Banana FM Radio kuna shida

Banana FM Radio kuna shida

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
198
Reaction score
209
Watangazi wa radio ya masafa ya fm ya Banana wameuandikia uongozi wa radio hiyo barua wakiutaka kulipwa mishahara ya ya miezi mitatu vinginevyo watachukua hatua stahiki.

Wametoa saa 72 kwa uongozi uwe umeshalipa mishahara wakidai kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo kushindwa kumudu gharama za maisha.

Uongozi wa radio umewajibu ukidai kuwepo na changamoto ikiwamo akaunti zake kufungwa.
Umeahidi kulipa mishahara wiki ijayo.

Acha tusubirie wiki ijayo maana yajayo yana.
 
Maisha haya! Nyumbani hawaelewi hujalipwa mshahara wanataka chakula mezani tuu.
Hatari sana kwa kweli ,hivi vyombo vyetu vya habari vinachangamoto sana hasa kwenye suala la maslahi ya watumishi.
Watu wakikusikia unatangaza wanajia hauna shida,kumbeeee
 
Back
Top Bottom