EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Balozi wa Zambia Tanzania amesema yule mtu aliyekutwa amefariki kwenye chumba cha hoteli ya Southern Sun baada ya kuhudhuria sherehe ya harusi ni Mzambia. Katika tukio hilo watu wengine wawili waliokuwa wana share chumba kimoja na marehemu walikutwa wakiwa katika hali mbaya. Polisi wamedai walikuwa wamekunywa mno.
Hata hvyo, balozi amesema haelewi ni kwa nini mwili wa marehemu Baster Bahadulu ulichukuliwa Muhimbili na watu waliodai kuwa ni ndugu zake kinyume na taratibu. Hajui kama marehemu alikuwa anaishi hapa nchini na hajapokea taarifa yoyote kwa ndugu wa marehemu hata pale walipoenda kuuchukua mwili wa marehemu Muhimbili.
Jana RPC wa Ilala alisema walionusurika kwenye hilo tukio wako huru na hawatachunguzwa. Hata hivyo, balozi analalamika kwa nini hawajafanyiwa uchunguzi juu ya kifo cha mwenzao ikizingatiwa kuwa wote walikuwa wamelala kwenye chumba kimoja. Marehemu alikuwa Mzambia na alikuja Tanzania mwezi uliopita kwa shughuli za kibiashara. Wawili walionusurika, mmoja ni mwanamuziki na mwingine mfanyabiasha. Wote ni raia wa Uingereza, lakini mmoja wao ana asili ya Kizambia.