Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,566
- 41,086
Mwalimu Nyerere aliwahi kutamka kuwa CCM siyo baba yangu wala siyo mama yangu.
Wazazi wako, hata ukisema kuwa kuanzia leo ninyi siyo wazazi wangu, ukweli hubakia palepale kuwa hao ni wazazi wako, huna wazazi wengine zaidi ya hao. Lakini hili halipo kwa vyama vya siasa au hata serikali, vitu ambavyo tumevikuta ukubwana, tukaungana navyo kwa sababu tunakubaliana na yale ambayo vyama hivyo vimekubali kuyasimamia.
Kama unaibiwa, ukaipata taasisi inayopigania kuzuia kuibiwa, utaungana nayo, lakini mpo kwenye mapambano ya kuzuia kuibiwa, ukaja kugundua taasisi ile imekengeuka na kuungana na anayekuibia, utaendelra kuwa naye? Wakati wewe unaimba zuia wizi, taasisi inasema linda wizi kwa nguvu zako zote, bado mtaweza kusimama kwenye behewa moja?
Wapo watu ndani ya CCM wanapambana kufa na kupona kuhakikisha bandari zote za Tanganyika zinaporwa na DP.
Wapo watu ndani ya CCM wanapinga kwa sauti kubwa na ya mwisho kulinda rasilimali zetu za bandari.
Wapo watu kwenye vyama vya upinzani, wanapinga kwa nguvu zao zote uporwaji wa bandari zetu.
Lakini wapo wapinzani pia, japo siyo kwa sauti ya juu, wanaunga mkono bandari za Tanganyika kuporwa.
Wananchi tuunganishwe kwa yale tunayoyasimamia.
WanaCCM, wapinzani na wasio na vyama, wasiokubali kuporwa kwa bandari zetu, uhuru wetu na heshima ya Taifa letu, tusimame pamoja kupambania kuzuia kuporwa kwa rasilimali zetu, utu wetu, na heshima ya Taifa letu. Itikadi zetu za kivyama, kidini, kikabila, maeneo, chuki kwa mambo madogo madogo, vikae pembeni, tuunganishwe na jambo moja pekee, ULINZI WA BANDARI ZETU, ULINZI WA HESHIMA YA TAIFA LETU.
Isijalishe lengo hili linafikiwa ndani ya mwezi, mwaka au miaka kadhaa, lakini kamwe tusikubali uhuru wa kufanya maamuzi yetu uliopiganiwa tangu babu zetu akina Mkwawa, Mirambo, Isike, Chabruma, Nyerere, Kawawa, na wengine wengi, leo ufikie kikomo kwa sababu tu DP ana pesa. Leo DP akitaka eneo kuanzia ikulu ya Dar, Azania Front, St Joseph, chuo Chang'ombe; DP akisema naitaka ardhi hii, eti sisi tuitikie 'hewala, tutatekeleza'. Hili kamwe lisikubalike, hata kama ni kwa mtutu wa bunduki.
Leo tukiona DP hatufai, maslahi ya Taifa ni madogo, tukimpata mwekezaji mwingine akawekeze Tanga, eti itabidi tukamwombe DP, akisema hapana, sisi tuseme, 'tumesikia bwana mkubwa, tutatii uamuzi wako'. Kamwe tusikubali.
Tanganyika siyo pori lisilo na mwenyewe,ni nchi ambayo ina watu kamili wenye ubinadamu uliokamilika, ulio sawa na wa mwarabu aliyewageuza babu zetu kuwa bidhaa kama shanga za kuvaa shingoni.
ULINZI WA RASILIMALI ZETU, HAKUNA MJAFALA, HAKUNA WA KUTUHADAA. DAIMA TUZILINDE, NAYE MWENYE KURUHUSU UPORAJI, NI ADUI WA TAIFA LETU.
Chama chetu kikuu cha siasa kwa sasa iwe RASILIMALI ZETU.
Moto zetu itakuwa:
ZIDUMU RASILIMALI ZETU, Tuzilinde milele.
PEOPLES,
Tuzilinde rasilimali zetu.
UHURU
Ni kulinda rasilimali zetu.