Balozi wa Zambia ailalamikia Polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Balozi wa Zambia ailalamikia Polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Aug 2, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Balozi wa Zambia Tanzania amesema yule mtu aliyekutwa amefariki kwenye chumba cha hoteli ya Southern Sun baada ya kuhudhuria sherehe ya harusi ni Mzambia. Katika tukio hilo watu wengine wawili waliokuwa wana share chumba kimoja na marehemu walikutwa wakiwa katika hali mbaya. Polisi wamedai walikuwa wamekunywa mno.

  Hata hvyo, balozi amesema haelewi ni kwa nini mwili wa marehemu Baster Bahadulu ulichukuliwa Muhimbili na watu waliodai kuwa ni ndugu zake kinyume na taratibu. Hajui kama marehemu alikuwa anaishi hapa nchini na hajapokea taarifa yoyote kwa ndugu wa marehemu hata pale walipoenda kuuchukua mwili wa marehemu Muhimbili.

  Jana RPC wa Ilala alisema walionusurika kwenye hilo tukio wako huru na hawatachunguzwa. Hata hivyo, balozi analalamika kwa nini hawajafanyiwa uchunguzi juu ya kifo cha mwenzao ikizingatiwa kuwa wote walikuwa wamelala kwenye chumba kimoja. Marehemu alikuwa Mzambia na alikuja Tanzania mwezi uliopita kwa shughuli za kibiashara. Wawili walionusurika, mmoja ni mwanamuziki na mwingine mfanyabiasha. Wote ni raia wa Uingereza, lakini mmoja wao ana asili ya Kizambia.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Lukuvi, Ndugai, na Zombe wasome huu mkorogo. Inakuwaje mtu anakufa lakini wale waliokuwa nae hawahojiwi kuhusu kifo cha mwenzao? Only in Tanzania!
   
 3. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  baasha imepita hapa sio bure

  mbona mpendazo wamemkamata juzi kwa kesi ya kutishia mtu kwa bastora
  tena kesi yenye imeshaisha

  lakini wanasema mwanasheria mkuu ndiye atahamua hatua za kuchukuliwa na wanasaka mlalamikaji
  japo wanajua walisha malizana

  sasa hapa imekuwaje?

  au kwa sababu wahusika ni raia wa uingereza?
  polisi wana shindwa mahojiano na hao watu? waweke wakalimani
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  EMT

  Hatujaanza leo kuwaachia "wakubwa/vigogo" or their associates..... unakumbuka issue ya mbwa kubaka binti wa kihehe? je umesahau issue ya yule changu aliyeuwawa na mwanajeshi wa Uk?? vipi yule dogo aliyeuwawa pale nyumba za mawaziri kijitonyama/victoria na mambo tiiii??

  Kuna kigogo aliua mtu shambani kwake kimara (tena anahusiana na hiyo harusi.... etc

  tuna clique iliyo juu ya sheria zote za jamhuri

  Hao jamaa walikunywa, wakavuta halafu wakasuguana na sasa mmoja kafa\

  anywau, yote ya shetani tu hayo
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,345
  Likes Received: 19,529
  Trophy Points: 280
  lema ni mwizi wa magari- zombe.....ilibidi nicheke.. hawa askari wengi waache kuvuta magugu haya sio mazuri jamani
   
 6. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mimi nina hakika wameogopa kwamba ni raia wa uingereza ili hali waingereza wenyewe hana mambo ya kutete upuuzi kama huu
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kuona kitu kama hiki mkuu. Hata kama walikuwa wamelewa kiasi hicho, sidhani kama rahisi hivyo kuwaachilia walevi wanzake kiaina.
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kama kigezo kilikuwa ni lugha, itakuwa na maana kuwa mtu anaweza kuja Tanzania na kufanya kosa so long haongezi Kiswahili.
   
 9. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red itself is a criminal offence. So, the police didn't even bother to go in that line as well.
   
 10. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Naona wengi wamesahau jinsi raia wa Uingereza walivyoua dada zetu miaka michache iliyopita na kuwatupa baharini.. Polisi waliwashika vijana hao wa UK, waliwaachia huru bila uchunguzi wowote wa maana. Sasa sijui ndio kuogopa waingereza au ki-english?

  BTW hivi tuna wakalimani kweli kwenye idara zetu kama polisi, uhamiaji nk. maana naona kila mtu yeye songo mbino tu kujifanya anaimanya lugha ya watu lakini ukweli wengi ni kiswahili tu tena hata hicho kiswahili fasaha kuongea na kuandika ni matatizo.
   
 11. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />Mkuu kiingereza ni janga la taifa tena polisi usiseme,watawahoji vipi bora waseme hamna kesi kuficha aibu.Nimeshuhudia trafiki akimwachia mzungu aliyepita rangi nyekundu kisa lugha na kuniachia mimi nilieshuhudia kwa aibu.
   
 12. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hivyo kweli unafikiri hawakutakiwa kutowa maelezo? Na iwapo maelezo na matokeo yanaonyeasha kuwa ulevi ndio kilichowasibu wote kwa pamoja panakuwa na haja ya uchunguzi zaidi? Nafikiri si vizuri kulizarau Polisi kama hivyo! Huyo Balozi anachunga unga wake tu hivyo Wazambia wote wanaokuja Tanzania hupiga ripoti ubalozini? Nikihisi kuwa kule ni sehemu ya kufata huduma inapohitajiwa na kwa kadhia yenyewe ya kuja kunywa pombe hiyo huduma ya kufatiwa haikuwepo.
   
 13. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu hapo kwenye red jibu ni ndio. Kama askari watafanya kazi shady namna hii then kutakuwa na assumptions nyingi sana. Pamoja na mambo mengine uchunguzi wakina ni muhimu; kwa nchi nyingine ungekuta tayari victim's family wamefungua lawsuit.
   
 14. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />
  Mkuu hii si kwa mzungu tu, we ukiona polisi atakuletea gozigozi barabarani tema ung'enge tu, tena unatakiwa uanze kumsalimia wewe na kumhoji kwa nini amekusimamisha yaani wanaondoka bila kuaga maana wengi wao hata kuaga ni kama vile hawajui. Na haichukui mda kukukariri wakikuona tu wanakupungia mkono bila tatizo..
   
 15. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hii ndiyo tanzania tuliyohaidiwa yenye neema,utawala bora na utii wa sheria.time will tell.
   
 16. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Polisi wako kwa ajiri ya kutuonea sisi wazalendo wanyonge,na sio wengine angekuwa mbogo hapo,kwanza angekaa miezi kadhaa ndani pengine hata miaka,ili wafanye uchunguzi hatuna amani kabisa ndani ya hii nchi.
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  No Crime Scene Investigation Lab nchi hii na kama zipo basi hatuna wataaramu tume kaaa kihongo hongo kwanza badala ya kutatua matatizo na hii desturi ya askari kujiamlia whether watapima eneo la tukio au hapana inatoka wapi it has to be on procedures kuwa eneo la tukio hakuna mtu yeyote kuondoa evidence kabla ya CSI-Lab kumaliza kazi zao mtu anakuja tu na ni askari huyo ana contaminate evidence

  My Take :
  Police wetu hawapendi kujishughurisha na kazi zao kikamirifu waaache tabia ya kupenda hongo au kutengeneza mazingira ya kupata rushwa wafanye kazi. Hii ni aibu jeshi la police kuto tumia vifaaa kama inavyo, Hilo tatizo ni kubwa Raia wa nchi nyingine kafa nchini kwenu kiajabu tu nyie mwaichukulia very simple
   
Loading...