Balozi wa Kenya aishambulia Russia kwa kuyatambua kama majimbo huru ya Ukraine

Hahahhahhahhhahahhahahahhahahahahahhahahhhahahhhahahahahahahhhahahah

putin kawaambia wakenye hiyo ligi ni soo ni kama kutikisa mbuyu unahisi unautikisa kumbe matako yako ndio yanayotikisika

pia kawapa ushauri mzuri wamalize njaa Kwanza
 
Kwa vyovyote vile, Putin na Urusi yake wapo pabaya, ikumbukwe Ukraine ina wanajeshi zaidi ya milioni moja na raia wake wengi wapo tayari kufa kizalendo, ni vigumu sana kuivamia nchi kama hiyo, na wakiamua kulipuana, umwagikaji wa damu utakaoshuhudiwa utaisababishia Urusi hasara kubwa sana hata kama watashinda, na itakua vita ya muda mrefu maana labda wawe na uwezo wa kuua kila mtu kwenye pembe zote za Ukraine.
Hamna kitu cha hatari kama kuvamia nchi ambayo watu wake wana uzalendo nayo, Mmarekani bado hukumbuka kilichomkuta Vietnam.
Ukraine hawana uwezo wa kupambana na the might Russia.Hata Nato nzima hawawezi
JamiiForums-1998190896.jpg
 
Ni waabudu mashetani haokweli kabisa,hiyo ata ukatae!!!
We umeona wapi Jeshi linabatizwa ndio ukubalike!!!na hawabatizi na Bibilia ama Qurani!!
Hao wanajulikana tangu jadi!!

Naye Gaddafi ni dictator na terrorist! Ata nchi yake Libya haijai msamehea!
Alitaka kugawanisha Nigeria mara mbili,(Muslim North Christian South),
Alipochukua Uongozi libya kwa mabavu,aliwaua opposition wote.
Aliwatumania Walibya wote waliyokuwa wametorokea nchi zengine wauawe.
Alikuwa anasaidia waasi magaidi,kwa nchi zengine ambazo hazikuwa zimejiweza.
Kwenye Benki ya South Afrika kuna pesa nyingi aliwekeza,ambazo aliiba Libya,mnyanyasaji wa raia kabisa!!!
Sawa mzee baba
 
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanya mkutano wa dharura baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kusema kwamba sasa anatambua sehemu ya Ukraine kama Urusi na atatuma wanajeshi wake kuwa walinzi wa amani katika majimbo hayo mawili.

Uingereza ilichukua hatua ya haraka kutangaza vikwazo. Urusi ilikemewa na nchi nyingi zikiwemo Mexico, Ireland, Norway, Ghana, na nyinginezo. Lakini ni Kenya ndio iliyojitokeza kwa makali yake kwa jinsi ilivyojibu hatua hiyo ya Urusi.

Balozi wake kwa Umoja wa Mataifa Martin Kimani alitoa hotuba ambayo wengi wamejitokeza kuisifia kama iliyoeleza kwa urahisi na ukali unaostahiki ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa ambao urusi imetekeleza.

"Uhuru wa eneo na mamlaka ya Ukraine yamevunjwa," alisema Balozi Martin Kimani.

"Mkataba wa Umoja wa Mataifa unaendelea kudhoofika chini ya shambulio hilo lisilo na huruma. Kwa wakati mmoja unatolewa kwa heshima na nchi zile zile ambazo kisha zikaupa kisogo katika kutekeleza malengo yanayopinga amani na usalama.... Kenya inasikitishwa sana na tangazo lililotolewa na Urusi la kutambua maeneo ya Ukraine kama mataifa huru'

Aliendelea kusema kuwa Kenya ina wasiwasi mkubwa juu ya athari ambayo Urusi inaweza kuwa nayo ikiwa itaruhusiwa na UN kushambulia na kunyakua nchi zingine.

Mfano wake ni kwamba mipaka ya Afrika ilikubaliwa na nchi zote za huko, licha ya mipaka hiyo kulazimishwa na wakoloni. Alieleza kuwa mataifa ya Afrika yalifanya uamuzi huo badala ya kuwa na vita visivyoisha.

"Tulikataa upanuzi kwa misingi yoyote, ikiwa ni pamoja na rangi, kabila, au kitamaduni," Kimani alisema. "

Baada ya hotuba yake hiyo ,maoni yalianza kutolewa huku akisifiwa kwa hotuba yake hiyo .Watumiaji wa mitandao ya kijamii walituma jumbe za kuonyesha 'makali' ya ujumbe wake na jinsi Kimani alivyojieleza na kuwakilisha msimamo wa kenya kuhusu hatua ya Urusi ;

Balozi Martin Kimani ni nani?

Balozi kimani aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Kudumu wa Kenya katika Umoja wa mataifa mwaka wa 2020 .

Kabla ya uteuzi wake wa hivi punde zaidi, Bw. Kimani alikuwa Mjumbe Maalumu wa Rais wa Kukabiliana na Itikadi kali na Mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Kupambana na Ugaidi nchini Kenya kuanzia Septemba 2015.

Pia aliwahi kuwa Katibu wa Mikakati katika Ofisi ya Mtendaji wa Rais kuanzia Disemba 2018.

Bw. Kimani alikuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa huko Nairobi, Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP) na Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Makazi (UN-Habitat) kati ya Desemba 2012 na Septemba 2015.

Mapema katika taaluma yake, Bw. Kimani alikuwa Mkurugenzi katika Mamlaka ya Kiserikali juu ya Maendeleo (IGAD) nchini Ethiopia, kuanzia Aprili 2011 hadi Disemba 2012.

Bw. Kimani alipata PhD na shahada ya uzamili katika masomo ya vita katika Chuo cha King's College, Chuo Kikuu cha London, mwaka wa 2010 na 2003, mtawalia, na pia shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha New Hampshire mwaka wa 1996

Source bbc swahili

Je, kiutalaamu hili limekaaje ....au ni sawa na sisimizi kumpiga biti tembo
View attachment 2127616
Putin ni mpumbavu anayetumiwa na shetani kufanya uharibifu. Na wanaoumuung amkopo wote ni mapumbavu kama yeye. Wote!.
 
Putin ni mpumbavu anayetumiwa na shetani kufanya uharibifu. Na wanaoumuung amkopo wote ni mapumbavu kama yeye. Wote!.
kwaiyo mto post umefikilia vzur ukakubaliana na ukooo wako upost uu ujingaMtoa POSt unaonaje huu muda ULIOTUMIA kupost huu ujinga wako ungekua unasoma namna ya kutfta pesa kWA kutumia fursa zilizopo mtaan kwako badilika Acha ujinga soma usiwe mtu wa akili za 0.0 yaani zero Brain
 
kwaiyo mto post umefikilia vzur ukakubaliana na ukooo wako upost uu ujingaMtoa POSt unaonaje huu muda ULIOTUMIA kupost huu ujinga wako ungekua unasoma namna ya kutfta pesa kWA kutumia fursa zilizopo mtaan kwako badilika Acha ujinga soma usiwe mtu wa akili za 0.0 yaani zero Brain
Zero brain ni wote wamuungao mkon0 putin na watu w usiyejua thamani ya general knowledge kwenye mafanikio. Wote, pumbavu.
 
Hii umeandika kwa mihemuko kwa sababu mkenya mwenzako karopoka huko. Hao raia waliotayari kupambana mbona wanakimbia mpaka

Hiyo ni kawaida kwa raia kutaharuki pale kuna tishio la vita vikuu, na watakimbia wengi, ila fahamu vita kama hivi huishia kuwa "war" badala ya "fight", maana Mrusi akilazimika kufanya carpet bombing huko Ukraine, atawaua raia kwenye nchi yao na kuanzia hapo ndio huwa tunaita "shit hitting the fan".
Hata Putin mwenyewe anajua vitamgharimu kishenzi, hapa bado anajaribisha kupima kina cha maji.
 
Back
Top Bottom