Balozi wa china: Sijavunja mkataba wa vienna

Balozi wa china: Sijavunja mkataba wa vienna

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2010
Posts
855
Reaction score
1,224

[TD="bgcolor: #ffffff"]PAMOJA na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kusema kuwa Balozi wa China nchini, Lu Youqing, amekiuka mkataba wa kimataifa wa Vienna kwa kujihusisha na siasa za CCM, balozi huyo ameibuka na kudai kwamba yuko tayari kufanya kazi na chama chochote cha siasa.
Kwa mujibu wa Youqing, yuko tayari kufanya kazi na asasi binafsi (NGO’s) au taasisi nyingine yoyote yenye lengo la kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.
Balozi Youqing alitoa kauli hiyo jana, akijibu mjadala ulioibuka hivi karibuni baada ya kuonekana akihutubia kwenye jukwaa la Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana, mkoani Shinyanga.
Akieleza sababu za kupanda kwenye jukwaa la CCM, akiwa na kofia ya chama hicho, balozi huyo alisema ziara yake haikuwa ya kisiasa bali ilikuwa na lengo la kuwapa elimu wakazi wa mkoa huo ili waone umuhimu wa uwekezaji wa viwanda vitatu vya pamba, vilivyojengwa na Serikali ya China.
Alisema uwekezaji wa viwanda hivyo ulitokana na ombi la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyeiomba China kujenga viwanda hivyo ili kuongeza thamani ya zao hilo kwa mkulima.
“Hata Katibu Mkuu wa CCM, Kinana alipokuja China, alifanya mazungumzo na wawekezaji wa China kuhusu miradi hiyo, na mimi kama msimamizi wa Serikali ya China, nikaona nitumie fursa hiyo kuzungumza na wananchi wa mkoa huo,” alisema.
Alisema baada ya miradi hiyo kukamilika, mwaka jana uzalishaji wa zao la pamba ulishuka, hivyo aliona atafute nafasi ya kuzungumza na wakulima hao kuwaeleza faida na umuhimu wa uwekezaji wa zao hilo.
“Kwa hiyo nilikuwa na mpango wa kwenda kuzungumza na wakulima wa pamba Shinyanga, ilipotokea CCM wana ziara mkoani humo, niliona ni bora nitumie nafasi hiyo kuzungumza na wananchi wengi waliofika ambao pengine nisingeweza kuwapata kwa wingi ule.
“Nilichozungumza ni kuhusu uwekezaji wa China mkoani humo, hapa tatizo liko wapi?” alihoji.
Alisema haoni kama amekiuka mkataba wa Vienna kwani hakujihusisha na siasa za kuinadi CCM kama inavyotafsiriwa na wengi.
Kuhusu kofia aliyovaa akiwa jukwaani na Kinana, balozi huyo alisema alivishwa na bibi mmoja wakati wakielekea kwenye mkutano na hakuona sababu ya kuacha kuivaa.
“Ile kofia nilivishwa na bibi mmoja mzee sana. Alinisimamisha, akaivua kofia yake kisha akanivisha wakati naenda jukwaani. Nilipenda ukarimu wake na ndiyo maana nilipanda nayo jukwaani,” alisema.
Balozi huyo alilaumu baadhi ya vyama vilivyovalia njuga suala hilo kiasi cha kumkatisha tamaa, kwani lengo lake ni kutaka kuhakikisha Tanzania inakuza uchumi wake na kila mtu awe na maisha bora.
Licha ya kujitetea, Septemba 12 mwaka huu, balozi huyo alihudhuria mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika uwanja wa Shycom na baadaye katika eneo la mnada wa Mhunze, Jimbo la Kishapu.
Balozi huyo alitambulishwa kwa wananchi na Kinana, kisha kuwahutubia akisema China imevutiwa na sera za CCM, hivyo watawekeza katika soko la pamba katika mkoa huo.
Ni katika mkutano huo, balozi huyo alicheza nyimbo za CCM za kubeza vyama vya upinzani huku akiwa amevaa kofia ya chama hicho.
Kitendo hicho kilikemewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kikielezwa kuwa kinakiuka mkataba wa kimataifa wa kidiplomasia.

Chanzo: Tanzania Daima



[TD="bgcolor: #ffffff"]
Balozi wa China akinzana na wizara


Na Mwandishi wetu



[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
[/TD]
[/TD]
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU.
Ndio umefikiri mpaka mwisho hapo. Ungefuatilia katika taarifa ya habari ITV leo pia ungesema Balozi wa China ni Mdaku, ITV ni chombo cha Udaku maana ameonekana na kusikika akizungumza hayo.
 
Ndio umefikiri mpaka mwisho hapo. Ungefuatilia katika taarifa ya habari ITV leo pia ungesema Balozi wa China ni Mdaku, ITV ni chombo cha Udaku maana ameonekana na kusikika akizungumza hayo.

Kuendelea kujadili rangi ya kofia aliyovaa balozi wa China ni ukosefu wa hamu ya kujadili mambo ya maendeleo.

Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
 
Kuendelea kujadili rangi ya kofia aliyovaa balozi wa China ni ukosefu wa hamu ya kujadili mambo ya maendeleo.

Inatakiwa ajifunze kazi za kibalozi na si kufanya kazi za Uenezi za CCM, kama Shonza, Mwampamba na Tambwe Hiza. au kama anataka kufanya kazi ya CCM aombe kazi Lumumba tu.
 
Mi naona we ndio mdaku pia mnafiki.

Hahahahahahaha

Kiongozi, mbona unanichekesha sana. Yaani habari imeandikwa na Tanzania Daima lakini lawama napewa mimi!!!

Ama kweli Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
 
Duh we pia hazijatimia, hivi huwa mnakula vitu gani hadi vinawafanya muwe wajinga namna hii? Au mmelogwa?

Uhusiano huu kati ya China na CCM umeanza kuwekwa wazi kupitia kwa Mwenezi wa CCM aliyepo ubalozi wa China. Taarifa za Bomu la Soweto kutoka China, vifaa vya uenezi vya CCM vyenye bendera na kadi za cdm kutoka China, Kofia ya Mwigulu ya Red Army ya China. Hakuna siri tena
 
Hii ni dharau ya wazi ya huyu dickless Chinese, sasa anadhani kua umaskini wa kifikra wa viongozi wetu unaweza kutumiwa vyovyote na hata kuwaongoza 'wasomi maandazi' kama akina Ze Marcopolo huko Lumumba nini cha kufikiri. Hii ni dalili mbaya na ya wazi kuwa Chinese sio development partners wa ukweli bali ni mafia wanaotoa protection money kwa tabaka tawala na kuwaibia watz. Nakumbuka madai ya 'CCMAsili' na mengi kati yao yanaleta mantiki.
 
Hata saa mbovu ya ukutani, huwa inasema kweli mara mbili kwa siku.

images

Hahahahahahaha

Kiongozi, mbona unanichekesha sana. Yaani habari imeandikwa na Tanzania Daima lakini lawama napewa mimi!!!

Ama kweli Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
 
It doesn't matter whether the incident has been reported by the udaku tabloid or not. This ambassador has revealed how ignorant and foolish he could be.
The next thing he will be participating in drafting the Constitution of this nation.
 
Lack of jusdgment, kusema kwamba hakukuwa na njia nyengine ya kuwavuta wananchi walio wengi ila kwa mkutano wa ccm naona amekosa hekima ya kufanya maamuzi. Jee alijaribu kufanya attempts zozote za kuiomba serikali kufanya utaratibu wa kuzungumza na wananchi? Jee kauli zake za kuifagilia ccm pale nayo vipi au alilazimika kwa hisani aliopewa na Kinana? Hoja hapa sio nia yake ya kuzungumza na wananchi juu ya agenda ya soko la pamba, hoja ni route aliotumia ambayo obvious imeonekana kwanza kuwagawa wananchi kutokana na itikadi za siasa katika masuala ya uchumi kwa wananchi wote, pili kuwapigia debe ccm kwa kivazi na hata kauli yake. Tatu ni kuitia katika mtikiso relationship ya china na Tanzania, hawezi kuwalaumu wanasiasa kwa sababu japo alikuwa na nia njema lakini route aliotumia haikuwa sawa. Sijaona utetezi wake wa kusema hakuvunja mkataba wa viena, kwa sababu hatutamjadili kwa sababu ya nia yake, vitendo ndio vinavyojadiliwa. Na alitegemea nini katika mikusanyiko ya vyama vya siasa hususan vijijini kwamba wazee wasingelimpa kofia ya chama, cha msingi hakukuwa na haja ya kushiriki katika mikusanyiko ya aina hii kutokana na vulnerability yake na kwa nafasi yake. Tukubali alikosa diplomatic judgement.. Anajiwashia moto zaidi kuvilaumu vyama vya siasa kwa kosa lake mwenyewe..
 
Ni upuuzi mtupu kumtetea huyu balozi. Mimi nauliza wako wapi Interpol walioshadadia kumbeba kijana Odong' Kefas Silas Odwar wa kaskazini mwa Uganda aliyekuwa anasoma kitivo cha Sheria UDSM? Baada ya kukutwa na kadi ya kushikishwa ya CCM? Alipelekwa chini ya ulinzi mkali na kubatizwa jina la jasusi mwanafunzi mwenzetu huyo eti baada ya kupata influence kubwa ya wanaUDSM katika uchaguzi wa urais wa chuo kikuu hicho na kuweka bayana mkakati wake wa kutumia nafasi hiyo kuihoji serikali ni jinsi gani jamii ya UDSM inafaidika na uwepo wa makaburu wanaomiliki Mlimani city katika eneo la chuo? Hili halikuwapendeza CCM wakaanza kuhaha hadi mzee asiye na busara Ngombalemwiru alishiki vita dhidi ya mwanaharakati yule. Nakumbuka walidai hata vyeti alifoji lakini aliwanyamazisha alipoleta vyeti vyake kutoka London alikokuwa akiishi baba yake . Haikutosha wakazusha kuwa ni mtoto wa aliyekuwa kiongozi wa waasi kaskazini mwa Uganda Joseph Konyi. Walipoona hilo halina nguvu wakambambika kadi ya CCM ikawa ndio sababu ya kumuondolea haki ya kuendelea kusoma nchini kwamba kajihusisha na shughuli za kisiasa. Ninakumbuka Odong' aliwahi kutangaza hadharani kuwa CCM na serikali yake ni wazembe kwani ktk harakati zao za kutafuta wanachama vyuo vikuu walizigawa kadi zao hadi kwa raia wa kigeni. Je Odong' na huyu mchina nani anastahili kufukuzwa nchini? Au wale waliombeba Odong leo hawoni hili? Kweli magamba yameenda mbali zaidi hadi kwenye ubongo ni hatari sana . Naomba kuwasilisha.
 
Kweli china mambo mengi ni feki, mpaka balozi wao ni wa kichina! Anazidi kuwalaumu wanasiasa wa upinzani na kukumbatia wa ccm, tayari huyu balozi yuko yuko upande mmoja ambalo ni kosa kwa afisa wa diplomasia! Ccm imemvuruga huyo balozi hata bila mwenyewe kujua!!
 
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU.

yawezekana kweli nigazeti la udaku kama unavyosema kilasiku,lakini waweza jisumbua kutuonyesha udaku wake as far as this issue is concerned?je niuongo kuwa barozi huyu alivaa kofia ya ccm,akapanda jukwaa la ccm, name akaisifia ccm?
 
Huyu balozi ni mbumbumbu mwenye kiburi na hana hata basic skills za diplomacy.Nilitarajia angeomba radhi

Kama Waziri Mkuu alifanya mazungumzo iweje asitumie platform za serikali?

Hakuna justification yoyote ya kuvunja sheria ! Ina Maana ukarimu wa bibi kizee ndiyo uliomsukuma kuvunja sheria na hata kutamka maneno aliyotamka?

Nadhani sasa huyu achukuliwe hatua kali zaidi.
 
Back
Top Bottom