Bandari zetu ni masalia tusikubali nazo zitutoke

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,929
Kesho ni hukumu. Lakini lolote linaweza kutokea. Tuliombee sana taifa huru la Tanganyika.

Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na upendo aliumba vitu viwili, Dunia (ardhi) na mwanadamu. Hivi viwili ndio vinabeba utukufu wake, heza na vyote, chezea vyote lakini sio hivyo viwili.

Madini tulishauza yote. Mbuga na maliasili nyinginezo tumeshagawa zote. Mafuta na gesi sio vyetu japo vipo juu ya ardhi yetu teule. Kuna ile migodi mitatu ya helium tuliyouza kwa dola milion mia sita tu.

Hatuna kingine kimebaki cha kuuza zaidi ya hizi bandari zetu.. Ndio pekee kilichosalia maana hata sisi wenyewe ni kama tumeuzwa tayari.

Bandari zetu ni masalia kwenye tunu nyingi tulizokwisha gawa kwa wageni. Tuzilinde kwa jasho na damu. Kwa machozi na maumivu. Kwa kila hali kwa kila silaha kwa kila mbinu. Bandari zetu zibaki.

Mungu Ibariki Tanganyika. Taifa huru linalogombaniwa kupokonywa hata kile kidogo kilichobaki.

My apology nimeandika na stress.
 
Ila hii serikali inashangaza sana, yaani inakiri waziwazi kwamba imeshindwa kuziendesha bandari zetu ndo maana wameamua kuzitoa kwa waarabu,
Kitu wasichokubali kukiri ni kwamba sio bandari tu hata hii nchi imewashinda kuiendesha, wawapishe wanaoweza
Kitu wasichokubali kukiri ni kwamba sio bandari tu hata hii nchi imewashinda kuiendesha, wawapishe wanaoweza

Wanatangaza mbele ya media kabisa.. Wana shida kubwa upstairs!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ndugu mshana kama viongozi wa juu na chama tawala wameamua kuwa iwe hivyo, wananchi wa kawaida ambao hata mlo wa siku ni shughuli pevu kupata wataweza kupinga nini hapo? Umasikini mbaya sana tajiri anaweza kukunyang'anya hata kile kidogo ulichonacho.
 
Back
Top Bottom