaulize wenzao wabunge wa CCM ambao walikuwa wanaamini kwa kuwa wao siku zote huwa wanapitisha kila jambo la serikali linalokuja Bungeni, wakadhani nao wako Salama salimini.....

Safari hii Waziri Mpango alipokuja na mpango wa kukifyeka kiinua mgongo Chao kodi, wamekuja juu kama mbogo aliyejeruhiwa......
 
the DEALER,

Umeandika vyema sana ndugu,Gavana Ndulu alichosema ni sahihi,Waliopitisha hili wanataka kutanguliza siasa kuwapooza Watanzania.
Gavana Nduļu hakuwai kusema chochote zile ni kauli za magazeti siyo ya gavana! Gavana hawezi kuongea kwenye magazeti!
 
Uko sawa 100%. Haitawezekana kuweka VAT kwenye 'bank charges' bila kuiangushia 18% kwa wateja wa bank. Kazi ya bank ni kutoa huduma ya kuhifadhi fedha, kutoa mikopo na kufanya malipo(miamala) mbalimbali kwa niaba ya wateja. Mapato yake ni riba,tozo za akaunti na tozo za huduma za miamala. Ni kwa vipi Serikali italazimisha kugawana mapato (revenue) ya benki bila kupitia kodi mwisho wa mwaka wa kodi?
kama selikali inadhani mabenk yanapata faida kubwa sana na wanataka kugawana mapato ni bora wangetengua sheria ya kodi ya mapato kutoka 30% hadi 48%, vinginevyo wakubali kuwanyonga wananchi
 
Mgh! acha wagombane tu ila mwisho wa siku sie wananchi ndio tutakaoumia tu!
 
mkuu uko sahihi huyo kamishna wa TRA amepotosha sana umma...hapo VAT lazima imwangukie mteja tu
 
Kwa mwenye elimu ya uhasibu lazima ashangae swala hili!!! Kama tumeshindwa basi turudi kwenye sales tax iliyokuwepo before VAT
 
Umeandika kisomi , ungepewa uwanja mpana hata wale wa serikali wangenong'onezana kuwa wamechemka!! Lakn tumekatazwa tusikosoe chochote kwenye serkali hii ya awam ya tano!! Usishangae kwa ukweli huu ukaitwa mchochez!!!
 
OK. Naomba pia kujua kuhusu Islamic Banking ambao hawana makato au charges zozote kwa mteja. Huwa wanaendeshaje biashara zao? Wanalipa kodi Serikalini? Kama hawa wanaweza kwanini mabenki mengine yashindwe japo kuiga utaratibu huu wenye gharama nafuu za uendeshaji?
Nchi ukiiendesha kiislam lazima iwe maskini kuliko kawaida
 
Asante mkuu unatuelewesha vizuri sana. Naomba kuuliza nipate uzoefu kwa upande wa wafanyabiashara wengine. Ninaponunua kitu kama mteja nakatwa 18 percent kama VAT. Je ni kodi zipi ambazo mfanyabiashara napeleka TRA zaidi ya VAT?
 
Naomba msaada huu ya haya....

1: Tax clearance

2:VAT

3: Mapato (TAX)

Tax Clearance isikuumize kichwa. Swala muhimu hapa ni ku clear kodi kwa maana ya kuona kama kuna kodi unapaswa kulipa na umelipa ndo tunaiita tax clearance! Kwa mfano kwa utaratibu wa sasa hv wa ku renew leseni lazima upate 'Tax Clearance Certificate' toka TRA ili upeleke manispaa nao wakupe leseni yako. Hicho cheti kinabainisha kuwa wewe mwenye kutaka leseni umelipa kodi!

VAT isikupe shida. Hii inatozwa kwa mlaji yaani final consumer ama taweza kuiita consumption tax. Kivipi? Ipo hv. Sema simu unayotumia kuingia JF inauzwa sh 100,000. Na simu hio ni moja ya bidhaa zinazotwa VAT. Sasa muuza simu atakuandikia risiti ya sh 180,000 yaani unamlipa pesa hizo. Mwisho wa mwezi kuna mahesabu atafanya yaani mahesabu ya VAT. Lengo ni kuona kiwango halisi anachopaswa kuwalipa TRA. Hili hufanyika kwa sababu naye kuna sehemu pengine amenunua kitu na kawekewa VAT. Sema kuna sehemu na yeye katozwa VAT ya sh 16,200 yaani kuna sehemu kakuta mzigo unauzwa sh 90,000 lakini akachajiwa VAT sh 16,200 kulazimika kuandikiwa risiti ya sh 106,200. Sasa mwisho wa mwezi analinganisha ile sh 18,000 aliochaji na ile sh 16,200 aliochajiwa. Kwa hio unaona hapo kuna tofauti ya sh 1,800. Sasa hio sh 1,800 ndo anatakiwa awapelekee TRA. Kama kwa mfano hesabu ikawa sh 16,200 less sh 18,000 maana yake itakuja sh -1,800 na hii inaonyesha kuwa TRA wanadaiwa na deni hili litalipwa kwenye mwezi ufuatao yaani una carry forward!

Kwa nini kila mwezi mahesabu ya VAT hufanyika? Hufanyika kwa sababu pale alipokuandikia risiti ya sh 118,000 haina maana kuwa zote ndio kipato chake hapana. Kipato chake hapo ni sh 100,000 tu na yule aliyemwandikia risiti ya sh 106,200 hapo kipato chake naye ni sh 90,000 tu! So mahesabu muhimu ili kuwekana sawa.

Mapato hii usijali. Unakumbuka pale sh 100,000 na sh 90,000? Sasa hayo ndio mapato ya hao wauzaji ambayo mwisho wa siku hutozwa kodi. Hutozwa hv. Wanachukua jumla ya mapato yao yote wanatoa jumla ya matumizi yote na salio ndio hutozwa kodi. Kama salio ni - hakuna kodi na kama ni + hutozwa kodi. Salio ni faida(+) ama hasara (-). Kodi hii tunaiita Income Tax yaani kodi ya mapato!

Iko hvyo!
 
Pale benki inapochaji bank charges yaani makato kwa muamala wowote ujue ndio mapato ya benki. Pale ipochaji interest kwenye mkopo ujue ndio mapato ya benki. Makato ya namna yoyote yale kwa ujumla yafanywayo na benki ndio 'REVENUE' yake.

Mwisho wa mwaka wa mahesabu lazima mapato yote hayo yachajiwe kodi tunaita 'income tax' ama corporate tax..

Sasa serikali kama itaamua kuchaji VAT kwenye makato yoyote ya miamala ya kibenki ama taasisi ya kifedha maana yake ni kuwa hio VAT anawekewa anayekatwa. Mwisho wa mwezi benki hupeleka VAT hio TRA kwa kufanya hesabu za ulinganisho wa output na input VAT. Kila mwisho wa mwezi lazima hesabu hizo zifanyike na TRA kupata chao. Mara nyingi unaweza kukuta TRA hawapati kitu yaani wanadaiwa baada ya kufanyika mahesabu hayo ya VAT.

Sasa, serikali inapoamua kuchaji VAT kwa kila muamala wa mteja wa benki kwa namna alivyosema CG-Commissioner General maana yake ni kuwa hio sio VAT bali ni income tax yenye rate ya 18% badala ya 30% inayotakiwa kuchajiwa kwenye corporate businesses! Kwa hio hapo anachoongelea CG sio VAT bali ni income tax.!

Kwa mujibu wa kanuni za kodi za nchi yetu income tax huchajiwa mwishoni mwa mwaka wa mahesabu na VAT huchajiwa kila mwezi. Maana yake ni kwamba serikali iseme jina la kodi hio itakayokatwa kwenye muamala wa mteja lakini wasisema VAT maana sio VAT. Ama kama wamekubaliana na benki; benki wakatwe kwenye miamala wanayoyafanya basi mwishoni mwa mwaka itabidi benki ilipe corporate tax ya 12% maana 18% iliShachukuliwa kwa kila mwezi. Of which kitu kama hiki hakipo kwenye kanuni za ki kodi!

Nilichoelewa ni kwamba. Kwanza, Serikali wanataka kugawana na benki makato wanayokatwa wateja. Tatizo kubwa ni kuwa walidhani jina VAT ndio itatimiliza malengo hayo vizuri, bila kujua namna VAT inavyotakikana kuchajiwa. Pili, naona hawajaangaliana kwa kina kuhusu namna benki inavyopata mapato yake ambayo mwisho wa siku hulipia kodi. Tatu, hakuna namna yeyote ile serikali ikataka kuchaji kodi kwenye hizi miamala za kibenki halafu wananchi wasibebeshwe mzigo. HAKUNA. Nne, Naona Serikali haijabaini kuwa VAT kwenye maisha ya wananchi wa kawaida ndio inaongeza gharama za maisha. Naweza kusema kwa 'jicho la tatu' VAT inasaidia kwa kiwango kikubwa sana kudhoofisha sarafu ya Tanzania kutokana na kutundikwa kwenye bidhaa nyingi zenye watumiaji wa kawaida!

Ndio hivyo!
Ni uchambuzi makini kabisa, umenisaidia kuelewa baadhi ya mambo.
 
Hata sisi hela tunyo peleka bank imeshakatwa kodi, kama ni mshahara umesha katwa
Kama ni mfanya biashara hiyo ni faida yake baada ya kulipa kodi.
Kwanini tukatwe tena kodi wakati tunachukua hizo pesa ambazo zimeaha lipiwa kodi?
 
Asante mkuu unatuelewesha vizuri sana. Naomba kuuliza nipate uzoefu kwa upande wa wafanyabiashara wengine. Ninaponunua kitu kama mteja nakatwa 18 percent kama VAT. Je ni kodi zipi ambazo mfanyabiashara napeleka TRA zaidi ya VAT?
Income tax yaani kodi ya mapato.....hapa sijazungumzia kodi zingine zenye majina tofauti taofauti mfano city levy, SDL na PAYEE kwenye mashahara wa mfanyakazi wako nk nk!
 
Hata sisi hela tunyo peleka bank imeshakatwa kodi, kama ni mshahara umesha katwa
Kama ni mfanya biashara hiyo ni faida yake baada ya kulipa kodi.
Kwanini tukatwe tena kodi wakati tunachukua hizo pesa ambazo zimeaha lipiwa kodi?
Hoja ya muhimu sana hii!
 
Mleta mada umenena vizuri sana nina mashaka na elimu ya kamishna wetu wa mapato...he was not serious
 
Back
Top Bottom