Simiyu: Watoto 2 wanyongwa ndani ya chumba cha wazazi, baba akutwa kajitundika mtini

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Mwanaume aitwaye Bundu Ng'habi mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Kata ya Kinamweli wilaya Itilima mkoani Simiyu, amekutwa amejinyonga juu ya mti huku watoto wake wawili mmoja mwenye umri wa miaka miwili na mwingine miaka minne wakiwa wamenyongwa ndani ya chumba cha wazazi wao.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu ACP Edith Swebe, amesema tukio hilo limetolea Agosti 11,2023 majira ya saa 1:00 asubuhi na kwamba mke wa marehemu bado hajulikani alipo.

"Katika tukio hili watoto wawili wamekutwa wamening'inizwa kwenye chumba wanacholala na wazazi wao, ambapo baada ya uchunguzi dalili zote zinaonesha wamekufa kwa kunyongwa, pia mwili wa baba yao mzazi ulikutwa ukiwa umening'inia juu ya mti kwa kujinyonga, tunaendelea na uchunguzi wa tukio ili kuweza kubaini chanzo cha matukio haya lakini tunaendelea kumtafuta mke wa marehemu ambaye mpaka sasa hajulikani alipo," amesema ACP Swebe
 
20230810_105032.jpg
 
Yumkini maisha yake yalizidi kuwa magumu siku hadi siku mke akaondoka kwenda kwa mwenye chochote kitu akiacha watoto chini ya uangalizi wa baba aliyeshindwa kuona mwanga mbele?

Solution akaona ajiue lakini zaidi sana akawaza kuliko kuacha wanae wakiteseka bora aondoke nao,inasikitisha sana.

Mungu awarehemu.
 
Kuwa mbali na Mungu saa nyingine nayo ni shida,inafikia mahali mtu unakata tamaa kabisa kama vile hakuna wa kuweza kukuinuia...
 
Back
Top Bottom