Banda la Tanzania, Lang'aa Maonyesho ya ITU Geneva. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Banda la Tanzania, Lang'aa Maonyesho ya ITU Geneva.

Discussion in 'International Forum' started by Pascal Mayalla, Oct 27, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,561
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Ule mkutano wa kimataifa wa Mawasiliano wa ITU, umemalizika leo, huku banda la Tanzania kwenye maonyesho hayo likiwa ni miongoni mwa mabanda yaliyonga'a.

  Banda la Tanzania limeng'aa kwa sababu ni miongoni mwa mabanda yaliyojipanga na yakapangika kwa kuja na timu iliyoongwa na Regulator (TCRA), ila ikaja na watoto wake bila ubaguzi, hivyo kujumlisha wadau kutoka sekta mama, (Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia) ambao aliwakilisha sekta ya umma, huku NGO' zikiwakilishwa na TAYOA na sekta binafsi ikiwakilishwa na Uhuru One, huku TzNic ikiwakilisha utambulisho rasmi wa .tz (dot tz).

  Niwawakea picha kwa hisani ya Muhidin Sufiani wa Sufiani Maphoto.
  *MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKAGUA BANDA LA MAONYESHO LA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA MAWASILIANO WA KIMATAIFA GENEVA

  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Peter Masika, kuhusu namna ya kuwawezesha vijana kutumia teknolojia ya mawasiliano ya kompyuta, wakati akikagua banda la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland jana.
  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tanzania Youth Alliance (TAYOA), Peter Masika, wakati akitazama mashine ya mawasiliano (ICT Mobile Booth), iliyotengenezwa na vijana wa TAYOA, wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU).
  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia mfumo wa kuwasiliana kwa masafa (tele-conference) katika Banda la HUWAWEI, wakati akitembelea mabanda mbalimbali yaliyopo katika maonyesho ya ITU, jijini Geneva, Switzerland.
  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Uhuru One, Mihayo Wilmore, kuhusu matumizi rahisi ya kompyuta ndogo na mpango wa kuzisambaza na kuwawezesha wanafunzi wa Tanzania kutumia kompyuta hizo, wakati wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland.
  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Elimu, Muhwela Kalinga, kuhusu Teknolojia ya mawasiliano katika ufundishaji mashuleni, wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) .
  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Kanda (TCRA), Victor Nkya.
  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Msaidizi wa Mawasiliano Rwanda, Antoine Sebera, kuhusu Teknolojia ya mawasiliano, wakati alipotembelea Banda la maonyesho Burundi,katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland.
  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa Mawasiliano wa Kampuni ya Qatar Assistive Technology Center, Ahmed Habib, ambaye ni mlemavu, wakati alipotembelea Banda la maonyesho la kampuni hiyo katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland.
  [​IMG]
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tanzania Network Information Center, Eng. Abibu Ntahigaye, wakati akikagua banda la maonyesho la Tanzania katika Mkutano wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU) uliofanyika Geneva, Switzerland.
  [FONT=Tahoma, sans-serif]
  [/FONT]​

  Pasco
  Geneva-Uswisi.

  Update 1.

  Ni kawaida kwa watu kudharau cha kwao na kuthamini cha wenzao, nimesema banda la Tanzania langara, nikasema naendelea.

  Nimesema, Banda la Tanzania limengaa kwa sababu zifuatazo, kabla sijazieleza, naomba niwape comparison moja tuu, Nilihudhuria maonyesho ya AGOA yaliyofanyikiwa hoteli ya InterContinental pale New York, kulikuwa na banda la Tanzania likisimamiwa na Wiozara ya Utalii na TTB, nikilinganisha na Banda la Wakenya, Tanzania sio tuu tulionekana kama kituko, bali tulikuwa ni kichekesho!, nilipododosa nikaambiwa ni mambo ya fungu eti hatuna pesa za kushiriki maonyesho ya maana!, wakati huo huo tuu mlolongo wa watu waliokuwemo kwenye ushiriki ni lukuki with nothing to show!, hiyo ilikuwa then.

  Tanzania imeng'aa, kwanza ile Tanzania kushiriki tuu, peke yake ni heshima kubwa, ITU ina wanachama [​IMG][​IMG][​IMG] ambao ni nchi zote wanachama wa Umoja wa mataifa, isipokuwa nchi 3, Vatican, Kosovo na Sudan ya Kusini, ulimwengu wetu una nchi 196. Ukiondoa uanachama wa nchi, ITU ina wanachama wa kisecta [​IMG][​IMG][​IMG] ambao kwa Tanzania ni TTCL, Vodacom na Open Univesity, ukiacha hao, ITU ina washirika [​IMG][​IMG][​IMG] Associates na vyuo [​IMG][​IMG] inavyoshirikiana nao.

  Kwenye maonyesho hayo, Tanzania ni miongoni mwa nchi 25 zilizoshiriki maonyesho ya kitaifa kuonyesha jinsi ICT inavyotumika kuboresha maisha. nchi nyingine za Afrika Mashariki ni Kenya, Uganda na Burundi, wakati nchi za Afrika ni Algeria, Angola, Malawi, Nigeria, Ghana, Namibia, Zambia na Afrika Kusini, hapo kwenye uwakilishi tuu wa Afrika, Tanzania tumejitutumua sana tuu na kujiunga na mataifa makubwa ya Ulaya , Asia na America kama, Argentina, Azerbaijan, Belarus, China, Czech Republic, Japan, Korea, Malaysia, Poland, Spain, na wenyeji Switzerland.

  Kushiriki tuu kwenyewe ni jambo kubwa tosha, ila kikubwa zaidi, sio Tuu, Tanzania, tumeshiriki, bali tumefanya nini katika ushiriki huo na katika mkutano kwa ujumla?.

  Itaendelea.
   
  Attached Files:

 2. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  weka picha.mia
   
 3. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,900
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Hongera tz dot com.
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  yaani hilo banda mgeni aliyelitembelea ni mwenyeji???
   
 5. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,072
  Trophy Points: 280
  that is what also I can see!!!
   
 6. Kwetu Iringa

  Kwetu Iringa JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 359
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Jamani nina swali la kizushi: Nani amewahi kumwona Mama Bilal akitabasaamu???
   
 7. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #7
  Oct 28, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Urongo...
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Pasco

  Sijaona jipya hapo? ITU na TAYOA wapi na wapi?
   
 9. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Nendelea kuchanganyikiwa siku baada ya siku!
   
 10. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Muulize mumewe! Labda faragha inatokea mara moja moja
   
 11. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Usitamani mke wa mtu.
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  afadhali yako mkuu wengine na kuchoka tumeshachoka. Makamu wa Rais eti kuona ubunifu wa watu wake anaenda kuuchungulia nje ya nchi....pathetic, kwa hiyo kama angeulizwa kuhusu haya anayoyaona na mgeni aliyekuja akayaona hapa nchini angesema 'hatuna kitu kama hicho'
   
 13. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Yupi sasa maana ana wawili au mmoja si mke ni sunnah??
   
 14. i

  ibangu Member

  #14
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani Watanzania wameenda Geneva kumwonyesha Mtanzania mwenzao yanayofanyika hapa Tanzania? Tungeonyeshwa viongozi wa mataifa mengine wakiwa kwenye hilo banda.
   
 15. prakatatumba

  prakatatumba JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,337
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu naomba picha zaidi ili kujiridhisha,hususani za raia wa nch nyngne waliotembea hlo banda
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,561
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  Tayoa wanatumia ICT kwa outreach program kwa vijana, wanamitambo ya kufa mtu, na kuzuri zaidi wana helpline ya simu za mitandao yote na kupiga ni bure.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,561
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280

  Ni kawaida kwa watu kudharau cha kwao na kuthamini cha wenzao, nimesema banda la Tanzania langara, nikasema naendelea.

  Nimesema, Banda la Tanzania limengaa kwa sababu zifuatazo, kabla sijazieleza, naomba niwape comparison moja tuu, Nilihudhuria maonyesho ya AGOA yaliyofanyikiwa hoteli ya InterContinental pale New York, kulikuwa na banda la Tanzania likisimamiwa na Wiozara ya Utalii na TTB, nikilinganisha na Banda la Wakenya, Tanzania sio tuu tulionekana kama kituko, bali tulikuwa ni kichekesho!, nilipododosa nikaambiwa ni mambo ya fungu eti hatuna pesa za kushiriki maonyesho ya maana!, wakati huo huo tuu mlolongo wa watu waliokuwemo kwenye ushiriki ni lukuki with nothing to show!, hiyo ilikuwa then.

  Tanzania imeng'aa, kwanza ile Tanzania kushiriki tuu, peke yake ni heshima kubwa, ITU ina wanachama [​IMG][​IMG][​IMG] ambao ni nchi zote wanachama wa Umoja wa mataifa, isipokuwa nchi 3, Vatican, Kosovo na Sudan ya Kusini, ulimwengu wetu una nchi 196. Ukiondoa uanachama wa nchi, ITU ina wanachama wa kisecta [​IMG][​IMG][​IMG] ambao kwa Tanzania ni TTCL, Vodacom na Open Univesity, ukiacha hao, ITU ina washirika [​IMG][​IMG][​IMG] Associates na vyuo [​IMG][​IMG] inavyoshirikiana nao.

  Kwenye maonyesho hayo, Tanzania ni miongoni mwa nchi 25 zilizoshiriki maonyesho ya kitaifa kuonyesha jinsi ICT inavyotumika kuboresha maisha. nchi nyingine za Afrika Mashariki ni Kenya, Uganda na Burundi, wakati nchi za Afrika ni Algeria, Angola, Malawi, Nigeria, Ghana, Namibia, Zambia na Afrika Kusini, hapo kwenye uwakilishi tuu wa Afrika, Tanzania tumejitutumua sana tuu na kujiunga na mataifa makubwa ya Ulaya , Asia na America kama, Argentina, Azerbaijan, Belarus, China, Czech Republic, Japan, Korea, Malaysia, Poland, Spain, na wenyeji Switzerland.

  Kushiriki tuu kwenyewe ni jambo kubwa tosha, ila kikubwa zaidi, sio Tuu, Tanzania, tumeshiriki, bali tumefanya nini katika ushiriki huo na katika mkutano kwa ujumla?.

  Itaendelea.

 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,561
  Likes Received: 18,294
  Trophy Points: 280
  eliakeem, Asante kukifagilia kikoa cha .tz, tufike mahali Watanzania tujivunie kile kikoa cha .tz badala ya kushupalia .com
   
 19. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,900
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  mkulu baadhi ya wa tz ni watu wa ajabu sana. wanapenda .co.uk; .co.za; .com.... lakini hawapendi .co.tz. hata kwa mwenye kaya naye eti ikulu.com aibu iliyoje..... badala ya kuweka mawasilianoikulu.co.tz
   
 20. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #20
  Oct 28, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hongera Mkuu Pasco, leta picha zaidi, namwona kijana wangu Mihayo hapo...
   
Loading...