Balozi wa afya ya akili

Nov 2, 2020
68
90
Habari wakuu,

Vijana wetu hususani walio shule ni miongoni mwa wanaosumbuliwa na matatizo ya afya ya akili, ikiwemo KHOFU ILIYOPITILIZA.

Kwenye maisha khofu ni jambo la kawaida, lakini inapotokea inazidi kiasi mtu anashindwa kufikia ndoto zake anazotarajia, hii inahesabika kama tatizo.

Kuna mwanafunzi akisikia neno mtihani ni kama amewekewa bunduki kichwani. Sikwambii akiuona physically mbele yake.

Kuna mwanafunzi si kwamba hawezi au hapendi somo, lakini kutokana na khofu ambayo inaweza kusababishwa na vitu vingi, anaweza akashindwa kufaulu vizuri, wakati mwingine anaweza akawa katoka nalo somo hilo kidato fulani, lakini ukashangaa kabadilika ghafla tu anafeli.

Bahati mbaya si kila shule ina kitengo maalum kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi na vijana wetu kisaikolojia tofauti na walimu wetu ambao wamepata elimu hiyo kama sehemu tu ya somo wakati wa mafunzo yao.

Kuliona hili, Taasisi ya Mental Health Tanzania, yenye makao yake makuu jijini Mwanza, Tanzania kupitia idara yake ya Klabu za Afya ya Akili imejizatiti kuwa mstari wa mbele kumsaidia kijana aliye shule kwa kufungua klabu.

Kupitia Klabu hizi, wanafunzi watafundishwa mengi kuhusu afya ya akili, magonjwa ya afya ya akili pamoja na mbinu gani wanaweza kuzifanya kujisaidia na kuwasaidia wenzao kwa hatua ya awali kutokana na matatizo yanayowasumbua.

Inawezekana unaesoma hapa ni mwalimu wa kawaida, mkurugenzi wa chuo au shule fulani au taasisi yeyote ya elimu na pengine unaweza kuwa mwanafunzi au mzazi ambae tutashirikiana kusimama kama balozi wa afya ya akili na ukawa tayari kufungua Klabu hii katika taasisi yako.

Tafadhari tuwasiliane ili nikupe muongozo wa jinsi gani unaweza kukamilisha usajili huo.

NINA IMANI VIJANA WANATUHITAJI KAMA TUNAVYOWAHITAJI, TWASAIDIE
 
Back
Top Bottom