Balozi wa china: Sijavunja mkataba wa vienna

Balozi wa china: Sijavunja mkataba wa vienna

Akili za kiccm za akina ze marcopolo & company mtakuja kutuletea adi al shabab wakafanya mauaji lakini mkimbiwa mtasema udaku. Si vema mtu uliumbwa na akili timamu kujitoa akili.
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU.

Hii statement umeishaitoa mara nyingi sana huku ukiachana na hoja iliyopo, japo magazeti ya udaku yalishawahi kuandika kashafa fulani kuhusu kiongozi fulani wa upinzani uliishabikia sana.
 
Balozi wa "nchi"anapopokelewa na askari wa "chama"............ndio maendeleo hayo?

IMG_2791.JPG
 
kuna hoja zikitolewa na mbunge wa upinzani, kwa kuisikia tu unajua msemaji ameandaliwa maneno na tundu lissu. pia kuna hukumu zinazo tolewa na kiti cha bunge kwa kusikia tu unajua zimetoka kwa lukuvi. maelezo ya balozi huyu yana u nape nape mwingi
 
Huyo Mchina kweli ni majanga! Kuelezea umma nini serikali yake imefanya mpaka aende kwenye mikutano ya CCM!
 
Kuendelea kujadili rangi ya kofia aliyovaa balozi wa China ni ukosefu wa hamu ya kujadili mambo ya maendeleo.

Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...

Call a spade a spade.... kama balozi wa Iran akipanda kwenye mkutano wa hadhara wa CUF akiwa amevaa sare ya cuf na akasema neno moja tuu "hakiiii!!!!!!!!!!'' au balozi wa Marekani akapanda jukwaa kwenye mkutano wa chadema akiwa kavaa tshirt ya M4C akasema, ''peoples......!!!!" Vipi tungejadili rangi ya Tshit au kofia.!???
CCM ni chama tawala na chama kilichokomaa kwa hili lina ukakasi na wote waliohusika walijikwaa busara ni kuomba radhii..?!! Je kama CCM inafanya hivi vyama vingine vikiiga polisi na hao usalama wa taifa watawaangaliaa?!!!

ACHA UNAFIKI.....
 
Simply Balozi wa china hana adabu kabisa ametudharau sana watanzania inakuwaje aende kuongea habari za maendeleo ya nchi yetu kwani hiyo ni kazi yake mpuuzi kama Kinana na Nape waliompa ujiko wa kusimama majukwaani na kuanza kuwasonga wananchi na maneno ya uchimvi ovyo kabisa yaani mpaka sasa hivi anaendekeza kiburi kwa sababu wachina waliopo hapa wamemwambia watanzania hatuna akili he has to leave
 
Anasema wanaomlaumu wanamkatisha tamaa kutusaidia kuondokana na umasikini!! Hii ndio kazi ya Balozi wandugu? Hata kama sisi ni masikini kwa hiyo hao wawekezaji wanatusaidia sisi? Kwenye nini? Ajira? Junior staffs? Daily contract workers? Kuna vitu ukiviangalia kwenye nchi hii unaona kabisa waafrika kuja kuendelea labda siku ya kiama maana nikijaribu kusoma speech ya kaburu Botha naona kuna ukweli mkubwa sana. In short ningekuwa mimi nadhani wao na vihela vyao wangekoma kuingilia mambo ya sovereign country kwa mgongo wa matusi wanayotukana eti anatusaidia kuondokana na umasikini. Nadhani ni bora angekaa kimya kuliko kubishia ukweli akidhani nchi hii haina wenye ufahamu.
 
eti alivalishwa na bibi kizee je angevalishwa gauni angekubali amakweli ukiambatananao utakuwa kama wao
 
Huyu Balozi nafikiri ama anafanya makusudi kwa sababu anajua hakuna atakachofanyiwa au ni mbumbumbu. Lakini nafikiri la kwanza ni sahihi zaidi. Tatizo wala si kuvaa kofia Bali kushiriki katika mikutano ya siasa na kutoa kauli zinazoashiria kuunga upande mmoja wa siasa. Hii si china yenye chama dola na kimoja. Nina hakika anajua kabisa Balozi wetu nchini china akiudhuria mkutano wa siasa wa wapinzani huko china atafungashiwa Vilago Mara moja. Hata akitoa kauli tu ya kuitaka serikali ya china kufuata haki za binadamu atafukuzwa mara moja.

Kauli hii ya huyu Balozi inaniaminisha kuwa onyo lililotolewa na wizara ya mambo ya nje (Kama kweli lilitolewa) halikuwa Kali la kutosha. Kawaida alipaswa kuitwa na kupewa onyo. Pengine ameaminishwa kuwa aliyotenda ni sahihi.

Sababu kwamba yeye ni mfanya biashara nayo ina walakini. Yeye Kama Balozi hakuja kufanya biashara, Kama ni hivyo anatakiwa awe na idhini hiyo ya kufanya kazi. Kinyume chake ilo ni kosa lingine. Kama ni kuwatafutia fursa watu wake wa china za biashara hawezi tumia mikutano ya siasa wala wanasiasa wetu, ama kwa taasisi zaomza kisiasa au mmoja mmoja kwa maslahi Yao ya kisiasa.
 
Issue hapa siyo kuwa yupo tayari kushirikiana na NGO wala chama issue ni kuwa alichofanya ni kosa.period!Jana nimemuona kwenye TV amehamaki mbaya anajaribu kujikosha kwa watanzani.......mesage sent and delivery yeye asubiri hatima yake.:A S 41:
 
Kwa hiyo huyu balozi anataka kutuaminisha kuwa Waziri wetu wa mambo ya nje mh Membe ambaye ikitokea akioteshwa na mungu atagombea urais 2015 ni mwongo?
 
aache utani huyo! jana nmeona vjana wa ktaa wamemvalsha mbwa t_shirt la ccm lenye pcha ya kilanja mkuu! wakamfunga eneo la mkutano wa chama. nae mchna anazake kofia za COWBOY hazpo?
 
Tanzania daima ni gazeti la kufungia vitumbua tuuu

Umenichekesha sana. Yani umenunua kifurushi, ukatafuta search engine, ukaingia jamii forum, ukalog in halafu unaandika comment hii. Pengine kuna tatizo la msingi mahali fulani
 


[TD="bgcolor: #FFFFFF"]PAMOJA na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kusema kuwa Balozi wa China nchini, Lu Youqing, amekiuka mkataba wa kimataifa wa Vienna kwa kujihusisha na siasa za CCM, balozi huyo ameibuka na kudai kwamba yuko tayari kufanya kazi na chama chochote cha siasa.
Kwa mujibu wa Youqing, yuko tayari kufanya kazi na asasi binafsi (NGO’s) au taasisi nyingine yoyote yenye lengo la kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.
Balozi Youqing alitoa kauli hiyo jana, akijibu mjadala ulioibuka hivi karibuni baada ya kuonekana akihutubia kwenye jukwaa la Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, mkoani Shinyanga.
Akieleza sababu za kupanda kwenye jukwaa la CCM, akiwa na kofia ya chama hicho, balozi huyo alisema ziara yake haikuwa ya kisiasa bali ilikuwa na lengo la kuwapa elimu wakazi wa mkoa huo ili waone umuhimu wa uwekezaji wa viwanda vitatu vya pamba, vilivyojengwa na Serikali ya China.
Alisema uwekezaji wa viwanda hivyo ulitokana na ombi la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyeiomba China kujenga viwanda hivyo ili kuongeza thamani ya zao hilo kwa mkulima.
“Hata Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alipokuja China, alifanya mazungumzo na wawekezaji wa China kuhusu miradi hiyo, na mimi kama msimamizi wa Serikali ya China, nikaona nitumie fursa hiyo kuzungumza na wananchi wa mkoa huo,” alisema.
Alisema baada ya miradi hiyo kukamilika, mwaka jana uzalishaji wa zao la pamba ulishuka, hivyo aliona atafute nafasi ya kuzungumza na wakulima hao kuwaeleza faida na umuhimu wa uwekezaji wa zao hilo.
“Kwa hiyo nilikuwa na mpango wa kwenda kuzungumza na wakulima wa pamba Shinyanga, ilipotokea CCM wana ziara mkoani humo, niliona ni bora nitumie nafasi hiyo kuzungumza na wananchi wengi waliofika ambao pengine nisingeweza kuwapata kwa wingi ule.
“Nilichozungumza ni kuhusu uwekezaji wa China mkoani humo, hapa tatizo liko wapi?” alihoji.
Alisema haoni kama amekiuka mkataba wa Vienna kwani hakujihusisha na siasa za kuinadi CCM kama inavyotafsiriwa na wengi.
Kuhusu kofia aliyovaa akiwa jukwaani na Kinana, balozi huyo alisema alivishwa na bibi mmoja wakati wakielekea kwenye mkutano na hakuona sababu ya kuacha kuivaa.
“Ile kofia nilivishwa na bibi mmoja mzee sana. Alinisimamisha, akaivua kofia yake kisha akanivisha wakati naenda jukwaani. Nilipenda ukarimu wake na ndiyo maana nilipanda nayo jukwaani,” alisema.
Balozi huyo alilaumu baadhi ya vyama vilivyovalia njuga suala hilo kiasi cha kumkatisha tamaa, kwani lengo lake ni kutaka kuhakikisha Tanzania inakuza uchumi wake na kila mtu awe na maisha bora.
Licha ya kujitetea, Septemba 12 mwaka huu, balozi huyo alihudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika uwanja wa Shycom na baadaye katika eneo la mnada wa Mhunze, Jimbo la Kishapu.
Balozi huyo alitambulishwa kwa wananchi na Kinana, kisha kuwahutubia akisema China imevutiwa na sera za CCM, hivyo watawekeza katika soko la pamba katika mkoa huo.
Ni katika mkutano huo, balozi huyo alicheza nyimbo za CCM za kubeza vyama vya upinzani huku akiwa amevaa kofia ya chama hicho.
Kitendo hicho kilikemewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kikielezwa kuwa kinakiuka mkataba wa kimataifa wa kidiplomasia.

Chanzo: Tanzania Daima



[TD="bgcolor: #FFFFFF"]
Balozi wa China akinzana na wizara


Na Mwandishi wetu



[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][/TD]
[/TD]
[/QUOTE]

Na Sikafu alilazimishwa kuvaa na nani na kuna sehemu ameonekana anakagua gwaride la chipukizi na sehemu nyingine akicheza ngoma na Kinana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom